Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,479
- 40,120
Dunia ya leo inakwenda kwa kasi sana wakati sisi tunawaza either tukimbie au tutembee.
Nishati ya umeme ni eneo muhimu sana leo kiuchumi na kiusalama kwa maisha yote ya binadamu. Lakini sisi Watanzania ni kama wataalam wetu na baadhi ya wanasiasa wameamua nishati hiyo ni eneo la kutuumiza ama wanafanya uzembe uliopitiliza unaotugharimu kodi zetu na uchumi wetu.
Hapa karibuni, mkurugenzi wa TANESCO aliutangazia umma kuhusu mgao wa nchi nzima kwa sababu alizozitoa kuwa wanarekebisha vituo vya kupooza umeme vya Kinyerezi na Ubungo kuviongezea uwezo. Ukiangalia body language ya Mkurugenzi hana shaka kabisa na anachokisema kitaleta athari namna gani kwenye jamii hususani kwenye uchumi wetu. TANESCO yetu tangu kale walikosa uwajibikaji hadi alipokuja Magufuli ambapo suala la umeme kukatika liligeuka historia.
Nina maeneo machache ya kujengea hoja, inawezekana THINKERS wa JF mkawa na mtazamo ama.maeneo mengine zaidi.
1. HUJUMA
Kuna uwezekano mkubwa TANESCO ikawa inatumika kuhujumu serikali na Wananchi kwa manufaa ya wachache. Inawezekana pia ikawa inatumika kuhujumu legacy ya mtawala aliyepo madarakani.
Pia hujuma inaweza kwenda mbali zaidi kwa kuhusishwa na mashirika makubwa yanayotaka kusambaza vifaa vya nishati mbadala kama vile Majenereta, vifaa vya Sola na kadhalika
Katika HUJUMA tusisahau kuhusu vita ya uchumi ambapo sisi Watanzania tuna dawati la uchumi kwenye Idara yetu ya Ujasusi wakati wenzetu wanaopambana nasi wana taasisi kamili ya ujasusi wa uchumi/ nje ambao wanahakikisha wanadhoofisha juhudi zozote za kiuchumi za mataifa kama yetu. Inawezekana kukawa na hoja nyingi kwenye eneo hili
2. UZEMBE
Wizara ya Nishati na shirika la ugavi ni kama wamefunga ndoa ya kulindana daima dumu. Serikali hupitisha bajeti ya wizara ambapo kwenye lots zake kuna fungu la matengenezo na ukarabati lakini miaka karibia yote kumekuwa na mgao wa sababu ya uchakavu wa mitambo na miundombinu.
Miaka fulani huko nyuma, TANeSCO waliagizwa kubuni mfumo pokezi (backup plan) kuwa endapo moundombinu inazidiwa na kuzima umeme, basi mfumo pokezi uwashwe ili kukidhi upatikanaji wa umeme wakati matengenezo yanafanyika kurejesha mfumo-kati wa umeme. Lakini hili halipo kwenye utekelezaji wao. Tanesco na Wizara wanapaswa kubadilika na kutatua hili tatizo kwa bidii zote kwani umeme ni uti wa mgongo wa uchumi wetu. Inapofikia mahala mpaka Rais anapanda ndege kwenda kushawishi wawekezaji kuja nchini ina maana lazima tuhakikishe upatikanaji wa umeme wa uhakika wa umeme. Hivyo hizi kata funua za TANESCO ni kufifisha juhudi za rais bila kujali gharama zinazotumika kuvutia wawekezaji.
3. KUTUMIKA KISIASA
Katika moja ya matukio mazito yaliyowahi kuikumba nchi yetu, ukiondoa la kufariki kwa Magufuli, ilikuwa ni kujiuzulu Bungeni kwa Waziri Mkuu kutokana na kashfa ya mitambo ya ufuaji umeme kupitia kampuni ya RICHMOND ambapo pamoja na yote inaonesha behind kulikuwa na mkono wa Serikali ya Marekani (gizani) kwani baadaye RICHMOND ililuja kununuliwa na kampuni ya SYMBION POWER iliyokuja kuzinduliwa na Rais wa Marekani Barak Obama na sasa Symbion imenunua mitambo mingine yenye utata wa kashfa ya IPTL...
Pia miezi michache baada ya kufariki JPM, mwanasiasa Zitto alizungumza kuhusu umeme kutokatika enzi za utawala wa awamu ya tano kwa sababu Rais aliamuru viwanda vipunguziwe matumizi ya umeme na umeme upelekwe kwa wananchi na hivyo kusababisha kuporomoka kwa uzalishaji na viwanda vingi kufungwa. Alichoshindwa kuoanisha na tamko lake ni kwamba, mpaka Magufuli anafariki uchumi wetu ulitupeleka kwenye nafasi ya uchumi wa kati kutoka kwenye uchumi wa chini. Hapo kama ni mdadisi unapaswa kuhoji nini kilipelekea uchumi kukua kwa kuzingatia uzalishaji ulishuka sana kipindi cha Jiwe? Hivyo hoja ya Zitto na kwa namna anavyozidi kujipambanua hivi karibuni, ilikuwa na lengo la kuguandaa kisaikolojia kwa yanayokuja mbele kwenye hii tasnia ya nishati. Nadhani haiusiani na tuhuma za baadhi ya wanasiasa kushinikiza kulipwa fedha na mawaziri wa Nishati ili wasiwaibulie kashfa mbakimbali.
Kisiasa TANESCO ni mwiba mkali siyo tu kwa mawaziri bali pia hata kwa rais aliyepo madarakani.
4. TANESCO INAONGEA UKWELI
ukiondoa hoja zote hapo juu, inawezekana ni kweli TANESCO inapitia wakati mgumu kwa kuzingatia
-Kutopewa fungu la ukarabati
-Maombi ya ukarabati kutozingatiwa
-Udhibiti wa mapato n.k.
Hivyo ili twende mbele inatakiwa tuangalie kwa nini shirika hili ambalo wateja wake wanalipia huduma zake zote kabla hawajatumia linakwama katika kuboresha huduma zake.
Shirika lisaidiwe kwa kuunda sheria mpya ya uanzishwaji wa shirika ama kuligawanya kimajukumu ama kulibinafsisha ili serikali ibaki kuregulate tu.
MAWAZO BINAFSI
Kutokana na sababu mbalimbali nilizoweka hapo juu, ninafikia kuwaza kwamba yafuatayo yanaweza kufanyika
1. SERIKALI IACHE UTAPELI
Wananchi wanalipia huduma ambayo hawaipati kikamilifu na inatolewa kama fadhila. Kupitia Tume ya Ushindani (FCC) mashirika yote yaliyosajiliwa Tanzania yanapaswa kuhakikisha wanatoa huduma kwa usawa, uwazi na uhakika. Kinyume na hapo wanakuwa wanakabiliwa na sanctions.
Lakini shirika la TANESCO hakijawahi kuwa na huduma bora, usawa, uwazi na uhakika. Je lipo juu ya sheria ama lina Presidential immune?
Hivyo serikali kupitia TANESCO kupokea malipo ya wanaoomba huduma, au kupokea malipo ya LUKU ilihali huduma haitolewi kwa uhakika ni dalili ya serikali kuwatapeli wananchi wake huku ikijilinda kwa mifumo yake isiwajibishwe kwa ujambazi huu.
Serikali inapaswa kuwa safi muda wote
2. HATUA ZICHUKULIWE
Endapo Wabunge wa bunge hili watashindwa kuisimamia serikali kwenyr hii hoja ya UMEME wa uhakika basi sisi wapiga kura tuwakatae kupitia sanduku la kura.
Inawezekana ndani ya TANESCO zipo hujuma zinaendelea na labda mifumo yetu wanajua hilo. Hatua zichukuliwe kukomesha haya mambo. Tusisubiri aje kiongozi mwenye uchungu na nchi, bali tuweke sheria zenye uchungu na nchi ili kumnyoosha yeyote ambaye atabainika kushiriki hujuma. Ikibidi tuiazime kwa muda katiba ya CHINA ili kujenga nidhamu ya watendaji na wanasiasa.
3. KUSHTAKI TANESCO
Kwa kuwa ni Rais pekee (na sasa spika wa Bunge) ana kinga ya kutoshtakiwa kwa dhambi atakazotenda. Basi hakuna mwingine aliye na kinga hiyo. Hivyo iwezekane suala.la Tanesco likapatiwa ufumbuzi kisheria mahakamani kwani bila kuchukua hatua hiyo, hakuna na hatotokea mwenye uwezo wa kuliweka sawa Shirika hili la Ugavi wa nishati ya umeme.
Natoa hoja....
Msanii wa JamiiForums