Don't risk to destabilizing Rwanda-warns President Kagame

Don't risk to destabilizing Rwanda-warns President Kagame

Wananyea kambi mkuu wamesahau kuwa ni TZ ndiyo iliyosabisha RPF waruhusiwe kuingia Rwanda kabla ya 1994 kupitia mazungumzo ya Arusha. Wakati ule tulipokuwa tunataka haki itendeke kumbe wao walidhani tunawapendelea, sasa hivi tunataka wawape nafasi wapinzani wao wanafungua midomo ya kashfa. Uzuri ni kuwa watz huwa hatusahau acha waendelee kutuvutia kwenye jukwaa la chuki maana najua mwisho watavuna mabua. Muda si mrefu watagundua kuwa hizo alliances uchwara za CoW ni mbwembwe tu.

Just FYI RPF fought from Uganda and didn't need any permission to attack and defeat your hero Habyarimana/interahamwe and COW is real na wanafanya vitu vyao acha wivu wa k-isenge ..sad thing about your post ni hao id-iots waliokupa likes
 
Tatizo lenu mko so blinded with hate,bias etc or just uninformed,hizo nonsense backed with nothing ulizoandika is just ridiculous and pure allegations kwa mtu yeyote anayefikiria vizuri,open up use hard numbers and stats from independent and credible org or institution to judge and rate Rwanda sio kuja hapa na garbage generalization mnazotuletea daily...Rwanda is doing fine na hairudi nyuma.

Tatizo lako unadhani kila anayefikiri tofauti basi ana chuki, hapana. Tunaongea kwa upendo na sio chuki. Ukimpenda mtu unamuelekeza.

Mie sio Mnyarwanda, ni Mtanzania, hivyo sina sababu ata chembe ya kuwa na chuki iwe na Kagame wala na kabila lolote la Rwanda, na mie binafsi nilikuwa namkubali sana Kagame toka 1994.

Katika miaka miwili hii, nimepata fursa ya kuhusiana na Wanyarwanda wa nyanja tofauti, na hicho ndicho nilichokiona. Na fahamu kwangu ilikuwa picha tofauti kabisa na niliyokuwa naiwazia, before nilikuwa nadhani Rwanda ilishatoka kule ilipokuwa kabla ya 1994, na nilipokuwa naona chaguzi Kagame anashinda kwa zaidi ya 95%, na zaidi ya 80% ni Wahutu nikajua sasa Rwanda imeshapona, lakini nilichokiona ndipo nilipoelewa kwanin ata Sadam Hussein alikuwa anashinda kwa 95%, watu wana chuki lakini ni police state, unaweza kuuita utakavyo lakini kiuhalisia ule ni "utawala tu wa kijeshi uliopo Rwanda kwa sasa", hivyo raia wanaogopa kuonyesha hisia zao hadharani.

Kwa sababu ya chuki ilivyojaa na kutoridhika kwa wengi kuongozwa na serikali wasiyoitaka, sioni namna ya hali hii kudumu kwa muda mrefu, hakuna namna ya nchi kuwa salama kama majority hawaioni serikali kuwa ni "yao" na kuwa ipo "kwa ajili yao".

Koba, kama u Mnyarwanda, ongezeni sasa juhudi katika maridhiano,ndio pona pekee ya Rwanda.

Naamini ata Kagame nae anatambua hilo ndio maana sasa anahangaikia sana Muungano wa Kisiasa wa Afrika Mashariki upatikae mapema iwezekanavyo, ili Afrika Mashariki ifunike matatizo ambayo otherwise hayazuiliki Rwanda, lakini lazima awe na plan B pia, kwani hakuna namna ya Afrika Mashariki itakayozitawala nchi zilizo chini yake bila ridhaa ya nchi zenyewe, na wakati wowote nchi hizo zitaweza kujitoa zikitaka.

Hivyo hakuna namna ya kuepuka utawala ambao majority ya Wanyarwanda watautaka, atengeneze sasa angali na nguvu mazingira ya Wanyarwanda kujiona wamoja, kujiona wote wapo sawa, na kuufanya utawala huo "ujao wa walio wengi" usiwe na madhara kwa "wachache".
 
kitu cha ajabu, wewe unayeongea ulikuwa mkimbizi ukakimbilia tz wakati wa kibano huko kwenu mfulukyunyozini kigali. umeishi tz upepata makazi hapa, chakula na choo ya kujisaidia, ukaenda shule na kujua hata kiswahili, umekua umerudi kwenu unawatukana watanzania. hii ndio inafanya dunia nzima ione watusi ni watu ambao sio wa kuwaamini wala kushirikiana nao. imagine, if today rwanda kikinuka tena, mtakuja tz wakati kwa sasa moja ya adui namba moja ya rwanda ni tanzania? na mmeguko wa uhusiano kati ya watz na wanyarwanda ambao kagame amesababisha hautakuja kuisha kamwe, na bahati mbaya its not more of tz risk, nyie ndio mtapoteza zaidi kuliko sisi.

operation kimbunga isingefanyika kama wasingekuwepo watu kama wewe rwanda, zaidi ya wanyarwanda 6000 walikuwa sacrificed kwasababu ya midomo michafu kama ya aina yako tu. comment ambazo ninyi mnazifanya zinasomwa na watz wote wa kawaida hadi viongozi wetu wa juu na hatred kati ya wanyarwanda na watz inazidi kuongezeka siku hadi siku. kuna siku mtakuja kutafuta sehemu ya kukimbilia kwasababu nakupa miaka 5 ijayo, kama kagame hatakuwa ameondoka madarakani, basi wahutu na watusi wa rwanda wataungana kumwondoa kinguvu na ikipidi kwenda msituni wakisaidiwa na tz, south africa na congo.
ugua pole ndugu yangu ..usifikiri ukisaidia mtu unahaki hata ya kuingilia maisha yake..kuna mpaka..ina maana jamaa akikusaidi utanyamaza hata akilala na mke wako??hiyo ni fact huwezi nisaidi na mwishowe u support watu walio niulia familia yangu unategemea nitakubali??huo ni unafiki hapo hakuna mapenzi yoyote,there is aline you can not cross.
 
Umeongea kwa mantiki lakini umesahau jambo moja tu, hakuna mtu yeyote anayeweza kuwafanya wanyarwanda wawe wakabila, ila tatizo lililopo ni kuwa watu walio wengi, ambao imetokea kuwa wengi wao ni wahutu, zaidi ya 80% hawapo happy na utawala huu na wanaamini huu ni utawala wa wachache.

Ndio maana namna nzuri kwa Kagame kufanya, ilikuwa ni kutafuta maridhiano kati ya makundi haya ya wanyarwanda, kutumia ubabe kuwazuia kusema, hutaweza kufanya hivyo milele, ndio maana wanaoona amani na utulivu wa Rwanda kwa namna ulivyo sasa sio endelevu.

Kutana na Mhutu yeyote, awe Mfanyabiashara, awe Mchungaji, awe Padre, awe Shekhe, au awe serikalini kwenyewe, wengi wao watakwambia huu sio utawala wao, na wana hasira kweli na utawala huu mpaka unashangaa kuwa kumbe hapa moto uliopo ni mkali sana japo bado hauonekani kwa nje. Hapo ndio utakapojua kuwa tatizo la Rwanda ni kubwa kuliko RDLR, tatizo ni kuwa majority, Wahutu hawaioni serikali ya Kagame kama serikali yao, bali serikali ya kidhalimu na ya kimabavu ya wachache.Hili ndilo tatizo.

Kikwete hakusema vile kwa kukosea, yeyote anayefungamana na Wanyarwanda na atalifahamu hili.Kagame ana nafasi ya kurekebisha hayo angali ana nguvu ya kufanya hivyo, vinginevyo future ya Rwanda bado ipo shakani, na hasa future ya Kagame, familia yake na ya walio wachache katika Rwanda.
Mimi sikuelewi...unamaana wahutu hawamkubali pk kwa sababu ni mtusi au kwasababu hawezi kuongoza??je..una maana kwamba kwa sababu wahutu ni wengi basi lazima kiongozi mkuu awe muhutu???sasa hiyo demokrasi iko wapi??kama ndio hivyo basi kikwete asingekua rais wa tanzania.
 
fine: lets say wahamiaji haramu toka Rwanda wanakimbia social services nzuri za serikali, how stupid of them! Lazima watakuwa interahamwe na FDLR tu wanaotaka kuipaka matope serikali ya kagame kwa kuonyesha dunia kuwa kuna shida Rwanda, wakati ni nchi ya maziwa na asali!
Wewe unatatizo kubwa sana..ni kuulize watanzania wangapi wamejazana southafrika,uchina,amerika,msumbiji...uganda,rwanda..nk.je hao watakua wamekimbia utawala mbovu au uchumi mbovu??kuwa na wanyarwanda tanzania ni sawasawa na kua na watanzania sehemu nyingine za dunia.
 
Mkuu, kagame alichofanya ni hivi: toka 1994 mauaji yale UN na dunia nzima yalikuwa yanaitwa Rwandan genocide, yakikubali kimsingi kuwa makabila yote yameuana kwa ukabila, interahamwe wameua watutsi, na jeshi la kagame limeua wahutu. Ilipofika mwaka 2000 wakimbizi wa kihutu DRC wakachoka kuvamiwa na kuuwawa na kagame wakaunda chama cha FDLR. Kagame kuona kwamba hawa FDLR watasikilizwa na international community ndio akaamuru definition ibadilike kuwa "genocide against tutsis" na akatunga sheria kali ndani ya Rwanda kusisitiza hilo, halafu ndio akaanza kampeni za kutaka hawa FDLR ndio wawe wahusika wa hiyo "genocide against tutsis".
Wewe muulize shabiki yoyote wa kagame humu ndani kwa nini ilichukua miaka 6 kwa definition kubadilika 2000 wakati mauaji yalikuwa 1994? uone jinsi atakavyobabaika.
Genocide ilikua ya watusi tu,kama ingekua ya wahutu nafikiri hivi sasa wahutu wangekua minority na mtusi awe majority kwani uwezo wakufyeka muhutu haukukosekana wakati ule..imagine wahutu waliorudishwa wakati wa vita ya congo,kumbuka wahutu waliorudishwa toka benaco kwanini hawakuuwawa?achana na hao baada ya vita niwahutu wangapi walibaki majumbani mwao na hawakufanywa kitu?hii ndio inaonyesha mtusi hakua na mpango wa kuua wahutu,na muhutu aliyeuwawa ni wale interahamwe na ex-FAR na wao ni wale waliokua wakileta upinzani vitani,kwahiyo usifananishe mambo.
 
Wewe unatatizo kubwa sana..ni kuulize watanzania wangapi wamejazana southafrika,uchina,amerika,msumbiji...uganda,rwanda..nk.je hao watakua wamekimbia utawala mbovu au uchumi mbovu??kuwa na wanyarwanda tanzania ni sawasawa na kua na watanzania sehemu nyingine za dunia.

1. Kwanza angalia idadi, "mnaojazana" ni nyie wanyarwanda, sio wabongo, wabongo wahamiaji haramu ni wawili watatu tu katika hizo nchi. sisi tuliwafukuza ndugu zako over 15,000! wewe nipe idadi inayofanana na hiyo ya wabongo wahamiaji haramu katika nchi moja ANYWHERE IN THE WORLD! wapi utapata kauli kama "watanzania 1000 warudishwa kwao"? Can you imagine wanyarwanda wahamiaji haramu ndugu zako nchi nyingine kama DRC wako wangapi? Uganda je?
2. na na vile vile angalia quality ya hao wahamiaji watanzania wanahamia nchi nyingine kutafuta kazi sio kuishi tu kwa sababu nyumbani hakukaliki. Watanzania wanapiga box hawaendi kuishi maporini huko america! Tofauti na mnyarwanda aliye radhi kuishi maporini na fisi Tanzania kuliko Rwanda kwenye laptop mashuleni!
 
usizuge bwana, tumefukuza wanyarwanda zaidi ya 15,000! kwa operesheni kimbunga, na sasa hivi tunaambiwa tayari wameshaanza kurudi maporini kwetu. Halafu wewe unatuletea ngonjera za social services nzuri za Rwanda, hivi ni nani mwenye akili timamu akimbie social services akaishi maporini nchi jirani? Hivi ni nani hataki mwanae wa shule ya msingi asomee laptop na Ipad tunazoimbiwa na serikali ya kagame aje aishi maporini kagera? Get real chief! Hatusemi Rwanda hamna kitu lakini hatukubali hizi propaganda za kitoto.
wewe kweli uko usingizini...unafikiri watu wote mahitaji yao ni mamoja?kuna watu wanaopenda kutumia mambo ya kimaendeleo na kunawenhine hupenda kuishi maporini kama hao unao wasema na wengi ni wafugaji na kwa bahati mbaya rwanda hakuna mapori ya kufugiamo ng'ombe,kila mfugaji anatakiwa kufugia ngombe zake zizini na anashauriwa kufuga hawa ng'ombe wa maziwa...nafikiri mpaka hapo umenielewa kwanini wanakuja huko..siyo uongozi mbaya.
 
Genocide ilikua ya watusi tu,kama ingekua ya wahutu nafikiri hivi sasa wahutu wangekua minority na mtusi awe majority kwani uwezo wakufyeka muhutu haukukosekana wakati ule..imagine wahutu waliorudishwa wakati wa vita ya congo,kumbuka wahutu waliorudishwa toka benaco kwanini hawakuuwawa?achana na hao baada ya vita niwahutu wangapi walibaki majumbani mwao na hawakufanywa kitu?hii ndio inaonyesha mtusi hakua na mpango wa kuua wahutu,na muhutu aliyeuwawa ni wale interahamwe na ex-FAR na wao ni wale waliokua wakileta upinzani vitani,kwahiyo usifananishe mambo.

1.Hoja yako ina hatari ya genocide denial, funny as it sounds. Genocide haina uhusiano na namba, wakiuawa watu watatu out of 100 under genocidal conditions hiyo ni genocide. Mauaji yanaitwa genocide kutokana na dhamira ya wauaji, utaratibu wa mauaji n.k sio tu namba.
2. kabla ya kutunguliwa ndege 1994, RPA walikuwa wameshateka na ku-control sehemu kubwa sana ya Rwanda for years since 1990. Cha ajabu na huko nako zikatoka maiti za genocide against tutsis, including upande wa ule mto uliotiririsha maiti kuja TZ! hivi interahamwe na vijipanga vyao vya mchina waliwezaje kupenya kati kati ya ngome za RPA, kuchinja watutsi, halafu kurudi past RPA to DRC?
3. Nikufahamishe kuwa wahutu wakimbizi ni wale ambao walikuwa in direct line ya njia za RPA kuingia mijini, mfano kama RPA walikuwa wanatokea Moro kuja dar, wakimbizi ni watu ambao walikuwa wanaishi around hiyo barabara, hao ndio walikuwa wanakimbia kwa sababu RPA walikuwa wanaua wahutu as they go. Hivi hujiulizi kwa nini international community iliwapa status hao wakimbizi kama wakimbizi na sio kama ex-FAR, interahamwe blah blah? Ni kwa sababu ni kweli ni wakimbizi sio vinginevyo. Mtu kama wewe hutaki kukubali kuwa wahutu hawa ni wakimbizi because sababu ya ukimbizi wao ni mauaji ya kagame!
4. Umesema vizuri kuwa "ni wale waliokuwa wakileta upinzani vitani". I agree with you. Idadi kubwa ya wahutu waliouawa ni wahutu ambao hawakutaka kutawaliwa na kagame. Hawa sio interahamwe wala genocidaires wala FAR wala nini, hawa ni wananchi wa kawaida ambao hawataki nchi yao itawaliwe na REBELS! Hili ndio tatizo la Rwanda hivi sasa. Kagame hana legitimacy kwa majority ya watu wa Rwanda, they did not choose him, he overthrew the gov, na kuweka mifumo ambayo itamfanya awe kiongozi milele. mwisho wa siku ordinary rwandese view him as just a tutsi rebel from uganda that took their country.
RPA haikuwa supported na majority ya wanyarwanda, bali a minority of tutsis and some token hutus. Wanyarwanda walikuwa upande wa serikali ya Habyarimana that's why kulikuwa na mazungumzo ya Arusha. Ingekuwa wanyarwanda hawamtaki Habyarimana kagame asingepata tabu kupigana na serikali kwa miaka minne, wahutu wenyewe wangempindua Habyarimana. So ordinary hutus had the right ya kufanya kila kilichowezekana to fight the RPA.
Na mkiendelea na misimamo yenu ya ajabu ajabu mtakuwa wakimbizi tena hivi karibuni, kwa sababu kimsingi most of Rwandese are ideologically FDLR!
 
wewe kweli uko usingizini...unafikiri watu wote mahitaji yao ni mamoja?kuna watu wanaopenda kutumia mambo ya kimaendeleo na kunawenhine hupenda kuishi maporini kama hao unao wasema na wengi ni wafugaji na kwa bahati mbaya rwanda hakuna mapori ya kufugiamo ng'ombe,kila mfugaji anatakiwa kufugia ngombe zake zizini na anashauriwa kufuga hawa ng'ombe wa maziwa...nafikiri mpaka hapo umenielewa kwanini wanakuja huko..siyo uongozi mbaya.

kwa hiyo wanaacha health insurance cover, access to hospitals, access to good schools with laptops and all that because they are "wafugaji wanaopenda kuishi porini". Okay sir, nimezinduka usingizini sasa.
 
Mimi sikuelewi...unamaana wahutu hawamkubali pk kwa sababu ni mtusi au kwasababu hawezi kuongoza??je..una maana kwamba kwa sababu wahutu ni wengi basi lazima kiongozi mkuu awe muhutu???sasa hiyo demokrasi iko wapi??kama ndio hivyo basi kikwete asingekua rais wa tanzania.

Uhalali wa serikali sio kuweza au kutoweza kuongoza bali kuwa ni serikali ya watu, na inayokubaliwa na watu walio wengi katika nchi husika.

Suala sio uhutu wala ututsi wa mtu, bali suala hapa kuwa Wanyarwanda walio wengi wanaiona hii serikali sio yao, na utawala wowote ni lazima uwe utawala wa wananchi husika.

Sasa kama bahati mbaya kwa Rwanda kuwa kundi moja, la Wahutu, lina watu wengi maradufu kuliko kundi lingine, hiyo ni fact ambayo hatuwezi kuibadili sasa.

Muhimu ni kujengwa maridhiano ya makabila na watu kujiona ni wamoja na wenye haki na hadhi sawa kama Wanyarwanda na kuijenga nchi yao.

Hofu kuwa ni lazima Mtutsi aongoze Rwanda ili Watutsi wawe salama sio hofu ya kweli, inawezekana kujenga jamii moja inayokubaliana na inayojali Urwanda wao kuliko kabila lao.Na hapa ndipo Rwanda inapopaswa kwenda, na tatizo Kagame kama walivyokuwa interahamwe ni sehemu ya kikwazo cha kujenga maridhiano hayo, maana nae ni sehemu ya hivyo vidonda vinavyowatonesha wengine maana RPF pia walifanya mauaji.

Kumbuka mfano wa Afrika Kusini tu hapo, weusi ni wengi kuliko makaburu, lakini mpaka leo makaburu wa Afrika Kusini wanaishi kwa amani na tena kiuchumi sasa wamenufaika zaidi kuliko ata walivyokuwa wanatawala kwa nguvu.

Hatujaona kuona Makaburu wakiuawa au kuonewa na majeshi ya serikali eti kwa sababu serikali inaongozwa na walio wengi ambao ni weusi.Inawezekama na Rwanda pia.

Angalia ata Burundi tu hapo, makabila hayohayo, na sijaona mauaji ya Watutsi japo serikali inaongoza sasa na Mhutu tena aliyekuwa muasi aliyekuwa anapigana vita kwa silaha.

Inawezekana Wanyarwanda kuishi kwa amani bila hofu kwa pande zote, ila kulazimisha kuwatawala walio wengi kwa nguvu za kijeshi bila ridhaa yao na kutafuta maridhiano ya kudumu ni hatari sana na hakuisaidii Rwanda, kinachofanyika ni kuhamisha tu tatizo na kama nilivyosema ni "kuufunika moto kwa majani".
 
Genocide ilikua ya watusi tu,kama ingekua ya wahutu nafikiri hivi sasa wahutu wangekua minority na mtusi awe majority kwani uwezo wakufyeka muhutu haukukosekana wakati ule..imagine wahutu waliorudishwa wakati wa vita ya congo,kumbuka wahutu waliorudishwa toka benaco kwanini hawakuuwawa?achana na hao baada ya vita niwahutu wangapi walibaki majumbani mwao na hawakufanywa kitu?hii ndio inaonyesha mtusi hakua na mpango wa kuua wahutu,na muhutu aliyeuwawa ni wale interahamwe na ex-FAR na wao ni wale waliokua wakileta upinzani vitani,kwahiyo usifananishe mambo.

Nadhani hujui kuwa ata Wangeuawa Wahutu Million 3 bado wangebaki kuwa majority Rwanda, hakukuwa na namna ya kuwafanya wawe minority.

Lakini wangeuawa Watutsi laki 8 basi kusingekuwa na mtutsi ata mmoja aliyebaki Rwanda.

Kama unaamini waliuawa watutsi pekee labda kama kwa tafsiri yako unamaana kuwa wahutu sio watu.

USHAURI: USIPOTEZE KITAMBULISHO CHAKO CHA KUPIGIA KURA CHA TANZANIA NA RUDI MARA MOJA UCHUKUE PIA KITAMBULISHO CHA URAIA CHA TANZANIA MAANA KITAKUJA KUWA MUHIMU SANA KWAKO...kama Kagame ataendelea na approach yake hii ya kutotafuta maridhiano.
 
1. Kwanza angalia idadi, "mnaojazana" ni nyie wanyarwanda, sio wabongo, wabongo wahamiaji haramu ni wawili watatu tu katika hizo nchi. sisi tuliwafukuza ndugu zako over 15,000! wewe nipe idadi inayofanana na hiyo ya wabongo wahamiaji haramu katika nchi moja ANYWHERE IN THE WORLD! wapi utapata kauli kama "watanzania 1000 warudishwa kwao"? Can you imagine wanyarwanda wahamiaji haramu ndugu zako nchi nyingine kama DRC wako wangapi? Uganda je?
2. na na vile vile angalia quality ya hao wahamiaji watanzania wanahamia nchi nyingine kutafuta kazi sio kuishi tu kwa sababu nyumbani hakukaliki. Watanzania wanapiga box hawaendi kuishi maporini huko america! Tofauti na mnyarwanda aliye radhi kuishi maporini na fisi Tanzania kuliko Rwanda kwenye laptop mashuleni!
kweli wewe si mwanauchumi katika population kuna tabaka mbalimbali..kama vile wakilima,wafugaji,wataalamu katika nyanja mbalimbali na hatamahitaji yao ni tofauti,na ukumbuke hizi nchi zetu parcentage kubwa ni wakulima na wafugaji..na ukumbuke kunatofauti kubwa kati ya tanzania na rwanda..tanzania wana aridhi kubwa ambayo iko under utilized..na rwanda wana aridhi ndogo na watu wengi,sasa huko kuhama kwa watu kunatokana na mahitaji yao binafsi..kama ni mfugaji atahsmia dehemu yenye eneo lakutosha kufanyia ufugaji wake,na kama ni mkulima atahamia sehemu yenye aridhi ya kutosha kufanyia ukulima wake,kama ni mtaalamu atahamia sehemu yenye kazi na kulipa vizuri ndio maana watanzania wengi walioko rwanda ni wataalamu siyo wakulima au wafugaji,na ndio maana wanyarwanda wengi walioko tanzania ni wakulima na wafugaji..sasa usitake kuhusisha watu wanao tafuta kazi na uongozi uliopo madarakani,huwezi zuia mtanzania anaye hama tanzania na kuenda rwanda kutafuta kazi na mnyarwanda anayehamia tanzania...
 
Labda niweke hivi : huwezi kusema wasomali wahamiaji haramu wanakimbia kile kile somalia, anachokimbia mtanzania tanzania.
 
Nadhani hujui kuwa ata Wangeuawa Wahutu Million 3 bado wangebaki kuwa majority Rwanda, hakukuwa na namna ya kuwafanya wawe minority.

Lakini wangeuawa Watutsi laki 8 basi kusingekuwa na mtutsi ata mmoja aliyebaki Rwanda.

Kama unaamini waliuawa watutsi pekee labda kama kwa tafsiri yako unamaana kuwa wahutu sio watu.

USHAURI: USIPOTEZE KITAMBULISHO CHAKO CHA KUPIGIA KURA CHA TANZANIA NA RUDI MARA MOJA UCHUKUE PIA KITAMBULISHO CHA URAIA CHA TANZANIA MAANA KITAKUJA KUWA MUHIMU SANA KWAKO...kama Kagame ataendelea na approach yake hii ya kutotafuta maridhiano.

...huyo kagame mwenyewe na yeye atafute vitambulisho vyake vya Uganda.
 
sijakataa kwamba wahutu hawakufa..ninacho sema katika mauaji ya kimbari target ilikua mtusi peke yake..hao wahutu waliokufa ilitokana na mapigano yaliyotokea ili kusimamisha haya mauaji..wengi wao walikua hao wauaji..na ukiniambia kwamba ni wengi kuzidi watusi waliokufa sitashangaa kwani na wao walikua wengi kuzidi watusi na walikua mobilized nchi nzima...na kwa taalifa yako majority ya watusi walioko rwanda..wengi walikua wakiishi ukimbizini waliokua wakiishi rwanda wakati huo ni wachache sana na wengi waliokolewa na majeshi ya RPF..sisi tunachoongelea ni kwamba hapakuwepo double genocide hatakidogo...kama kuna muhutu alikufa wakati huo ni consequency ya waliyokua wakifanya wakati huo...jamaa walikua wamegeuka vichaa kwa sababu ya damu za watusi walikua hawaogopi hata risasi.
 
Labda niweke hivi : huwezi kusema wasomali wahamiaji haramu wanakimbia kile kile somalia, anachokimbia mtanzania tanzania.
hapo uko right....ndio maana wengi wa watanzania rwanda ni wataalamu na wengi wa wanyarwanda tanzania ni wakulima na wafugaji...wasomali wao wanakimbia vita na ukumbuke rwanda hakuna vita ni nchi ya amani.
 
Huna haja ya kupanic, wakati mwingine ni vizuri kusikiliza, au kusoma kuupata upande wa pili nwa shilingi. Kuna usioweza wewe kuyaona lakini yapo wazi kwa wengine.Na sote tunaitakia heri Rwanda ila tofauti na wewe tunaona hatari iliyo mbele.

Rafiki mzuri atakueleza mapungufu na sio kukusifia wakati muelekeo wako hauna mwisho mwema, kutoona mapungufu kwenye approach ya Kagame kwa faida ya amani ya kudumu ya Rwanda ni ishara ya upofu.
ungejua kwamba approach ya pk ndio imewezesha rwanda kua na amani!kwanza pk alitoa msamaha kwa wauaji wengi tu,na hilo liliku uchungu kwa watusi,kwani watusi wengi walitamani kufanya revenge lakini hawakuruhusiwa kufanya hivyo,wahutu wote walieuhusiwa kusoma bila ubaguzi lakini wakati wa utawala wa wahutu haikua hivyo,wahutu walirudishwa kazini hata jeshini,jiulize umewashinda adui zako but unaamua kushirikiana nao,fdlr wanarudi nakuookelewa vizuri na kupewa mitaji ya kuanzisha maisha,sijui ni reconciliation ipi unataka?..kitu ambacho pk hawezi fanya ni kuwapa jukwaa wauaji na kuongea nao kamavile hakuna kibaya walichofanya na hiyo itakua tusi kubwa kwa wapinga genocide na wahanga wa genocide...lakini option ya kupewa msamaha ipo siyo kuwapa jukwaa.
 
Siku ipo na itakuja ambayo majority wa Wanyarwanda watahitaji kuiweka serikali ya inayokubaliwa na walio wengi.

Rwanda kwa sasa ni moto uliofunikwa kwa majani, hakuna future kwa Rwanda bila maridhiano.

Majority wa Wahutu hawapo happy, na huwezi kuwa na nchi ya majority hawapo happy na utawala alafu utegemee utengamano wa kudumu.
Sasa kwa maoni yako rwanda itawaliwe na muhutu? Kwasababu ni wengi?basi tanzania ingetakiwa kutawaliwa na msukuma badala ya kikwete kutoka kabila dogo.
 
...huyo kagame mwenyewe na yeye atafute vitambulisho vyake vya Uganda.

Kwa sirka ya Kagame, nadhani yeye atafia Rwanda either akiwa madarakani au kwa kufanyiwa na maadui zake.

Ila ni muhimu kwake kuitafutia familia yake makazi salama mbali na Rwanda, Uganda ni karibu sana, haitakuwa safe kwa familia yake.
 
Back
Top Bottom