Sasa kwa maoni yako rwanda itawaliwe na muhutu? Kwasababu ni wengi?basi tanzania ingetakiwa kutawaliwa na msukuma badala ya kikwete kutoka kabila dogo.
Suala sio Rais atoke kabila gani bali suala hapa ni Rais akubaliwe na majority wa nchi husika, na sio kuwatawala kinguvu.
Kwa mfano wa Tanzania unaweza ona mfano Kikwete alipata kura nyingi Tabora kuliko za Lipumba mwenyeji wa Tabora, ndio watu hao, wanamchagua Rais wao bila kujali katoka kabila gani, waTanzania walio wa makabila tofauti wamemchagua wengi Kikwete bila shuruti awe Rais wao na waliomkataa wapo huru kumpinga kwa uhuru bila kukamatwa wala kuuawa kama ilivyo kwa Rwanda.
Na hapa ndio Tanzania tulipofanikiwa, na ndipo ambapo Kagame ameshindwa na haelekei ata kuwa na dhamira ya kufanya hivyo.
Ni muhimu sana kwa Rwanda kuelekea njia hiyo ya maridhiano ya kujenga undugu kati ya jamii za Rwanda utakaopelekea amani ya kudumu.