Dokezo: Kifo Cha Utata

Stavros Myles

JF-Expert Member
Jun 7, 2020
350
390
Ni majira ya asubuhi maeneo ya maporini, binti mmoja mwenye asili ya watu wa Brazil anaonekana akiwa anatembea polepole.

Hali ya hewa ya upepo inamfanya binti huyu atumie mkono wake kuzirudisha nywele zake nyuma, sauti kubwa ya upepo inafanya masikio ya binti huyu yapitie hali ngumu mno.

Skirt ya huyu binti mara nyingi ilikuwa ikipandishwa juu na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi. Mara ghafla kiza kizito kinatanda juu ya anga hilo, hali hii ya ghafla inapelekea binti huyu aanze kukimbia kuelekea kwenye nyumba moja iliyokuwako porini hapo.

Mwendo wa kitambo kidogo unamsaidia kuufikia mlango wa nyumba ile ambayo hakuwa anajua inamilikiwa na nani, mwanga uliokuwa unatoka kwenye nyumba hiyo ndio uliomfanya aikimbilie. "hodi! hodi!" binti huyu alitoa sauti yake akiwa anatumia mkono wake wa kushoto kupigiza kwenye mbao za mlango huo.

Muda mrefu ulipita lakini hakutokea mtu yeyote aliuekuja kumfungulia mlango. Binti huyu aliamua kuufungua mlango na hapo alifanikiwa kuingia ndani ya nyumba ile. ndani ya sebule ile kulikuwa kimya mno, hakukuwa na dalili yoyote ya kwamba nyumba hiyo ilikuwa ina mtu anayeishi ndani yake. 'vuuuup' sauti hii nzito ilisikika baada ya ceiling board kuangusha karatasi zito la nailoni la rangi nyeusi.

Uzito wa kitu kilochokuwamo ndani ya karatasi lile la nailoni ilifanya kutokea kwa kishindo kizito mno, mavumbi na taka taka zilishuka kutoka kwenye ceiling board kwa pupa. Binti huyu alijikuta akifunika pua yake kwa mkono wake wa kulia na kurudi nyuma. Mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio mno kwa muda huo, bila hata kutambua binti huyu alijikuta akibamiza kichwa chake kwenye ukuta.

Mara ghafla kwa mbali binti huyu alifanikiwa kuona kivuli kilichoonekana kupitia mlango wa chumba fulani kilichokuwa na mlango ambao ulifunguliwa nusu, taa ya kandili ilifanya kivuli kile kionekane kikubwa mno katika kuta za chumba husika. 'Usiende' hii sauti ilisikika kichwani mwa binti huyu akiwa anajaribu kuinua mkono wake kusogea mbele ya kile chumba lakini aliona ingekuwa bora kama angepata msaada kutoka kwa mtu huyo ambaye alikuwa ndani ya chumba kile.

" Samahani kuna mtu humu ndani? " binti huyu aliuliza akiwa anasogeza miguu yake iliyokuwa imevishwa raba fupi, hakukuwa na sauti yoyote ile iliyojibu. Binti huyu alisogea tena na kufikia kitasa cha mlango ule akiwa na lengo la kuufungua ili apate njia ya kitorokea kama kungetokea jambo lolote la hatari.

Baada ya kusogeza uso wake ili kuchungulia humo ndani kulikuwa na nini mwanga wote ulitoweka kwa sekunde moja tu, sasa kiza kizito kilitanda ndani ya kile chumba. Sauti nzito ya kiumbe kilichokuwa kina hema ilisikika tena kwa utuo mno.

Mara ghafla kimya kikarejea lakini upande wa sebuleni kulisikika hatua za mtu aliyekuwa akitembea polepole. Kwa vishindo vya hatua zile ilikuwa ni kama sauti ya viatu vyenye visigino virefu vilikuwa vikitembea. Muda huu binti huyu alikuwa akitetemeka mno na hakuwa na mpango wa kurejea tena sebuleni. " binti karibu sebuleni, umeingia kwangu nataka tuongee kodogo" sauti nzito ya kizee ilisikika kutoka sebuleni. Binti huyu aliamua kurudi kwenye kile chumba ambacho hapo punde tu kilikumbwa na kiza kizito.

Baada ya kuingia ndani mwanga ulirudi tena lakini kwa muda huu mlango ulijifunga. Taa ya kandili iliyokuwa imewekwa juu ya meza ndogo iliyokuwa na rundo la vitabu iliendelea kutoa mwanga. "Njoo haraka nina mambo mengi yakufany" sauti ya kizee nzito iliongea kwa mara ya pili lakini muda huu haikupita hata sekunde kandili ilianguka na kumwaga mafuta, moto ulishika vitambaa vilivyokuwa katika hicho chumba na binti huyu alikuwa akipambana kutoka kwenye chumba hicho, baada ya jitihada za hali ya juu hatimaye binti huyu alisukuma dirisha na kujirusha.

Safari ya uhai wa binti huyu iliishia pale pale baada ya kuchomwa na Rake (Reki) iliyokuwa mahali hapo. Damu ilikuwa ikimtoka kwa wingi mno, sehemu ya kifua iliyochomwa na reki ile ilikuwa inapoteza uhai kwa kasi mno.

" Careen Careen, amka wewe" aliongea Mrs. Morgan akiwa anantingisha binti yake aliyekuwa amelala. Baada ya kutingishwa kwa muda mrefu Careen alikurupuka kutoka kitandani akiwa anatweta na kutoa pumzi fupi fupi za haraka mno.

"It 's another nightmare, what 's wrong with you Careen" (ni ndoto nyingine ya kutisha, shida yako ni nini Careen) aliongea Mrs.Morgan akiwa amemkumbatia binti yake huyo aliyekuwa anatokwa na machozi.

"But this time it 's not me, there was this girl...she was . I can 't explain but it was not me ...ahh. ah I swear mom ".......


DOKEZO TU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom