Asante sana Mzee Mwanakijiji kwa mahojiano, nimemsikiliza Mh. Ngeleja alipokuwa akijikanyaga kanyaga kujibu maswali yako pamoja na kutoa maelezo.
Kitendo cha yeye kukuomba ufunike funike kimenipa mashaka kiasi. Hivi kama serikali na Tanesco wana nia njema kuna haja ya kuomba msaada wako ili utuelimishe zaidi. Ametumia neno baya, kwamba wewe ni kama "kiongozi wa dini na una wafuasi wengi". Kwa hiyo yeye anaamini kwamba ukisema chochote kiwe kibaya ama kizuri wafuasi wako wataitikia AMEEEENI ama AMIIIIIN (kwamba watakubali kuwa kiko sawa tu)!
Mh. Zitto na wewe una watu wengi sana wanaokuamini, nina mashaka unaweza kuwa ulipewa info nzuri na ukaruka hewani ili wao (serikali) wapate nguvu ya kuendelea na kununua hiyo mitambo ya Dowans. Itafakari sana kauli ya Ngeleja aliyoisema kwenye haya mahojiano na Mwanakijiji. Ombi langu kwako ni moja, jiridhishe kwamba hujalishwa kasa, maana mitambo hiyo ikinunuliwa na ikaja kubuma after 3 yrs, utakuwa umeua upinzani kwa bua, sidhani kama CHADEMA watakuja kuaminika tena. Msimamo wa Kamati yako naona umekaa kimtego mtego.
Uzuri wa maelezo ya Mh. Ngeleja ni kwamba amekiri kwamba hakuna ulazima/uharaka wa kununua mitambo ya Dowans ila kwa kuwa opportunity imejitokeza ndiyo maana wanataka kununua. Kwa hiyo kauli kwamba ama tununue mitambo ya Dowans au tuingie gizani, ilikuwa ni spinning.
Ukisoma press release ya Dr. Rashid inapingana na maelezo ya Ngeleja. Dr. Rashid anaonyesha kwamba ni lazima mitambo hiyo inunuliwe, wakati Ngeleja anasema hali ya maji kwenye mabwawa yetu ni shwari na nakisi ya umeme iliyopo imekuwepo siku zote ingawa hapo mbeleni kidogo kutakuwa na ongezeko la mahitaji ya umeme. Sasa hizi contradictions zinatoka wapi au labda Ngeleja ana info nusu?
Idea ya kununua mitambo ya Dowans ilianza tangu mwaka jana Oktoba, leo ni March 2009 ambao ni mwezi wa 6 tangu wapate hiyo idea, kwanini hawakuamua kuanza mchakato wa kununua hiyo mitambo mipya tangu kipindi hicho? Nina uhakika mpaka kufikia mwezi June mwaka huu tayari mitambo ingekuwa Dar na ingekuwa imefungwa.
Swala la capacity charges kumbe kampuni karibu zote mikataba ilishakwisha kasoro IPTL tu ambao bado wanaendelea nao. Maelezo waliyopewa kamati yanasema wazalishaji binafsi wanakomba hela za capacity charges na kumbe kabaki mmoja tu. Kwa hiyo hata tukinunuwa mitambo ya Dowans bado mzigo wa kuibeba IPTL uko pale pale mpaka watakapokubali kuuza mitambo yao.
Ngeleja anasema bei ya mitambo ya Dowans ni kama shilingi bilioni 60 hivi (ambayo inazalisha MW 100), kuna mtu hapa jamvini kasema kwa bilioni 70 tunaweza kupata mitambo ya kuzalisha MW 200. Ngeleja anasema bei ya mitambo mipya kutoka GE ni kama bilioni 90. Kwa wenye data na utalaam wa bei tunaomba watumwagie hapa, lakini bei hizo ziwe za mitambo kama ya Dowans ambayo wanasema inatumia gas kwa kuwa gas ni bei poa.
Ngeleja anasema kwamba kununua mitambo mipya ni process ambayo inaweza kuchukua si chini ya miezi 20 mpaka 24. Hivi hiyo mitambo inatoka hapa hapa kwenye hii dunia ama inatoka sayari ya Mars? Tendering inaweza kuchukua muda mrefu lakini kuna exception na nina uhakika within 6 months tunaweza kumpata supplier na akashusha mzigo Dar. Hiyo miaka miwili inatoka wapi? Lini procurement ya mitambo ya kufua umeme ilichukua muda wa miezi 20 mpaka 24?