Tunawezaje kuzuia double agents, inazidi na itazidi kuwa changamoto

Kamkunji

Member
Sep 14, 2023
92
274
1. Mara ya kwanza nipo Bole International Airport kwenye harakati zangu akanifuata binti mmoja mwenye asili ya Comoro na Zanzibar, nafikiri yule ni mshirazi (mbwera), akaniuliza maneno mawili matatu, nikamjibu nilivyoweza, akaniambia anatoka Zanzibar anaelekea Seychelles(ushelisheli), katika kuzoeana pale wakati tuko transit(almost 2hrs), nikagundua huyu si mtu wa kawaida, akili ikagonga, alikua amevalia hijab na niqab, lakini sura ilikua inaonekana vizuri sababu baada ya story kunoga alitoa niqab kiasi, kutest uhalisia ya yale mambo aliyokua akinieleza nikamuomba tupige selfie kadhaa, mwanzoni akakataa, nikaweka noti, then baadae akakubali, nikaweka noti pia, nikabaki na ukumbusho wa sura maana dunia kijiji kuna siku naweza kutana nae, kuhusu elimu yake kasoma Zanzibar, then Uingereza kwa ufadhili wa serikali ya Zanzibar, ni Pilot na vyeti alinionesha, ila majina alificha, akasema hana kazi, so hua anapenda kusafiri, sasa anaenda kufanya nn ushelisheli, akaniambia mara nyingi hua kuna ndugu zake anaenda kuonana nao, baadae nikagundua ni mtu mwenye mahusiano ya karibu na baadhi ya viongozi wa serikali ya Zanzibar na ushelisheli kwa pamoja, nikanote kitu, possibly anakula huku na huku.

2. Mara ya pili nimeenda kumuona kiongozi fulani wa kisiasa nchi jirani, kwa hisani ya rafiki yangu, ilikua ghafla tu ili kutaka kujua kitu fulani cha kibiashara, nikakutana na kijana namfahamu kabisa, yupo pale ofisini, aliponiona ni kama hakutegemea, eye contact iligoma, kuhusu mwenyeji wangu, yeye hanifahamu vizuri na bahati nzuri kuna wakati utaifa wangu huchachanganya, hasa kwa majina yangu, na ninaweza kuongea lugha kadhaa za ukanda huu, kwa namna alivyoshtuka nikajua aliyokua anayafanya hayana afya kwa ustawi wake na nchi yetu, nikakausha mpaka leo, na wala sina mawasiliano nae, japo tukionana tunafahamiana.

3. Kuna yule kijana mwingine mweupe toka kanda ya kati, mtaalamu wa lugha ya kiswahili, sahivi yuko nchi jirani akitangaza vivutio vya utalii wa nchi hiyo na kusifia kila kilicho mbele yake, ni haki yake kufanya anachotaka na yuko huru kabisa, nafahamu inaweza kua kama nchi tuna manufaa nae lakini nikiongea kwa uzoefu wangu wa kuifahamu kanda hii na maeneo mengine mengi, nishauri wahusika, yule mtu asipewe access ya kujua mifumo na utendaji kazi wa nchi kiundani zaidi, kwa kisingizio cha lugha na diplomasia, hayo anayoyajua yanatosha. kati ya watu ambao instincts zangu zinaniambia si salama basi na yule yumo, tunaweza kuamua kumtumia kama nchi lakini nawaambieni kama hatukufanya hivyo miaka mitatu iliyopita, tumechelewa. Nazungumzia access za mifumo, si uteuzi wa kisiasa, huo uteuzi mtu yeyote anaweza kupata alimradi tu chama chenye nchi wameona unafaa

Lengo la uzi wangu huu ni kukumbusha kua, system zetu ziwe makini zaidi, siyo kila king'aacho dhahabu, vijana tunaowaamini wanafika bei kirahisi sana, kinachotokea wanatumwa kuleta taarifa hii wao wanapeleka kwanza za kwetu walizokusanya, halafu wanarudisha zile ambazo ni obvious kila mtu anaweza kuziona, Wengi wao ni millennials generation, hakuna namna ya kuwaridhisha isipokua tu kua makini, Double agents walikuepo, wapo na wataendelea kuwepo lakini isiwe kirahisi hivyo. Mdau wewe unaona kama nchi tufanye namna gani tafadhali?

Mbarikiwe nyote ndugu zangu.
 
Mnaidharau sana idara yaani double agent ww ambae sio proffesional umjue halafu watu wenye taaluma zao wasimfahamu sio kweli amini upo salama ndugu yangu watu hawalali kwa ajili yako
Idara gani unaizungumzia ndugu hii iliojaa uvccm nako unasema ni iadara mara ngapi majasusi ya kinyarwanda yapo full mitaa ya kwanzia Nyakahura hadi kahama hadi wengine wameoa na kuoa na wanaishi huku ni idara gani isiyokuwa na macho sembuse Ije igundue mtu aliefundwa akafundika?

Idara ilikuwa kipindi cha Nyerere hadi mkapa kidogo ilikuwa macho mno ila now ni twende sawa watoto wetu wasome shule nzuri na kula vizuri mengine majaaliwa
 
1. Mara ya kwanza nipo Bole International Airport kwenye harakati zangu akanifuata binti mmoja mwenye asili ya Comoro na Zanzibar, nafikiri yule ni mshirazi (mbwera), akaniuliza maneno mawili matatu, nikamjibu nilivyoweza, akaniambia anatoka Zanzibar anaelekea Seychelles(ushelisheli), katika kuzoeana pale wakati tuko transit(almost 2hrs), nikagundua huyu si mtu wa kawaida, akili ikagonga, alikua amevalia hijab na niqab, lakini sura ilikua inaonekana vizuri sababu baada ya story kunoga alitoa niqab kiasi, kutest uhalisia ya yale mambo aliyokua akinieleza nikamuomba tupige selfie kadhaa, mwanzoni akakataa, nikaweka noti, then baadae akakubali, nikaweka noti pia, nikabaki na ukumbusho wa sura maana dunia kijiji kuna siku naweza kutana nae, kuhusu elimu yake kasoma Zanzibar, then Uingereza kwa ufadhili wa serikali ya Zanzibar, ni Pilot na vyeti alinionesha, ila majina alificha, akasema hana kazi, so hua anapenda kusafiri, sasa anaenda kufanya nn ushelisheli, akaniambia mara nyingi hua kuna ndugu zake anaenda kuonana nao, baadae nikagundua ni mtu mwenye mahusiano ya karibu na baadhi ya viongozi wa serikali ya Zanzibar na ushelisheli kwa pamoja, nikanote kitu, possibly anakula huku na huku.

2. Mara ya pili nimeenda kumuona kiongozi fulani wa kisiasa nchi jirani, kwa hisani ya rafiki yangu, ilikua ghafla tu ili kutaka kujua kitu fulani cha kibiashara, nikakutana na kijana namfahamu kabisa, yupo pale ofisini, aliponiona ni kama hakutegemea, eye contact iligoma, kuhusu mwenyeji wangu, yeye hanifahamu vizuri na bahati nzuri kuna wakati utaifa wangu huchachanganya, hasa kwa majina yangu, na ninaweza kuongea lugha kadhaa za ukanda huu, kwa namna alivyoshtuka nikajua aliyokua anayafanya hayana afya kwa ustawi wake na nchi yetu, nikakausha mpaka leo, na wala sina mawasiliano nae, japo tukionana tunafahamiana.

3. Kuna yule kijana mwingine mweupe toka kanda ya kati, mtaalamu wa lugha ya kiswahili, sahivi yuko nchi jirani akitangaza vivutio vya utalii wa nchi hiyo na kusifia kila kilicho mbele yake, ni haki yake kufanya anachotaka na yuko huru kabisa, nafahamu inaweza kua kama nchi tuna manufaa nae lakini nikiongea kwa uzoefu wangu wa kuifahamu kanda hii na maeneo mengine mengi, nishauri wahusika, yule mtu asipewe access ya kujua mifumo na utendaji kazi wa nchi kiundani zaidi, kwa kisingizio cha lugha na diplomasia, hayo anayoyajua yanatosha. kati ya watu ambao instincts zangu zinaniambia si salama basi na yule yumo, tunaweza kuamua kumtumia kama nchi lakini nawaambieni kama hatukufanya hivyo miaka mitatu iliyopita, tumechelewa. Nazungumzia access za mifumo, si uteuzi wa kisiasa, huo uteuzi mtu yeyote anaweza kupata alimradi tu chama chenye nchi wameona unafaa

Lengo la uzi wangu huu ni kukumbusha kua, system zetu ziwe makini zaidi, siyo kila king'aacho dhahabu, vijana tunaowaamini wanafika bei kirahisi sana, kinachotokea wanatumwa kuleta taarifa hii wao wanapeleka kwanza za kwetu walizokusanya, halafu wanarudisha zile ambazo ni obvious kila mtu anaweza kuziona, Wengi wao ni millennials generation, hakuna namna ya kuwaridhisha isipokua tu kua makini, Double agents walikuepo, wapo na wataendelea kuwepo lakini isiwe kirahisi hivyo. Mdau wewe unaona kama nchi tufanye namna gani tafadhali?

Mbarikiwe nyote ndugu zangu.
Mkuu unamuonaje Bongozozo?yule jamaa siyo mtu wa kawaida na viongozi wetu wanamshobokea sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
jambo la ajabu siku hizi ni kua ni rahisi sana hawa watu kujulikana, hasa waliochukuliwa kipindi cha mwishoni cha msoga,
Ni kawaida sana watu wanakumbia tu yule sasa hivi ni usalama
 
Back
Top Bottom