Dotto Bulendu: Tumefika Hapa? Hakika Tumepoteza Mwelekeo kama Taifa

Hivi ndiye huyu huyu Tundu Lisu aliyekwenda kutukashifu BBC na Marekani? Kama ni hivyo hakuna sababu ya kumwonea huruma, maana hata yeye hana hiyo roho ya huruma. Wacha abebe msalaba wake mwenyewe.
 
Unitukane, unidhihaki, unidhalilishe duniani, uisaliti nchi ninayoiongoza, uniite dikteta, uniite rubbish, bado nikuangalie, nikutibie, nikulipe mshahara, nikulindie kibarua chako. Kwani we umekuwa nani Mungu??!! Au binadamu namba moja duniani?!! Mwambieni kwanza ajifunze kuheshimu watu na mamlaka..mengine ataongezewa. Vinginevyo hata kidogo alicho nacho atanyang' anywa.
Hata Al bashiri alikuwa anatamba na maneno kama hayo lakini Leo hakuna ajuaye wale mahabusu na wafungwa walio kule kwenye gereza alilopelekwa wanamfanya nini!
Hata wababe wengi tuu wameishia hivyo.
 
Duh! Una roho ngumu. .. Unafanyaje hivi mpaka mtu unakua na roho ngumu kama yako?
Huyu atakuwa na undugu na yule jinga aliyetaka kuchukua nafasi ya mkuu wake kisha akatupwa kutoka kwenye sehemu yenye barabara za dhahabu na kuandaliwa ziwa la moto.
 
Hivi ndiye huyu huyu Tundu Lisu aliyekwenda kutukashifu BBC na Marekani? Kama ni hivyo hakuna sababu ya kumwonea huruma, maana hata yeye hana hiyo roho ya huruma. Wacha abebe msalaba wake mwenyewe.
A
 
Ametelekeza daaah!
IMG_20190917_093616.jpeg
 
*Anaandika Dotto Bulendu wa DW-Sauti ya Ujerumani Na Star TV*

1.Amejeruhiwa na Risasi mchana kweupe,wenzake pamoja na Kiongozi wao mkuu wa mhimili wakaenda kumuona hospital ya Rufaa akiwa hajitambui,anavuja damu,haongei wala hajui chochote.

2.Alipelekwa Hospital Nairobi bila uficho,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Makamu wa Rais wa nchi wakaenda Nairobi kumuona na kumpa pole.

3.Familia yake ikaandika barua ofisini kwake kuomba apatiwe haki yake ya matibabu,ofisi yake ikajibu kuwa haiwezi kubeba hizo gharama kwani utaratibu wake wa kwenda Nairobi Hospital eti haukufuatwa.

4.Akatangazwa kusitishiwa mshahara wake,akalalamika baadae akarudishiwa mshahara Kama ilivyo kawaida.

Akiwa kitandani anaupambania uhai wake,akatangazwa kuwa amefutwa ubunge kwa madai kuwa hajulikani alipo na hajajaza fomu za mali na madeni za watumishi kwa mujibu wa sheria,kuondoshwa kwenye ubunge kwa tuhuma hizi kutamuweka nje ya ulingo wa kuwania nafasi za uwakilishi za kisiasa mfano Ubunge na Urais kwa miaka mitano.

Haki ya msingi ya binadamu yeyote ni haki ya kuishi,ndiyo maana linapokuja suala la kupigania Uhai gari la kubeba wagonjwa halifungwi na sheria za barabarani maana tunalenga kuokoa uhai wa binadamu.

Mtu mwenye utu,anayeamini Mungu yupo,anayesali Kanisani ama msikitini au popote hawezi weka masharti kwenye suala la kuokoa uhai wa mtu.

Mtu mwenye utu,anayemuogopa Mungu hawezi fanya sherehe ya kufurahia bunadamu mwenzake kupita kwenye tishio la kupoteza uhai.

Mtu anayemuogopa Mungu hawezi shabikia tishio ana jaribio la binadamu mwenzake kuuawa,leo kama kuna mtu anamdhikahi mtu aliyenusulika kifo na kuwa sehemu ya mkakati wowote wa kumzidishia mateso binadamu yeyote aliyepo duniani kwa kusudi la Mungu akasome Mwanzo,Zaburi,injili,Ufunuo na Quran tukufu aone kama kuna sehemu inayosema tufurahie mateso ya wenzetu.

Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Maandiko matakatifu yanatuambia amri kuu kuliko zote ni Upendo,kweli tumefika mahali upendo siyo sehemu ya maisha na sasa tunaweza furahia mateso ya binadamu?

Sheria tulizotunga wenyewe zinasema Uhai ni moja ya msingi mkuu wa binadamu,Uhai hauna mbadala,ukitoka umetoka,leo kweli tunajenga jamii ya watu wanaoweka masharti makali dhidi ya binadamu anayepigania uhai wake?

Leo tumefika mahali binadamu wanapelekena kwenye vyombo vya sheria tena za binadamu kuvutana kwa hoja kuwa mgonjwa alikosea ama hakukosea kupambania uhai wake?

Leo tunajenga jamii inayokusubiri unasuke na kifo halafu ianzishe mjadala wa kama ulikosea ama kupatia kuupambania uhai wako?

Ni jamii hii hii inayosali kwa kusema...

"Eeeh mwenyezi Mungu Mtukufu ,
Muumba Mbingu na Dunia
Umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabunge ya mataifa ili haki yako itendeke""

Kila nikisoma mistari hiyo👆👆👆,najiuliza ni haki gani tunaizungumzia?wakati haki ya kwanza ya binadamu yeyote ni uhai?leo tuna jamii isiyoguswa na uhai wa binadamu,ipo tayari kwenda kubishana kisheria eti binadamu aliyeupambania uhai wake kakosea na anastahili Adhabu?

Ni Mungu yupi tunayemtaja kila siku?ama kuna Mungu mwingine ambaye hatambui thamani ya uhai na ameweka mipaka ya namna ya kuupambania uhai?maana jumapili iliyopita nilipokwenda kusali,tukaambiwa Mungu wetu hapendi watu wanaojikweza na waliojaa viburi.

Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu,tusubiri kukwezwa na tusijikweze,tunajenga jamii ya watu wenye viburi,wasiostushwa na kuono mioyo ya watu inajazwa chuki.

*Eeeh Mwenyezi Mungu utusaidie.*
 
UTAWALA UKIIUPONDA HADHARANI LAZIMA UTAKUTWA NA MASWAIBU,SIJUI HASOMI HABARI ZA KABENDERA!!!?
 
Mama Samia Suluhu hata baada ya kufika Nairobi Hospital hufahamu Lissu alipo?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ibilisi, ibilisi, ibilisi, ibilisi, ibilisi mbaya sana anaitafuna Tanzania vipandevipande bila huruma,
 
Kwenye kaburi la Ndugai itabidi lipandwe maua ya saa nne no siyo maua yaa nne, itabidi lipandwe michongoma
 
*Anaandika Dotto Bulendu wa DW-Sauti ya Ujerumani Na Star TV*

1.Amejeruhiwa na Risasi mchana kweupe,wenzake pamoja na Kiongozi wao mkuu wa mhimili wakaenda kumuona hospital ya Rufaa akiwa hajitambui,anavuja damu,haongei wala hajui chochote.

2.Alipelekwa Hospital Nairobi bila uficho,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Makamu wa Rais wa nchi wakaenda Nairobi kumuona na kumpa pole.

3.Familia yake ikaandika barua ofisini kwake kuomba apatiwe haki yake ya matibabu,ofisi yake ikajibu kuwa haiwezi kubeba hizo gharama kwani utaratibu wake wa kwenda Nairobi Hospital eti haukufuatwa.

4.Akatangazwa kusitishiwa mshahara wake,akalalamika baadae akarudishiwa mshahara Kama ilivyo kawaida.

Akiwa kitandani anaupambania uhai wake,akatangazwa kuwa amefutwa ubunge kwa madai kuwa hajulikani alipo na hajajaza fomu za mali na madeni za watumishi kwa mujibu wa sheria,kuondoshwa kwenye ubunge kwa tuhuma hizi kutamuweka nje ya ulingo wa kuwania nafasi za uwakilishi za kisiasa mfano Ubunge na Urais kwa miaka mitano.

Haki ya msingi ya binadamu yeyote ni haki ya kuishi,ndiyo maana linapokuja suala la kupigania Uhai gari la kubeba wagonjwa halifungwi na sheria za barabarani maana tunalenga kuokoa uhai wa binadamu.

Mtu mwenye utu,anayeamini Mungu yupo,anayesali Kanisani ama msikitini au popote hawezi weka masharti kwenye suala la kuokoa uhai wa mtu.

Mtu mwenye utu,anayemuogopa Mungu hawezi fanya sherehe ya kufurahia bunadamu mwenzake kupita kwenye tishio la kupoteza uhai.

Mtu anayemuogopa Mungu hawezi shabikia tishio ana jaribio la binadamu mwenzake kuuawa,leo kama kuna mtu anamdhikahi mtu aliyenusulika kifo na kuwa sehemu ya mkakati wowote wa kumzidishia mateso binadamu yeyote aliyepo duniani kwa kusudi la Mungu akasome Mwanzo,Zaburi,injili,Ufunuo na Quran tukufu aone kama kuna sehemu inayosema tufurahie mateso ya wenzetu.

Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Maandiko matakatifu yanatuambia amri kuu kuliko zote ni Upendo,kweli tumefika mahali upendo siyo sehemu ya maisha na sasa tunaweza furahia mateso ya binadamu?

Sheria tulizotunga wenyewe zinasema Uhai ni moja ya msingi mkuu wa binadamu,Uhai hauna mbadala,ukitoka umetoka,leo kweli tunajenga jamii ya watu wanaoweka masharti makali dhidi ya binadamu anayepigania uhai wake?

Leo tumefika mahali binadamu wanapelekena kwenye vyombo vya sheria tena za binadamu kuvutana kwa hoja kuwa mgonjwa alikosea ama hakukosea kupambania uhai wake?

Leo tunajenga jamii inayokusubiri unasuke na kifo halafu ianzishe mjadala wa kama ulikosea ama kupatia kuupambania uhai wako?

Ni jamii hii hii inayosali kwa kusema...

"Eeeh mwenyezi Mungu Mtukufu ,
Muumba Mbingu na Dunia
Umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabunge ya mataifa ili haki yako itendeke""

Kila nikisoma mistari hiyo👆👆👆,najiuliza ni haki gani tunaizungumzia?wakati haki ya kwanza ya binadamu yeyote ni uhai?leo tuna jamii isiyoguswa na uhai wa binadamu,ipo tayari kwenda kubishana kisheria eti binadamu aliyeupambania uhai wake kakosea na anastahili Adhabu?

Ni Mungu yupi tunayemtaja kila siku?ama kuna Mungu mwingine ambaye hatambui thamani ya uhai na ameweka mipaka ya namna ya kuupambania uhai?maana jumapili iliyopita nilipokwenda kusali,tukaambiwa Mungu wetu hapendi watu wanaojikweza na waliojaa viburi.

Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu,tusubiri kukwezwa na tusijikweze,tunajenga jamii ya watu wenye viburi,wasiostushwa na kuono mioyo ya watu inajazwa chuki.

*Eeeh Mwenyezi Mungu utusaidie.*
Ngoja wakuzingire
 
Hekima ingetumika kidogo kuonyesha kwamba tukio lililofanywa na watu wasiojulikana limetusikitisha wote. Na kwakuwa ni watu wasiojulikana jitihada za kumhudumia mgonjwa zinaendelea kufanyika bila kujali matatizo binafsi ya mgonjwa
 
Balozi nani ?
Sky, hii serikali ni majanga, aliyekuwa Balozi wetu huko Belgium alifutwa kazi baada ya kwenda kumuona Lissu hospitalini nchini humo, alionekana kana kwamba anataka kuthibitishia dunia kwamba serikali inajua Lissu alipo, akafutwa kazi ya UBalozi
 
Back
Top Bottom