1. Hata kama uko makete hakikisha walau mara moja kila wiki unawasha AC kwa muda usiopungua nusu saa kusudi AC ya gari yako idumu.
2. Kila baada ya kupita kwenye mazingira yenye vumbi vumbi kagua cabin filter, ibadilishe ikibidi ili AC yako iendelee kukupa hewa safi
3. Epuka safari za mwendo mdogo (mf below 60km/hr) kwa muda mrefu. Kama kuna ulazima wa kusafiri kwa spidi ndogo kila mara (kwa sababu ya foleni au ubovu wa barabara) hakikisha unapata safari ya mwendo kasi (angalau 80km/hr) kila wiki au baada ya wiki mbili kuiweka gari katika hali nzuri
4. Usisahau betri za maji zinahitaji ku-refill mara kwa mara ili betri yako idumu
5.Taa ya oil ikiwaka wakati wowote gari ikiwa inatembea hakikisha unapunguza mwendo haraka na kusimama ( haijalishi kama uko katikati ya serengeti). Ni kwa faida yako na gari yako.
6. Taa yoyote (hasa usiyoielewa) ikiendelea kuwaka kwenye dashboard (hata kama gari inaweza kutembea) waone wataalamu mara moja.
7. ....mengine itabidi tuweke tozo kidogo...ha ha ha...watu wanaweza kugraduate humuhumu bure..lol