Dowans: Another Richmond in making?

Msaada kwenye tuta:

Serikali ilishatangaza rasmi, baada ya kigugumizi cha Waziri Ngeleja, na mvutano wa Kamati za Shelukindo na Zitto, kwamba wameghaili kununua mitambo ya Dowans.

Sasa hapa ni nini kipya kimeendelea zaidi ya wazo la mwenzetu mmoja kwamba mwezi April, mwezi wa masika, waja, hivyo tutakosa umeme, tununue mitambo ya Dowans?!

Kipya nini hapa?
 
Dark City,
Thanks. Ninakuelewa kuhusu wanasiasa na perceptions. Nilidhani hapa kwenye JF we are above perceptions and we attempt to search for truth and only truth. This is my only objective sina sababu nyingine.
Hoja ya Double Standards, ni hoja dhidi ya wale wanaokataa na hawasemi kitu dhidi ya ununuzi wa mitambo chakavu ya IPTL. I am not in any way justifying the same.
Issue ya kutangaza Tender is very plausible, lakini what are the facts hata kabla hatujatangaza Tender. What has emerged now that merits this subject to be debated. Kwangu mimi inaelekea bado kuna wingu zito limejificha katika swala hili ndiyo maana niko very eager, kupata ukweli wa kilichoko ndani ya Kamati ya Mashirika ya Umma na Kamati ya Nishati na Madini.Kati yetu nani anajua exactly what are the points of contention? Kama yuko ayaweke jamvini tuyachambua, ndiyo maana ninasisitiza kuwa swala zito kama hili is not only a matter of political interest, and therefore we must raise above our narrow political interests and argue and debate objectively and constructively.
 
Ochu, heshima mbele mkuu

Asante kwa analysis yako but with due respect I have to differ with your opinion.

Kama sheria ya Tanzania ndio imeanishwa kutumika katika huo mkataba basi uchambuzi wa sheria hapo juu waweza kuchukua mkondo wake.

Lakini, as i can feel it, this was a kind of International Business Transaction na inanifanya nichelee kukubaliana na wewe kuhusu hizo principles ulizoweka hapo juu unless umeona mkataba unasimamiwa na sheria ya nchi gani au kanuni zipi; yote yanawezekana, unaweza kuta Tanzania courts do not have jurisdiction on the matter na kwamba ikitokea kukiwa na msuguano wa mkataba, labda Iternational Arbitration will take over mfano mzuri ni Kesi ya IPTL na TANESCO ambayo ilifanyika hapa marekani.

Deal kubwa kama hiyo, I am sure jamaa watakuwa wameweka kifungu kinachoonyesha sheria ya nchi gani itatumika au vitu kama Incoterms au UCP.

Kwa hiyo tukiupata huo mkataba itakuwa vema na rahisi kuuchambua otherwise we are just dealing with some kind of speculation.

**************

Inavyoonekana Mawakala wa mafisdadi hawakosekani. Wako kila mahali, watajaribu kuweka uhalali katika kila haramu, wataliita giza kuwa mwanga, watachimbua kila sheria, watachunguza kila kipengele, kanuni, taratibu -- watatembea kila urefu wa kilometre hapa duniani na hata ahera ili tu watafute kisingizio cha kuwaibia Watanzania masikini.
INAONEKANA KAMA VILE HAKUNA SERIKALI HAPA KUZUIA HII. SERIKALI INAYO KILA HAKI KUSTOP -- KWANI LAZIMA??? WANANCHI TUSIKUBALI MAFISADI WATUZIDI KETE, TUSIKUBALI KABISAAAAAAAAAAA!
 


Maneno mazito sana hayo nilokuza MH.Dr.Slaa , ndio maana wengine tunatafuta kujua nini kinaendelea kati ya kamati hizi na ununuzi wa mitambo chakavu.
 
Maneno mazito sana hayo nilokuza MH.Dr.Slaa , ndio maana wengine tunatafuta kujua nini kinaendelea kati ya kamati hizi na ununuzi wa mitambo chakavu.
Ndiyo maana ninafikiri hoja ni kwa Kamati hizi mbili zikae na kutupatia Taifa hili missing information.
 
Dakta Slaa inaonekana Mbunge Kijana tayari anaijua hiyo "missing information" ndio maana anatoa mapendekezo/hoja kwa kujiamini - mwambie aje atupe hiyo taarifa tusiyo nayo tumuelewe la sivyo ataishia kuwa kama Waziri Kijana aliyeingilia Sheria ya Manunuzi!
 
Campanero,
Zitto huingia JF in his own right sina sababu ya kumwambia. Atakuja kwa wakati mwafaka atakaoona unafaa. Kama kuna swala la kuingilia mchakato nadhani he is mature enough to detect early enough what is good for him and vice versa.
 
Mh. Dr. Slaa..
with due respect, mkuu wangu ZItto amechemsha!.. kachemsha big time kama alivyochemsha Masha ktk issue ya vitambulisho.. Ni kosa kubwa kwa kamati yake kuingilia swala ambalo sasa hivi halipo ktk siasa isipokuwa ni utekelezaji wa serikali.. hapa mkuu nakubaliana na Mwakeyembe 100 kwa 100..Hatuhitaji siasa ambazo zinakuja na fikra za muda mfupi!..Pili, kama kiongozi wa Chadema utelezaji mbovu wa sera nzima ya umeme ni silaha kwake na chama chake sio kazi yake yeye ku solve matatizo ya uongozi uliopo...tena kwa maamuzi mabaya kama haya.

Kitu kimoja alichotazama Zitto ni kuhusiana na nchi kuwa kizani?.. hii point haina mantiki kabisa kwa sababu hadi sasa hivi hatujainunua mitambo hiyo na nchi haipo kizani..hivyo muda huu unaotumika kubishana na kuundwa kwa kamati ni muda ambao ungetumika kuagiza mitambo mipya yenye guarantee ya warrant ya miaka mingi zaidi...Licha ya yote hayo mitambo ya Dowans ni chakavu kinyume cha kanuni na sheria za manunuzi ya mitambo..
Kutumia siasa na sababu ya mitambo ya IPTL ni makosa yanayorudiwa hivyo inazidisha kuonyesha jinsi tulivyo wafinyu ktk kufikiria..Ni sababu kama hizi ndizo zilizotuingiza ktk mikataba feki na mkingine ya kuuza mali zetu kwa bei ya NJUGU kwa sababu tumefikiria zaidi gharama badala ya vipengele muhimu zaidi ktk manunuzi kulingana na biashara inayokusudiwa..Tumefunga mikataba ya migodi yetu ya madini kwa sababu ya kufikiria gharama, tumeshindwa hata kusimamisha usafiri Dar kwa sababu ya kufikiria gharama, tumeshindwa kuweka vifaa na huduma nzuri bandarini kwa sababu tunafikiria gharama..Vitu vyote hivi kwa muda mrefu vimetugharibu zaidi na pia tumepoteza bishara kubwa kwa sababu sisi wagumu sana ktk maisha ku plan long term strategically hata iwe maisha yetu binafsi..

Hakuna hadithi hapa mkuu wangu, serikali iliyopo madsarakani ilituahidi kuwa mitambo ya Richmond ni ya muda mfupi tu na kwamba nchi yetu ina invest ktk uzalishaji umeme kwa nguvu za jua, makaa ya mawe na pia kuifanyia ukarabati mitambo iliyopo ili tatizo la umeme lisiwe tatizo la kudumu.. Hiyo promise iko wapi?..miaka mitatu sasa tunazungumzia kitu ambacho huwezi kunambia kwamba hawa watu walifikiri sisi wajinga sana kutuletea Richmond kampuni feki wakatuibia fedha zetu halafu leo tumefikia maamuzi ya kununua mali tuliyoibiwa..Hadi sasa hivi tumekwisha lipia fedha zaidi ya thamani ya mitambo hiyo na umeme bado ni tatizo kubwa Dar tena gharama zake ni kubwa kulingana na uwezo wa wananchi!..

Mchezo huu ni sawa na wizi wa Vibaka ambao wanakuja kuibia taa za gari lako kisha kesho yake ukizitaka inabidi uzinunue tena toka kwao.. kwa sababu hakuna jinsi sheria zetu ni butu.. Ni maisha ambayo sasa hivi nyie viongozi mnataka kuyaingiza hata ktk utendaji kazi wa serikali..
Upuuzi mtupu..hakuna habari ya nchi kuwa kizani wakati mnalipia fedha kila siku kwa mkataba feki..kisa mnaogopoa nchi kuwa kizani kama kweli walikuwa na nia njema kwa nini waisifikirie hilo kabla Richmond hawajaingia nchini..besides, hakuna hata kiongozi mmoja aliyesimamishwa mahakamani hadi sasa...hizo objective arguement zitaanzia wapi?..
 

Yaani maamuzi ya Zitto yakifanyiwa tathmini tayari inaonekana haifai kujadili maamuzi ya viongozi kwa sababu ''tumewachagua wenyewe'' ila kutathmini maamuzi ya Rais na mawaziri ni sawa. Kwa mtindo huu sidhani kama nyota ya asubuhi itachomoza!
 

Zak Malang, Heshima yako mkuu.

Reading between the lines; I do'nt want to create a storm in a cup of tea. If you read carefully at my reaction to the above thread, I was and i am still trying to look at the bread and butter issues so as to advice people on the right way to go kuliepusha taifa na masuala ya unncessary damages. Mzee, we advocate for a rule of law and nothing else and we are trying to help the nation katika hii transition kutoka kwenye makucha ya ufisadi et al kuelekea katika democracy ya kweli.

Shadow.
 
Mkandara,
Naheshimu maoni yako. Umekosea vibaya sana kwa kutokurejea hadidu za rejea ya Kamati ya Zitto. Nadhani utafiti mdogo ungekuweka pazuri katika hoja yako. This was my starting point. Hakuna haki ya kuhukumu kama hujafanya utafiti. Yaani basis yako ni hoja ya Mwakyembe tu? Porojo hazisaidii sana katika maswala makubwa mazito yenye kuhitaji kufikiri sana.
 
Ndiyo maana ninafikiri hoja ni kwa Kamati hizi mbili zikae na kutupatia Taifa hili missing information.

Kamati hizi sioni wakija na jipya hata wakikaa kwani tayari kila mwenyekiti wa Kamati kwa muda wake ameshaweka msimamo ama wake au wa kamati yake hadharani kupitia vyombo vya habari.

Zitto akisema inunuliwe ,
Shelukindo akisema hatuwezi kununua mitambo chakavu .

Nafikiri kuna tatizo kubwa kuliko tunavyoliona hapa na kulijadili hapa wakati muafaka ukifika yatawekwa hadharani yale yaliyofichika.
 

Kama ni kupiga kura katika hili suala niko tayari kupiga kura kwamba tukae gizani hata miaka 2. Lakini tukimalizana na hilo giza tutatoka angalau tutakiwa na akili. Hiyo ni bora kuliko kuingizwa kwenye pressure ambazo zinatufanya mara nyingi tufanye mambo ya hovyo kama ya Richmond! Na mimi naamini wafanyabiashara mafisadi wanafanya haya mambo makusudi tu. Ingekuwaje mtu kama Dr Rashid (CEO wa TANESCO) aseme wazi tena kwenye media kwamba kama hatutanunua mitambo ya Dowans basi hakuna njia nyingine zaidi ya kuingia gizani. Kama ningekuwa boss wake hakika ningemfukuza kazi dakika hiyo. Unawezaje kuwa kiongozi wa shirika kubwa kama hilo halafu usiwe na plan B?? Hii ni harufu kubwa sana ya rushwa na mtu yeyote makini hatakiwi kujihusisha na hili dili.
 


[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]"Serikali imetafakari maoni ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na imejiridhisha kwamba ni vema TANESCO wasishiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mitambo ya Dowans.

"Serikali tayari imekwishaiagiza TANESCO kutoshiriki kwenye zabuni hiyo. Wizara ya Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla tuna imani kubwa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Bunge kwa ujumla. "Kwa kuzingatia maslahi ya Taifa pamoja na sababu zetu ambazo tuliziona ni za msingi katika nia ya kushiriki kwenye zabuni, tumeona ni vema TANESCO isishiriki zabuni hiyo," alisema
[/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]William Ngeleja, [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Waziri wa Nishati na Madini, [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sasa cha zaidi nini hapa?
[/FONT]​
 

Mh. Dr. Slaa unakuwa unakosea unapokuja hapa HF kwa design ya kutetea watu wa chama chako tu. Kuna wakati mnapaswa kuweka siasa pembeni na kujali maslahi ya taifa. Ya Zitto mwache ajibu yeye mwenyewe, kwani hana access na internet? kwanini asije kujibu mwenyewe? Haifai namna hiyo.
 

Si unajua tena Sherukindo anataka achukulie hapo ujiko????/
 
Nashindwa kujua nani tumwamini,pia ni wapi kama Taifa tunataka kwenda.Kila mtu anashabikia upande na uamuzi wake,nafiki la msingi tungewaacha wataalam wetu wafanye kazi kitaalam bila kuingiza siasa,pia wangeuliza watengenezaji wa mitambo ili kujua gharama halisi,mbona inawezekana kuuliza,na kufanya utafiti?naogopa kuona kuwa tunaandikia mat badala ya kalamu,,,,
 
Spinning zinaendela hivi sasa na TBC1 wapo na Idrissa Rashidi naye anasema kuwa kw3a sasa Mwanza na Kigoma kuna mgawo , ila sababu kubwa ni kutokana na migodi haswa North mara na Buzwagi kuingizwa kwenye grid ya Taifa.

Anaendelea kusema kuwa mahitaji ya umeme yameongezeka kwa asilimi 10 na haswa kanda ya ziwa kutokana na migodi, na pia Tanga kutokana na kiwanda cha cement kipya kilichoanzishwa.
 
Mh. Dr. Slaa,
Mkuu nimekusikia sana tatizo bado unatumia siasa ktk ku solve tatizo hili..Mimi Mbongo na nimeishi miaka yote ya ujana wangu Bongo.. naelewa harufu mbaya ya mnyama hatari kama Simba bila hata kumwona..

Mimi sina haja ya kusoma hadidu za Zitto kwa sababu alivyoanza tu kasema alimwomba ruksa Spika..hapo tu tayari anaingilia kazi isiyokuwa yake kisha swala hili la Dowans ni swala ambalo yeye alitakiwa kukaa mbali kabisa nalo hasa upende huo!...Trust me, sioni tofauti yake na Masha ktk swala la vitambulisho hata kama kuna tofauti za miradi hii.

Sasa tuzungumze kama watu wazima. wewe kama kiongozi na pongine unayeunga mkono kamati ya Zitto nambie sababu ambazo wewe zimekuvutia ktk maamuzi hayo!..Kwa sababu mimi sioni kabisa argument yenye malengo mazuri.. nipe points zako wewe kutokana na hadidu hiyo maanake mimi sikuoina la maana kabisa kufikia maamuzi ya kuunga mkono ununuzi wa mitambo iliyochakaa..
 
Sheria ya Manunuzi inasemaje kuhusu manunuzi ya kawaida na ya dharura? Inasema tununue Dowans ili tusiingie gizani? Kuidharau sheria hii ndio kulizaa Richmond kwa mujibu wa Kamati Teule!Kutofuata kanuni bora za manunuzi ndio kulizaa dili la Rada!Dakta Rashidi analijua hili fika! Mbunge Kijana analijua hilo pia!Dakta Slaa kuna 'missing information' gani hiyo inayopingana na sheria? Utawala wa Sheria ndio utatunusuru katika hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…