Mkuu hapo namba mbili gari inapokuwa kwenye mwendo haiwezekani kupiga gear ya reverse na ukaingia, mfano ukiendesha let say gari yako ni manual wakati unabadilisha gear toka na.3 kwenda na.4 hata kama itatokea bahati mbaya gia liva umeipeleka usawa wa reverse itapiga kelele kisha wewe unaivuta kushoto kidogo inaingia
Kwa upande wa automatic hapa kidogo kuna shida kwa kuwa madereva wengi huwa tunaingia barabarani kwa kuwa ni rahisi kuliendesha ila nalo reverse haiwezi kuingia kama gari lipo kwenye mwendo kwani gia liva inapokuwa pale kwenye D wengi anapoihamisha kwenda kwenye neutral huwa wanaisogeza huku amebonyeza ile button kubwa juu ya over drive (hapa ndio penye shida kwani gari ya automatic kutoka D kwenda Neutral unasukuma tu bila kubonyeza ikifika kwenye N inagota na haiendi kwenye reverse na the same kama ukiisogeza kwenye D 2 nako inasogea ila ukitaka iende L au reverse ndio unabonyeza ile button. Hii huwa inawakumba wale wazee wa kutaka kutumia neutral kwenye mteremko wanajisahau kusogeza tu gia liva wao wanasogeza gia liva huku wamebonyeza (jaribu tu kesho uone maana gia liva ya auto inasogea freely kwenye D, N na 2 inapokuwa kwenye mwendo except kwenye L na R ndipo unabonyeza kitufe kikubwa ndio inaingia