Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,550
- 729,440
Mchawi anayejipendekeza kupaa bila kupata maarifa kamili hujikuta akipiga mweleka mkubwa sana kutokana na uzito wake au vinginevyo
Na huko angani kuna tufani za kila aina Usijaribu kupitisha helicopter yako kwenye anga la Boeing hutafika safari yako
Lakini pia kwenye kupaa kuna mahesabu yake...kwamba utapaa upande gani na umbali gani na urefu gani.kwamba kama unaenda Lamu kwa mwendo wa kawaida pengine ni masaa matatu hivi lakini wewe unataka kwenda kwa sekunde tatu tuu inabidi ujigawe roho na mwili yani unacheza kamari na Mungu
Kwahiyo unautanguliza mwili kwanza kisha ndio roho hufuata...vikishafika vyote salama huungana tena na kuwa binadamu kamili na kuendelea na mambo yake