Double Standards za Ikulu kumtetea Ombeni Sefue

Double Standards za Ikulu kumtetea Ombeni Sefue

Ushahidi gani unataka zaidi ya huo niliotoa, tuwaombe wahariri wa magazeti watoe picha iliyopigwa siku ya kusaini mkataba, muongo atajulikana ni nani kati ya gulwa na mtetezi wa ikulu
We chizi kweli kama unategemea magazeti ndio source kuu ya information,inadhihirisha jinsi gani upo level za chini za kupata habari.
 
Mmmm hapa kazi hipo jpm unakibarua sana kusafisha nchi hii mm naona cha muhimu nikukaza sara aisee
Usafi wa nchi hii unapaswa kuanza kwa kurekebisha mifumo ya sheria kwa kuanza na Katiba Mpya, hususan Katiba ya Wananchi kwa kuhuisha Rasimu ya Tume ya Warioba ambayo pamoja na mambo mengi mazuri, inazuia viongozi na watumishi wa umma kuficha fedha nje ya nchi kiholela, jambo ambalo aghlabu hufanywa na viongozi hao wanapopiga dili na Trans-national Companies kama hizo.
 
Ikulu wako sahihi; Double standards is a relative term depending on your corner of intetest; kwa hili unaonekana you are all out to settle scores na Sefue kwa sababu zako mwenyewe!!, kama Dira wana taarifa zenye mashiko waende Takukuru; vyombo vya habari vinaweza kuwa Whistleblower; tuhuma huchunguzwa polisi; takukuru na kesi hufanyika mahakamani!
Jamhur walienda Takukuru??
 
Mkuu Tumia japo akili ya shule ya msingi, wamesema, mwenye ushahidi aupeleke Takukuru au Baraza la maadili, na wametoa maelezo na evidence vizuri sana, maana kuna mengine yalifanyika wakati BALOZI ombeni akiwa BALOZI wa Tanzania Marekani na Umoja wa mataifa, na mengine yalifanyika akiwa na wiki tu kwenye wadhifa wake huu, sasa kama wewe unao ushahidi peleka Takukuru.

Kumbuka Katibu mkuu kiongozi si mtu mdogo kwa wadhifa, kwa hiyo hawezi tu kujitokeza hadharani kujibu upuuzi, na utambue kwamba, Ni lazima kulikuwa na consultations kati ya ofisi yake na idara ya habari maelezo juu ya tamko hilo.
Nauliza tu Gazet la Jamhur ushahid waliupeleka Takukuru au Baraza la Maadili??
 
Tamko la ikulu limesema kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au wachukuliwe hatua, hatuwezi kuacha nchi iendeshwe kwa majungu
Takukuru iko chini ya nani!
Hivi una uwezo wa kumchunguza
na kutoa matokeo chanya
 
Nashindwa kuielewa hii nchi linapofika swala la kuwajibishana kwa viongizi wa juu serikalini hasa kwenye suala la ufisadi
Najiuliza sipati jibu mpaka saa izi muhusika wa tuhuma hizi
1. Richmond- Ilihusishwa na aliyekuwa waziri mkuu wakati huo ndugu Edward Lowassa na watendaji wengine lakini mpaka sasa hakuna kesi na waatu hao wanaendelea kula matunda ya kazi yao.... imekuwa huu ndio utetezi waoo mkubwa MWENYE USHAHIDI AUTOE AU AENDE MAHAKAMANI AKAFUNGUE KESI. lakini hakuna kesi inayofunguliwa watu wanabakiza blaa blaa kwenye vijiwe vya kahawa tuuu
2. EPA, MEREMETA, RADAR NA TUHUMA ZINGINE..... Utetezi ni ule ule MWENYE USHAHIDI WA KUTOSHA AUTOE AU AENDE MAHAKAMANI......nashindwa kabisa
3. PEMBE ZA NDOVU NA UTORISHWAJI WA TWIGA......Utetezi ni ule ule MWENYE USHAHIDI AUTOE AU AENDE MAHAKAMANI...
4. ESCROW..... Hii ndo aibu kubwa kabisa lakini watu wanajilia pesa walizochma bila jasho

MASWALI YANGU....
1. NANI ANAO/ANATAKIWA KUWA NAO HUO USHAHIDI WA HIZO TUHUMA????
2. NANI ANATAKIWA KUUTOA HUO USHAHIDI??
3. NANI ANATAKIWA KUFUNGUA HIZOO KESI??
4. KAMA KAZIFUNGUA MAENDELEO YA HIZO KESI NI UPI??
5. KAMA HAJAFUNGUA NANI AWAJIBIKE AU KUPEWA MZIGOO???
Hizi ni danganya toto kabisaa. Inawezekana hata IKULU NI JIPU LINALOTAKIWA KUTUMBULIWA.....
Ni mtazamo tuu
 
Jamhur walienda Takukuru??

Dokezo lao lilikuwa la kitaalamu zaidi; with all relevant data mpaka mchoro wa mabomba ya wizi ikawashawishi JPM na MKM kuifanyia kazi; sasa hii ya Dira; ngonjera; just dropping names!
Ni dhahiri ni ripoti ya umbea zaidi na kwa kuwa Ikulu imewashushua; kama wana uhakika na ripoti yao wachukue hatua zaidi wakianza na kutoomba radhi au wafunguke zaidi!
 
Ndio maana tunasema majipu ya Magufuli yatawahusu watumishi wadogo tu wa serikali na mashirika ya umma. Lkn hayatagusa MAFISADI papa ya viongozi wa ccm.
 
Kwa hiyo ni haki kwa mwandishi yeyote kuandika kisicho na ukweli? Kama Ikulu ingemtetea na kuna ushahidi hapo your topic ingekuwa na mantiki lakini as you can see everything is a lie so, what did you expect? For Ikulu to remain quite about it is a confirmation of the allegations.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Ndio maana tunasema majipu ya Magufuli yatawahusu watumishi wadogo tu wa serikali na mashirika ya umma. Lkn hayatagusa MAFISADI papa ya viongozi wa ccm.

Kama katibu mkuu wa Maliasili,
kamishna mkuu wa Tra, afisa mtendaji mkuu wa vitambulisho, Edward Hosea
wa Takukuru Dg wa Dar rapid transport; just to mention a few ni wafanyakazi wa ngazi ya chini katika serikali na mashirika ya umma; basi hujui unachozungumzia hata kidogo! Umbea wa kulipiza kisasi kwa kuwa umeguswa hauna nafasi hata kidogo!
 
Dokezo lao lilikuwa la kitaalamu zaidi; with all relevant data mpaka mchoro wa mabomba ya wizi ikawashawishi JPM na MKM kuifanyia kazi; sasa hii ya Dira; ngonjera; just dropping names!
Ni dhahiri ni ripoti ya umbea zaidi na kwa kuwa Ikulu imewashushua; kama wana uhakika na ripoti yao wachukue hatua zaidi wakianza na kutoomba radhi au wafunguke zaidi!
Mdau MTK kusema mwenye ushahidi aupeleke PCCB bado hakumfany jamaa kuwa hajatenda kosa,wasiwasi wangu wanapoguswa watu flani flani basi utetez unakua mkuubwa kweli,tuhuma zinetolewa nadhan vyombo husika ndo vinapaswa kusema au kuwaambia Dira leten ushahidi wenu,sio kusema ahusiki,unayakumbuka ya eskro watubwa ikulu walihusika hapa,akina Gurumo walihojiwa,Omben sio malaika bhana,hao dira wanajua kuna sheria za kufungia magazet,next wek wakija na ushahid mtasema wa kupika
 
Kama wako confident na walichokiandika basi wasiombe radhi na wafunguke zaidi kuprove story yao; wakifungiwa waende mahakamani washitaki serikali; mbona Mwanahalisi walithubutu na wakaibwaga serikali! Hakuna mabadiliko yasiyo na victims; wasitake kutenda kishujaa halafu wakagwaya madhila; wakubali kuwajibika kwa matendo yao, na historia itawatambua hivyo!
 
Nadhan hili ndo linalotarajiwa
 
We chizi kweli kama unategemea magazeti ndio source kuu ya information,inadhihirisha jinsi gani upo level za chini za kupata habari.
We mbuzi wa kafara, nazungumzia picha Kenye magazeti, hutaki kuelewa shutdown
 
Wewe nawe ni kodonda tu, wenzio wanaimba ngonjera za Rais hajui kiingereza kule.
 
Ikulu wako sahihi; Double standards is a relative term depending on your corner of intetest; kwa hili unaonekana you are all out to settle scores na Sefue kwa sababu zako mwenyewe!!, kama Dira wana taarifa zenye mashiko waende Takukuru; vyombo vya habari vinaweza kuwa Whistleblower; tuhuma huchunguzwa polisi; takukuru na kesi hufanyika mahakamani!

Something rubbish is allowed to smear the forum!! Aliyetuhumiwa ni serikali au Sefue? Yaani Sefue akituhumiwa serikali ndo inajibu? Sefue ni mtu binafsi bila kujali madaraka yake, sawa na yule Daktari wa juzi aliyetumbuliwa na PM Majaliwa. Mbona PM hakumwambia yule mama aende PCCB?

Walio makini walitakiwa waanzie hapo hapo kumchunguza Ombeni Sefue kwa kutumia taarifa za gazeti kama walivyofanya kwenye bomba la mafuta. waliipa high rating gazeti kwa kufunua yaliyojificha na wakaenda kuthibitisha.
 
Tuhuma ni za Sefue kama Sefue (jipu), hapa alitakiwa ajitetee yeye. Na kwa kuanzia alitakiwa apeleke mashitaka yake media council au yeye Sefue aende mahakamani kuomba asafishwe, si kazi ya idara ya maelezo kumsemea Sefue. Wanasema, Sefue hajawahi wala hatawahi kuingilia zabuni, wanajuaje nafsi yake??? Wao ndo wasemaje wa Sefue? Anayetuhumiwa ni Sefue sio Serikali why idara ya maelezo wamtetee na kutisha chombo cha habari? Wao walichotakiwa ni kuomba kama kuna ushahidi au weledi umekiukwa wa habari hiyo tena baada ya Sefue kulalamika si wao kuwa wasemaji wa Sefue. Kuwa Katibu mkuu haimwondolei sifa yake ya wizi, kama anayo, na haimwondolei haki yake ya msingi ya kutuhumiwa kama kaiba. Sefue toka nje wewe mwenyewe useme, si kutuma watu wasiohusika.
 
Back
Top Bottom