Dotto Bulendu: Tumefika Hapa? Hakika Tumepoteza Mwelekeo kama Taifa

Ameandika Mwandishi Dotto Bulendu

1.Amejeruhiwa na Risasi mchana kweupe,wenzake pamoja na Kiongozi wao mkuu wa mhimili wakaenda kumuona hospital ya Rufaa akiwa hajitambui,anavuja damu,haongei wala hajui chochote.

2.Alipelekwa Hospital Nairobi bila uficho,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Makamu wa Rais wa nchi wakaenda Nairobi kumuona na kumpa pole.

3.Familia yake ikaandika barua ofisini kwake kuomba apatiwe haki yake ya matibabu,ofisi yake ikajibu kuwa haiwezi kubeba hizo gharama kwani utaratibu wake wa kwenda Nairobi Hospital eti haukufuatwa.

4.Akatangazwa kusitishiwa mshahara wake,akalalamika baadae akarudishiwa mshahara Kama ilivyo kawaida.

Akiwa kitandani anaupambania uhai wake,akatangazwa kuwa amefutwa ubunge kwa madai kuwa hajulikani alipo na hajajaza fomu za mali na madeni za watumishi kwa mujibu wa sheria,kuondoshwa kwenye ubunge kwa tuhuma hizi kutamuweka nje ya ulingo wa kuwania nafasi za uwakilishi za kisiasa mfano Ubunge na Urais kwa miaka mitano.

Haki ya msingi ya binadamu yeyote ni haki ya kuishi,ndiyo maana linapokuja suala la kupigania Uhai gari la kubeba wagonjwa halifungwi na sheria za barabarani maana tunalenga kuokoa uhai wa binadamu.

Mtu mwenye utu,anayeamini Mungu yupo,anayesali Kanisani ama msikitini au popote hawezi weka masharti kwenye suala la kuokoa uhai wa mtu.

Mtu mwenye utu,anayemuogopa Mungu hawezi fanya sherehe ya kufurahia bunadamu mwenzake kupita kwenye tishio la kupoteza uhai.

Mtu anayemuogopa Mungu hawezi shabikia tishio ana jaribio la binadamu mwenzake kuuawa,leo kama kuna mtu anamdhikahi mtu aliyenusulika kifo na kuwa sehemu ya mkakati wowote wa kumzidishia mateso binadamu yeyote aliyepo duniani kwa kusudi la Mungu akasome Mwanzo,Zaburi,injili,Ufunuo na Quran tukufu aone kama kuna sehemu inayosema tufurahie mateso ya wenzetu.

Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Maandiko matakatifu yanatuambia amri kuu kuliko zote ni Upendo,kweli tumefika mahali upendo siyo sehemu ya maisha na sasa tunaweza furahia mateso ya binadamu?

Sheria tulizotunga wenyewe zinasema Uhai ni moja ya msingi mkuu wa binadamu,Uhai hauna mbadala,ukitoka umetoka,leo kweli tunajenga jamii ya watu wanaoweka masharti makali dhidi ya binadamu anayepigania uhai wake?

Leo tumefika mahali binadamu wanapelekena kwenye vyombo vya sheria tena za binadamu kuvutana kwa hoja kuwa mgonjwa alikosea ama hakukosea kupambania uhai wake?

Leo tunajenga jamii inayokusubiri unasuke na kifo halafu ianzishe mjadala wa kama ulikosea ama kupatia kuupambania uhai wako?

Ni jamii hii hii inayosali kwa kusema...

"Eeeh mwenyezi Mungu Mtukufu ,
Muumba Mbingu na Dunia
Umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabunge ya mataifa ili haki yako itendeke""

Kila nikisoma mistari hiyo, najiuliza ni haki gani tunaizungumzia? wakati haki ya kwanza ya binadamu yeyote ni uhai?leo tuna jamii isiyoguswa na uhai wa binadamu,ipo tayari kwenda kubishana kisheria eti binadamu aliyeupambania uhai wake kakosea na anastahili Adhabu?

Ni Mungu yupi tunayemtaja kila siku?ama kuna Mungu mwingine ambaye hatambui thamani ya uhai na ameweka mipaka ya namna ya kuupambania uhai?maana jumapili iliyopita nilipokwenda kusali,tukaambiwa Mungu wetu hapendi watu wanaojikweza na waliojaa viburi.

Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu,tusubiri kukwezwa na tusijikweze,tunajenga jamii ya watu wenye viburi,wasiostushwa na kuono mioyo ya watu inajazwa chuki.

Eeeh Mwenyezi Mungu utusaidie.
Kinachotokea afrika ya kusini ndicho alichofanyiwa tundu lissu dodoma bensaa8 azory gwanda Alphonso mawazo na wengine wengi tu
 
Dotto Bulendu namfahamu vizur Sana na Ni ndugu yangu wa karibu Sana. lkn lazima nikili kwamba....
Tangu kusitishwa kakipindi kake Flani pale star TV na kauwezo kake ka kufikiri kameshuka Kama 37% ivi,yaani anacopy tu matukio pumba tupu ataki kuumizwa kichwa
I hope kilichomtokea Lissu, kimpate mzazi wako, au wewe au mtoto wako au yeyote unaempenda.
 
Unitukane, unidhihaki, unidhalilishe duniani, uisaliti nchi ninayoiongoza, uniite dikteta, uniite rubbish, bado nikuangalie, nikutibie, nikulipe mshahara, nikulindie kibarua chako. Kwani we umekuwa nani Mungu??!! Au binadamu namba moja duniani?!! Mwambieni kwanza ajifunze kuheshimu watu na mamlaka..mengine ataongezewa. Vinginevyo hata kidogo alicho nacho atanyang' anywa.
Nakuombea mzazi wako au watoto wako au nduguyo amiminiwe risasi na watu wasiojulikana siku moja
 
Dotto Bulendu wewe ni Mhadhiri hapo SAUT Main Campus. Ebu ondokaka kazini bila kutoa taarifa rasmi kwa uongozi uone kama hicho kibarua utaendelea kuwa nacho. Hata kwenye kusomea "ufather" ulipigwa chini kwasababu hukufuata misingi halafu unawatetea wengine. Ajabu sana!

Wewe ni kati ya watu wasiokuwa na akili kabisa ondoka kazini kwa maana hiyo huyu aliondoka kazini? na kwa taarifa yako huyu atalipa tena asilimia 100% ya WCF kw kuwa aliumia akiwa kazini tena hata asipokuwa mbunge kwa next 20 years ataishi bila shida yoyote.. Ukiniambia mkewe ndio kasimamishwa kazi hapo nitaelewa ... Tundu Lissu kapata ulemavu wa kudumu mguu na bado unatubutu kuna na cheap argument hapa.
 
Uoga na unafki
Ulianza taratibu but siku zinavyosogea unazidi kuongeza speed!!! Mwanzoni ulizuga kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa but nowadays unafanya kweli.
Sijui uoga? Unafiki?;? Njaa?!? Au umetishiwa?!?

All the best coz naamini unachokifanya unakijua na malengo unayo.
 
Polisi,viongozi na watu mbalimbali waliuawa kwa kupigwa risasi pale Kibiti lakini hukuweza kulaani kwa kuandika makala kama hii Ila umeona TL ni more human than those who were killed by unidentified gun men.

My Take: We are all equal in eyes of GOD
Kwani Lissu anahusika vipi na vifo vya Kibiti jamani?
 
Kuna maswala ukiyaandika kwa ushabiki yanaharibu. Tunapotoa maoni kwenye maswala ya kitaifa hasa kwa mwalimu na mwandishi wa habari kama Dotto lazima uweze kuweka mizani ya habari zako vizuri, wazungu wanasema balance report.

Kwenye uzi huu Dotto umeongelea bahari za kifo na Mateso aliyopitia Lisu, pili umeongelea vyazifa zake za uongozi.
Kwenye mateso aliyopitia sitaki niongelee sana hapa, ila nitaongelea badae.
Ninachotaka kusema kwa sasa ni kwamba Kupoteza kwa ubunge wake kuna watu lazima wafurahie kwa sababu zifuatazo.
1. Lissu ametumia uhuru wake wa kujieleza vizuri sana hadi kupitiliza.
2. Lissu anatumai maneno makali sana hadi yanaumiza na kukela watu.
3. Lissu anamuandama sana Rais wa nchi hadi anasahau hata kazi yake ya Ubunge kiasi kwamba wafuasi wa Rais na Rais mwenyewe wanakeleka. Kwa nini umukele mwenzako wakati anatekeleza majukumu yake ya kitaifa kwa kiasi kile?
4. Lissu kaamua kwenda nchi za nje huko kwenda kumkela tu Rais wa nchi na watanzania, huku akiomba TZ ikose ushirikiano wa kimataifa, Bahati mbaya wamempuuza huko.
5. Lissu mekuwa mtu wa kufurahis nchi inapokosea na inaposhitakiwa badala ya kusaidia jinsi ya kuninasua na badala yake anatumia maneno ya kejeli sana kukosoa na kuona wenzake hawana akili.
Lissu asizani kumkela mkuu wa nchi unaweza ukawa huru na salama popote pale duniani.

Tujifunze kuwa na kiasi.

Nakushauri Dotto uwe unaweka usawa . kama unataka kuwe na furaha hii nchi lazima kila mmoja aambiwe kosa lake katika jamii.

Kuna makosa hayawezi kupelekwa mahakamani ila lazima yakemewe kijamii na kwa kalamu. Lissu aonywe, anakela watu na wanakosa Amani moyoni.
The fact that hujui kuspell "kukela - kukera"....says it all. Kwahiyo kwavile Lissu alikua anamkosa Rais ndio anastahili kupigwa risasi na sasa wamvue ubunge?Tumia akili. Hivi Uhuru Kenyatta anasakamwa anatukanwa, umesikia hata siku moja Raila amepigwa risasi? Tatizo la Tanzania ni elimu na nidhamu ya uoga. Aliyewaambia Rais hakosolewi ni nani? Rais ni Mungu? Wewe hapo ulipo kesho ukichaguliwa kuwa Raisi, would that make you God kwamba hutakosea? Kwanini Rais anaumia hivyo kukosolewa mpaka aone kutoa roho za watu ndio suluhisho? Hizo ni dalili za mtu ambae hana sifa za kuwa kiongozi. Yeye ni mtawala na sio kiongozi. Mnakerekwa na kukosa amani ya moyo hivyo mnaona suluhisho ni kuua. Haya basi Mungu kawaonyesha kwamba only HE decides when someone's life is over in this world. Na hata mkimuua Lissu, watatokea Lissu wengine 10, mtafanya kazi ya kuua watu.
 
Ndio maana nikasema lazima tubalance mambo, ukiona unamkela mwenzio shituka. Leo hii Rais akikosoa kitu lazima watu walalamike, akisema tu Mbowe ni mpuuzi na mjinga, habari ziafika hadi ulaya. Kila mtu ajarubu kuheshimu mwingine. Tofauti na Urais JPM pia anafamilia na watoto..he needs respect.
Ujanja ujanja wa kusema Rais halosolewi ni mwamvuli wa kujifichia tu lakini huwezi ukawa unamkosoa mtu kwa lugha na kejeli, kukela, kutukana, mara mpumbavu, mara hana hakili, mara bogasi, mara mshamba..hiyo sio heshima.
Tumieni lugha za staha.

Unaongelea Odinga na Kenyata.. naomba uwaache hao watu saivi wanakula kuku Ikulu wako pamoja. Acha.
 
Jeez!! Elimu Elimu Elimu
 
kwan lissu aliondok bila taarifa?kwa akili yako alikua anakula bata Nairobi na Ubelgiji?pumbafu sanaa,eti nae mama yako alishikwa uchungu kuzaa bumunda kama ww
Kutukana ni utamaduni was nyumbu kama wewe. Taasisi hazifanyi kazi kama unavyofanya na mkeo. Labda Ufipani kwa nyumbu kama nyie!
 
Wewe ni kati ya watu wasiokuwa na akili kabisa ondoka kazini kwa maana hiyo huyu aliondoka kazini? na kwa taarifa yako huyu atalipa tena asilimia 100% ya WCF kw kuwa aliumia akiwa kazini tena hata asipokuwa mbunge kwa next 20 years ataishi bila shida yoyote.. Ukiniambia mkewe ndio kasimamishwa kazi hapo nitaelewa ... Tundu Lissu kapata ulemavu wa kudumu mguu na bado unatubutu kuna na cheap argument hapa.
Hiyo nako anaweza ASILIPWE kama sheria itafutwa. Huyo ni mhuni. Anatumia ujinga wenu was kutokujua kuwaadaa. Lakini kwa Serikali makini ya JPM, Bunge adilifu la Ndugai na Mahakama yetu inayosimamia kweli na haki Lissu hana chake! We muibie mumeo mpelekee. Lakini huku HAPANA!
 
Dotto Bulendu namfahamu vizur Sana na Ni ndugu yangu wa karibu Sana. lkn lazima nikili kwamba....
Tangu kusitishwa kakipindi kake Flani pale star TV na kauwezo kake ka kufikiri kameshuka Kama 37% ivi,yaani anacopy tu matukio pumba tupu ataki kuumizwa kichwa
mtu anayetetea uhai na haki, tena bila malipo na hata kusababisha akose malipo, daima uwezo wake wa kufikiri utakuwa juu. anayetetea tumbo na daima kuunga mkono juhudi ili apate msosi daima uwezo wa kufikiri utashuka chini
 
It depends na mwendo kasi wa dereva wetu kama basi lina abiria 100, na liko mwendo kasi wa speed 180km/h, halafu kuna mtu amejitokeza ghafla na kusimama kati kati ya barabara ili kuzuia safari, ungekua wewe ndio dereva, unafanyaje?. Kwa mwendo huu ukichuna break kwa nguvu, tairi zina bust kwa friction, gari inapinduka kwa kubinuka kwa mbele linakuwa kichwa chini miguu juu na kuendelea kuserereka, unaua abiria 100 kwa kumkwepa mtu mmoja?. Ukimkwepa, kutokana na high velocity, gari inapoteza mwelekeo na kupinduka kwa bingiri bingiri kwa upande upande kwa kuwafirigisha watu kama mashine ya kufulia nguo, kuchinja abiria wote, katika situation kama hiyo, kama wewe ndio dereva, unaamua nini?.
P
Mayalla mbona unavunja moyo hivi ?!. Duh kama ni post uipate ipumzishe nafsi yako. Kwa kungojea hiyo post utajikuta unafanya dhambi.

Lissu hakuwa mtoro. Alikimbizwa matibabuni huku hajutambui. Leo unamhukumu as if ni mtoro. Nasari uliona nani kalalamika ?!. Suala lake lilikuwa tofauti . Lilikuwa na utoro.
 
Tena usikute miongoni mwa abiria kuna wadunguaji, walipomuona tuu yule mtu aliyesimama kati kati ya barabara, na wanajua lazima dereva atampitia tuu na kwa vile amesimama lazima pia atasababisha impact, waduguaji wanaoweza kuamua kumlaza kwanza chini ili kupunguza impact, ndipo gari inampitia kwa juu na kuendelea na safari mwendo mdundo as if nothing happened!. Uamuzi wa kumlaza sio wa dereva, yeye dereva aliambiwa aendelee tuu kuendesha as if mbele hakuna kitu.

Usikute hata siku ile naohodha wetu alipozungumzia kinachofanywa vitani kwenye usaliti, na akasema wazi wazi, tuko vitani kwenye vita vya kiuchumi, na vita ya kiuchumi ni mbaya kuliko vita ya kawaida, vita ya kawaida adui unamjua unamuona unamuwahi kabla hajakuwahi, lakini vita ya kiuchumi, adui humjui, na aliposema tuu kuwa kuna mmoja simu yake tumeidukua, pale pale vijana wa kazi wakaingia kazini kusafisha barabara, kabla gari ya mwendokasi haijamfikia, wakaamua kumlaza kabla na hata bila kumwambia dereva kuwa wanamsafishia njia, dereva yeye kazi yake iwe ni moja tuu, kuendesha huku macho mbele, kanyaga mafuta, kanyaga mwendo, mwendo mdundo, mbele kwa mbele asitazame pembeni hadi tufike safari yetu.
P
Yah , yawezekana hakujua !!. Lakini ndiyo asikemee kweli ?! Hao uliowaita abiria hawawezi kuwa na maono ya kufanana. Wengine watamuonea Imani mtu aliye barabarani .

Akemee jambo hili ni la aibu kwa taifa.
 
Ujanja ujanja wa kusema Rais halosolewi ni mwamvuli wa kujifichia tu lakini huwezi ukawa unamkosoa mtu kwa lugha na kejeli, kukela, kutukana, mara mpumbavu, mara hana hakili, mara bogasi, mara mshamba..hiyo sio heshima.
Tumieni lugha za staha.
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom