MCC: Vita kati ya Serikali ya Magufuli na vibaraka (Wadau wa Richmond, Dowans na Symbion)

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Shirika la misaada ya Marekani, MCC limesitisha msaada wake wa awamu ya pili kwa Tanzania kwa kisingizio cha Uchaguzi wa Zanzibar na Sheria ya Makosa Mitandaoni.

Uongo mkubwa. Marekani siyo wageni wa siasa za Zanzibar, wapo siku zote, Adui namba moja wa Marekani ni Muislamu kutokana na dhana yao potofu kwamba Ugaidi duniani unatekelezwa na Waislamu. Vita yao ya Ugaidi katika nchi za kiislamu zinadhihirisha hilo. Kauli ya Mgombea urais mmoja nchini humo iladhihirisha hilo. Zaidi ya 85% ya ndugu zetu wa Zanzibar ni Waislamu. Leo Marekani ni rafiki yao? Kichekesho.

Marekani ni Wakeukaji wakubwa wa haki za binadamu na faragha. Ni marekani haohao walioingia mgogoro na Ujerumani na Brazil kutoakana na kitendo cha kuingilia mawasiliano ya marais wa nchi hizo, Marekani hata ukienda Chooni unamulikwa na Kamera. Nani wa kulalamikia vitendo hivyo? Au kwa sababu wao ni baba wa Dunia? Kunya anye kuku, akinya Bata Kaharisha.

SITISHO hilo limekuja siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari John Pombe Magufuli kusema kuwa anakerwa sana na Mikataba isiyo na tija kwa Taifa na kutolea mfano mkataba unaoifanya Kampuni ya SYMBIONS ya Marekani kufanya shughuli zake nchini.

Aidha SITISHO hilo la MCC awamu ya pili limeungwa mkono kwa haraka sana na CHADEMA(chama ambacho Aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND ambayo mitambo yake ilinunuliwa na SYMBIONS, kampuni ambayo inatoka katika nchi inayositisha msaada wa MCC aligombea urais kupitia kwa chama hicho na kugharagazwa na rais anayejongoza Serikali inayokataa kulamba miguu ya Wazungu). Tamko hilo limetolewa kupitia kwa Waziri Kivuli- Mambo ya nje. Tena akisema kuchelewa kusitishwa kwa msaada wa MCC kumechelewa sana.

Tatizo siyo Uchaguzi wa Zanzibar wala Sheria ya Makosa Mitandaoni, tatizo ni RICHMOND, DOWANS NA SYMBIONS.

Richmond ndiyo ilipelekea Edward Lowsssa kushinikizwa kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu mwaka 2008. Mpaka leo Lowassa anasema Mkataba wa Richmond ulikuwa halali na kwamba kujiuzulu kwake kulitokana na watu kuitaka nafasi ya Uwaziri Mkuu na siyo Mkataba feki wa Richmond.

Symbions , Kampuni ambayo ilinunua mitambo ya Richmond na ambayo mpaka leo inalipwa mamilioni ya pesa ambazo ni jasho la walipa kodi wanyonge pamoja na kufanya shughuli zake Tanzania, inaendesha shughuli zake sana katika nchi ambazo zimeumizwa sana na Marekani kwa njia ya vita kwa kisingizio cha kutetea haki za binadamu. Symbions iko katika nchi za Iraq, Mashariki ya Kati, Haiti, Afighanistan na zingine nyingi.

Ujasiri wa LOWASSA kusimama tena bila aibu na kusema RICHMOND ilikuwa halali hautokani na kitu kingine bali U-KIBARAKA wake kwa Marekani. Mahojiano yake na gazeti la "THE CITIZEN" la Mei 30, 2015 alipoulizwa kama mkataba wa Richmond ulikuwa halali unathibitisha ukweli huu pale alipojibu na kusema "It took a former US Secretary Of State, Hillary Clinton and US president, Barack Obama to come to Tanzania to confirm that the power generating plant was Okay" akimaanisha "Iliwachukua Katibu wa Ikulu ya Marekani , Hillary Clinton na Rais wa Marekani , Barack Obama kuja Tanzania kuthibitisha kuwa mtambo wa kuzalisha Umeme ulikuwa safi"(Tafsiri yangu). Kwa undani juu ya mahojiano kati ya LOWASSA na gazeti la the citizen, soma hapa: http://www.thecitizen.co.tz/News/Ric...z/-/index.html

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga (CCM) na mshirika mkubwa wa Lowssa, ROSTERM AZIZ, ambaye kwa sasa kimya chake hakuna ajuaye kina maana gani na hakuna ajuaye alipo kwa sasa ni alikuwa mdau mkubwa sana wa RICHMOND, DOWANS na SYMBIONS. Rosterm alijaribu kukanusha kuwa hakuw na ubia wowote na Richmond , lakini mmoja wa waanzilishi wa Richmond, bwana GIRE alithibitisha kuwa Rosterm alikuwa ni mmoja wa wamiliki wa RICHMOND. GIRE alithibitisha hilo wakati anawasilisha nyaraka mbele ya Mahakama ya kimataifa kitengo cha Biashara(International Chamber of Commerce-ICC) wakati wa Sakata la TANESCO na DOWANS. soma hapa:http://www.theeastafrican.co.ke/news...z/-/index.html

Moja ya Changamoto ambayo Nchi za Kiafrika ambazo zinaonekana kuwa na misimamo ya kukataa kuwalamba miguu WAZUNGU ni pamoja na kuwa na VIBARAKA wa Wazungu ndani ya nchi hizo. Kenya, Uganda, Zimbabwe, Rwanda, Libya, Misri, Tunisia na nyingine nyingi zimekumbana na changamoto hiyo. Kenya, Uganda na Zimbabwe zinaelekea kuishinda changamoto hii siyo kwa sababu nyingine, bali misimamo ya Wananchi wake kupitia masanduku ya kura , upashanaji habari kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vingine vya habari n.k. Misri, Tunisia, Libya wananchi wake hivi sasa wanajuta kwa sababu waliwafuata VIBARAKA.

NI zamu yetu Watanzania, kuamua kusuka au Kunyoa. Mwaka 2020 siyo mbali, kwa mara ya kwanza tutashuhudia MAREKANI wakitoa mapesa mengi kuhakikisha VIBARAKA wake wanaingia ikulu. Ni lazima wafanye hivyo kwa sababu sasa wanaamini chini ya JPM ni vigumu sana kujipenyeza kwenye rasilimali zetu.

Ni wajibu wetu Wananchi kusimama kama walivyosimama Uganda, Kenya, Zimbabwe, Rwanda n.k
Serikali nayo ifanye juhudi zote kung'amua haraka sana misaada yenye masharti kama MCC, kung'amua vibaraka wa Wazungu kama akina ROSTERM na Washrika wake.
 
Hivi kuna kiongozi hapa Africa alikua na jeuri kama kanali muamar ghadafi? Vp aliishia wapi?Nnachokwambia labda US na wazungu hawajakuamulia kuchukua rasilimali ulizonazo lkn wakiamua ni asubuhi tu wamemaliza mchezo. Tuombe tusifikie huko.
 
Hivi kuna kiongozi hapa Africa alikua na jeuri kama kanali muamar ghadafi? Vp aliishia wapi?Nnachokwambia labda US na wazungu hawajakuamulia kuchukua rasilimali ulizonazo lkn wakiamua ni asubuhi tu wamemaliza mchezo. Tuombe tusifikie huko.
Wazungu ni watu tu Kama wewe, walimuweza Gadafi kwakuwa wananchi walikubali kutenganishwa na serikali Yao ila Kama sisi wananchi tutakuwa kitu kimoja na serikali ya JPM hao wazungu itakula kwao Kama Zimbabwe
 
Wazungu ni watu tu Kama wewe, walimuweza Gadafi kwakuwa wananchi walikubali kutenganishwa na serikali Yao ila Kama sisi wananchi tutakuwa kitu kimoja na serikali ya JPM hao wazungu itakula kwao Kama Zimbabwe
Naona umeanza kujifariji kwa lugha laini laini eti wazungu ni watu kama wewe, hahah by the way unaongelea Zimbabwe ipi? Hii ambayo wananchi wake wanatorokea Afrika kusini kila siku kwenda kua vibarua au hii ambayo trillion 1 ya Zimbabwe unanua ndizi mbivu 6 au unaongelea Zimbabwe ipi? Acha kulinganisha Tanzania nzuri na Nchi kama Zimbabwe.
 
Hivi kuna kiongozi hapa Africa alikua na jeuri kama kanali muamar ghadafi? Vp aliishia wapi?Nnachokwambia labda US na wazungu hawajakuamulia kuchukua rasilimali ulizonazo lkn wakiamua ni asubuhi tu wamemaliza mchezo. Tuombe tusifikie huko.
Acha Uoga...! Ndiyo maana muda huu Mafaili ya wanadiaspora....na alumni wa nje nitalazimika kuyaanzishia mjadala yakaguliwe ilitujue kama kutakuwa na wale wenye tabia za "Wahuni wa Benghazi ya Libya" (rejea: 'WAHUNI' WA BENGHARZ wakiwa kwenye maandalizi ya "uhuni" )
 
Shida ya US ilikua ni nini? Wamepata au hawajapata waluchokitaka?
Kumbuka hii ni Tanzania....! Tunachujana pole pole Ghadafi alijihamini sana bila kuwa na tahadhari ...Tanzania tutajiadhari hata kwa kudondokewa na unyasi tutafanya uchunguzi 'nawaza tu'...!
 
Kumbuka hii ni Tanzania....! Tunachujana pole pole Ghadafi alijihamini sana bila kuwa na tahadhari ...Tanzania tutajiadhari hata kwa kudondokewa na unyasi tutafanya uchunguzi 'nawaza tu'...!
Sawasawa, ila unaweza kujihami vp bila tahadhari?
 
Lowasa na genge lake wamebanwa pande zote...si muda mrefu Rostam atawafuata wengine pale Kisutu
 
Wazungu ni watu tu Kama wewe, walimuweza Gadafi kwakuwa wananchi walikubali kutenganishwa na serikali Yao ila Kama sisi wananchi tutakuwa kitu kimoja na serikali ya JPM hao wazungu itakula kwao Kama Zimbabwe

Ni kweli, mwanangu
 
Kwa hiyo ukiukwaji wa Demokrasia huko Zanzibar ni halali kwa kuwa 85% ya watu huko ni waislam ambao hawatakiwi na Marekani?

Acheni upumbavu.
Nafikiri kuna watu wanaumwa ukada nakutuletea visababu vya kidini,ifike mahali tuache uchama na tuseme ukweli. Sikubaliani na utegemezi wowote ila siungi mkono umangimeza na ukoloni mweusi. Pia ni lazima tuwe makini kujadili misaada na ukiukwaji wa demokrasia, sio kwakuwa umepewa vijisenti basis unaamua kuwa kondom, nachukia sana watu wa namna hii
 
Back
Top Bottom