Double standards: TAKUKURU yashindwa kuwachukulia hatua watoa rushwa wa CCM wasema chama ndio kiwachukulie hatua

Hatari sana, nimeona pia gazeti moja limemchafua sana Tundu Lisu Leo, Nikajiuliza hivi ndo ingekuwa magufuli kaandikwa hivi ingekuwaje.....Ila hivi vyombo vya serikali vijue kabisa kuwa Urais ni kupokezana , Leo huyo mnaempendelea kesho atakuwa mpinzani, na huyu mnarmkandamiza kesho ndo atakuwa rais, Sijui mtaficha wapi sura zenu. Kumbukeni Malawi, Kenya, Zimbabwe, Congo na nchi nyingine nyingi kuwa vyama tawala sasa hivi ndio vyama vya upinzani.
Jengeni hijo mueleweke. Hilo la sijui nchi gani ili kuwa hivi, mtasubiri sana.

TUKUTANE OKTOBA 28!
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
Kosa la rushwa haliishii kuondolewa kwenye uchaguzi, linatakiwa liishie mahakamani.
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
acha ujinga rushwa ni jinai sio swala la kisiasa
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
Kamati ya maadili vipi wakati watu wamekamatwa na Rushwa kabisa na sauti zipo zina trend hapo kwa kweli wanakosesha imani Wananchi juu ya taasisi hiyo nyeti
 
Hii imedhihirisha kuwa takukuru siku zote hufanya kazi kwa niaba ya ccm. ndio maana imerudisha mpira kwa 'mwajiri wake'. Kesi ya nyani imerudi kwa ngedere
 
JE! CHADEMA NI MNOFU LAINI KWA TAKUKURU NA CCM NI MFUPA MGUMU KWAO?

Tuhuma za 'matumizi mabaya' ya fedha zilizosadikiwa kuchangwa na Wabunge wa CHADEMA zilipelekea Wabunge wote wa CHADEMA kuhojiwa huku kamera zikiwamulika wakati wa kuingia na kutoka ndani ya Ofisi za TAKUKURU. Tuhuma za 'rushwa' katika mchakato wa uteuzi wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM zinaipelekea TAKUKURU hiyo hiyo iamue kuwa suala hilo lishughulikiwe na CCM yenyewe ndani ya CCM!

Mambo kama haya yanaleta ukakasi na yanaweza kujenga chuki na hasira katika mioyo ya watu dhidi ya mamlaka na watawala wao! Wenye mamlaka pamoja na vyombo vya dola pamoja na taasisi zilizopewa majukumu ndani ya nchi wawe makini sana katika kutenda haki isiyo na upendeleo!

Katika hili, maswali ni mengi zaidi kuliko majibu! Je, TAKUKURU imeonyesha hekima kwa kuwa kwa kufanya hivyo [kuchunguza rushwa ndani ya CCM] itakuwa inajichunguza yenyewe? Je, TAKUKURU inaogopa kushugulikia kwa kuwa safari hii 'haijatumwa'? Je, TAKUKURU imebaini kuwa zoezi litakuwa gumu kutokana na uwingi wa watu wanaotuhumiwa? Je, TAKUKURU inataka kuueleza umma kuwa tuhuma za rushwa ndani ya vyama vya siasa siyo sehemu ya majukumu yake?

Sauti zetu zinawakilisha idadi kubwa ya watu walio wanachama na wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa, wenye dini na wasiokuwa na dini. Zaidi ya yote, sauti zetu zinamuwakilisha pia YEYE aliyetutuma pasipo kujali udhaifu wetu, uchache wetu, na udogo wetu (Yeremia 1:4-10)!

Hivyo, ye yote atakayetuchukia sisi tunaohoji na kukemea atakuwa hajitendei haki yeye mwenyewe na watu anaowapenda kwa kuwa ni wajibu wetu kuwaonya na kuwakemea hata hao anaowapenda na kuwaheshimu ili waongoze vizuri ili wote tusitumbukie shimoni (Ezekieli 33:1-20).

Tunawalika watu wote kuimba wimbo uitwao 'Rehema na Hukumu' uliotungwa na Mfalme Daudi (Zaburi 101). Lakini kwa wasio waimbaji wanaweza kuanza kujifunza kuuliza maswali magumu kuhusiana na Haki kwa kusoma kitabu cha Habakuki katika Biblia.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Hatupaswi kuilaumu TAKUKURU kwa hatua hiyo, kwani imeamua kufanya hivyo ili kamati ya maadili ya CCM iweze kuwachukuliwa hatua wahusika wa vitendo vya rushwa kwa kuwaondolewa sifa za kugombea nafasi mabalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
Kwani mkuu mtu angeendelea na mashitaka yake na hao TAKUKURU na kamati ya maadili kupewa taarifa juu ya mtu wao si inatosha kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
 
Hizi taasisi kama Takukuru hazina maana ya kuwepo ni mizigo tu kwa walipa kodi ni sehemu tu ya watawala kuwapatia kazi vibaraka wao. Nothing more.
 
Back
Top Bottom