MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,443
Baada tu ya TANESCO kuanza mgao wao wa siku 9,ghafla kampuni ya kimarekani ikaibua na kununua mitambo ya Dowans.Huu ni mchezo wa kuigiza ambao hauhitaji elimu yoyote kuushtukia,TANESCO kama vile hawajui kuwa hii SYMBIONS ni DOWANS ileile wanajifanya kuchangamkia kuingia nayo mkataba!!Ifikie wakati serikali na TANESCO wajue kuwa watanzania ni kweli tuna shida ya umeme ILA SIO HUU WA DOWANS WALA PACHA WAKE SYMBION.Kwani hiyo mitambo ya Dowans ni lazima ifanye kazi Tanzania???Kwanini hao Dowans watoto wasiende kuuza umeme wao Msumbiji,Kongo na kwingineko ambako mitambo hiyo haijachafuka????kwanini iwe Tanzania.Hatuhitaji kupotezewa muda wa kulumbana katika hili,"Nyoka akivua gamba sumu yake huongezeka ukali maradufu"!!!Hawa symbion ni Dowans walelwale waliojivua gamba!!!Hatuutaki umeme wao,bora mtuache na giza kuliko kutuhadaa kwa mbinu nyepesi za mgao wa siku tisa halafu mnaichukua Dowans kiujanja ujanja!