Ndugu Kibona,
Nashukuru kwa tafakari yako.
Binafsi nimejaribu kutaka kujua zaidi kuhusu hiyo hotuba ya Kagame ila kinyarwanda kimetumika zaidi na siifahamu hiyo lugha.
Ila nadhani kila tamko linategemea kilichoulizwa au kujadiliwa.
National Dialogue ina maana ya maongezi au majadiliano ya kitaifa. Na bila shaka Rwanda haiwezi kujadili maswala ya kitaifa kiusalama bila kujadili maswala ya vita na FDLR. Mfano, Rais Obama hawezi kujadili usalama wa USA bila kuongelea al-qaeda au ISIS kwa sasa.
Mimi nisingependa kuunga mkono upande wowote ila najadili mantiki ya uwepo wa mijadala mingi kuhusu Rwanda ndani ya forum yetu pamoja na kwamba Rwanda ni nchi jirani na kwa namna moja au nyingine matatizo yao yanatuathiri.
Point ni kuwa tumeshuhudia matusi ya watusi na wahutu humu ndani pindi wanapojadili issues zao. Badala ya ku argue wanaenda mbali na matusi mengi.
Uhutu au utusi si dili. Sisi tuna makabila zaidi ya 120 na bado tunaishi kwa kistaarabu na chaguzi zetu mara zote zimewaweka kwenye uongozi watu wanaotoka makabila madogo ila wakichaguliwa na watu wengi. Wao bado wanajadili MAJORITY Vs MINORITY kikabila. Tumeshuhudia hata viongozi wetu walio wajinga wakizungumzia Rwanda kwa vigezo kama hivyo. Huu ni "ujinga". Na hapa ndo natofautiana na akina Mukama... au jMali wanaojadili kikabila.
Wananchi tunataka uongozi usiogonganisha watu bali kuwaunganisha. Kuongea ukabila karne ya 21 ni sawa na Baba anayembaka binti yake.
Tuaombee hawa wanyarwanda watazamane kwa uti na si ukabila. Awaonyeshe yaliyo mema kwa kila upande badala ya kuona wenzao kutoka upande hasi (negative side).
Anjo
mkuu, sijui ni kwanini umeniunganisha na watu ambao wana-support ukabila Rwanda. Mimi kama mtanzania siwezi kushabikia ukabila popote pale. Huwezi kufuta makabila ila unaweza kufuta ukabila. Tanzania hatuna Ukabila ila tuna makabila. Na hakuna mtu anasema kuwa ili tusiwe na ukabila basi iwe marufuku kusema wachaga, wahaya, wasukuma n.k That would be madness. Mbona sisi hatuna ukabila lakini makabila yapo?
Kagame ndio mkabila namba moja, anasema "hakuna watutsi wala wahutu kuna wanyarwanda tu", halafu anajaza watutsi kwenye nafasi zote za uongozi, nafasi zote nyeti kuanzia wajumbe wa nyumba kumi mpaka mawaziri, jeshini etc. Sasa kwa Rwanda kuna mainly kabila mbili tu na wote wanajuana. watutsi ni minorities kwa less than 15% wakati wahutu ni kama 80%, kwa namna hiyo you can't fool anybody, huwezi kuwa na minorities dispropotinately hivyo kwenye madaraka. Ni sawa sawa na wahindi wa TZ wawe kama watutsi wa Rwanda madarakani Tanzania, hilo halitawezekana except by deliberate efforts kama anazofanya Kagame.
Hata leo hii wasauzi ni wamoja, lakini haitatokea mawaziri wote, wakuu wa majeshi ya polisi, jeshi la nchi, wanamaji, anga..., usalama wa taifa, wajumbe wa nyumba kumi mpaka wabunge...., wakuu wa shule..., huko koote kuwe na wasauzi weupe (makaburu wa zamani) halafu uanze kusema sisi tunaosema sema ni "wajinga", everything is well, south africa is one!
Tatizo la Rwanda ni hili: HAKUNA UMOJA WA KITAIFA. Rwanda bado sio TAIFA ni NCHI TU, same problem ipo kwenye nchi zingine kama BURUNDI hata na KENYA ingawa wao kidogo wamepiga hatua. Katika mazingira ya kutokuwa na UMOJA WA KITAIFA, huwezi hata kidogo kutengeneza nchi isiyo na ukabila kama TANZANIA. Anachotakiwa kufanya ni kujenga umoja wa kitaifa ambao utawafanya makabila yote yajione sawa.
Kukosekana kwa umoja wa kitaifa ndio kunatengeneza kutokuaminiana. watutsi na wahutu hawajapatana, they simply live together, tolerate each other in fear of kagame. Ukweli ni kuwa hata victoire ingabire asingepiga kampeni leo hii angekuwa rais, kwa sababu wahutu given the chance watampigia kura mhutu mwenzao just to get rid of the tutsis. Na watutsi nao kama kagame wanajua hili ndio maana wanajazana kwenye nafasi zote nyeti hata ikibidi kuchukua watutsi raia wa nchi nyingine kama Tanzania, kenya, DRC etc, alimradi tu watutsi wamecover hizo nafasi.
Kwa watu wenye akili tunaona hili halitakwisha until there are genuine talks aimed at true nation reconciliation.
Umesema kuna viongozi wetu "wajinga" wanazungumzia hili, well, mmojawapo ni Thabo Mbeki aliyesema hivi kuhusu mgogoro huu: "Majority must be represented while minority must be protected". Sijui kama na yeye anaingia kwenye orodha yako ya "wajinga" sisi ila basically that's what i think should be done in Rwanda.
Hata marekani nayo imezungumzia hili kupitia hii cable hapa chini, sidhani nao ni "wajinga" kama jmali, mbeki na kikwete.
"(C/NF) As Ambassador Arietti noted in his departing message (reftel), Rwanda remains a deeply divided society, and average Rwandans still identify closely with their ethnic origins. Some Hutus argue that the massive gacaca program, now completing the judgment of over one million (Hutu) genocide cases, like the nationwide campaign against "genocide ideology," which by definition only Hutus could manifest, particularly now that the 1994 genocide has been renamed "the Tutsi genocide," are secondarily intended to keep Hutus off balance, unwilling to serve in high places (for fear of being brought low) and generally out of office. For example, new Minister of State for Education Theoneste Mutsindashyaka recently addressed 750 secondary school headmasters, and, according to the pro-government New Times, angrily told them that 80 percent of them were "masterminds of genocide ideology." Assuming that headmasters match the general ethnic breakdown in society, the Minister essentially accused every Hutu in the room being a genocide ideologist."
source:
Cable: 08KIGALI525_a