Trump awaambia wafuasi wa Republican ni yeye pekee anayeweza kushinda uchaguzi wa 2024

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
3a152d3d-8271-40b5-a6e0-840de533132e.jpg

ReutersCopyright: Reuters
Wawaniaji wa urais wa chama cha Republican wameshiriki jukwaa moja kwa mara ya kwanza katika kinyang'anyiro cha Ikulu ya Marekani 2024 kwenye hafla ya kampeni ya Iowa.

Wapinzani wakuu Donald Trump na Ron DeSantis waliongoza hafla ya wa kila mwaka ya chama cha Republican maarufu Lincoln Dinner.

Wagombea wote 13 walipewa dakika 10 za kuzungumza wakati wa hafla hiyo.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa Bw Trump anaongoza kwa wapinzani wake licha ya kukabiliwa na changamoto za kisheria.

Aliwaambia waliohudhuria kuwa yeye ndiye mgombea pekee ambaye anaweza kushinda uchaguzi wa mwaka ujao na kudai kuwa hiyo ndiyo sababu pekee ya yeye kukabiliwa na msururu wa mashtaka ya jinai.

Bw Trump tayari amesisitiza kuwa atawania Ikulu ya White House, hata kama atapatikana na hatia.

Kulikuwa na zaidi ya watu 1,200 katika katika hafla hiyo - wote wana ushawishi mkubwa juu ya nani atateuliwa kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani. chanzo.BBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom