Dogo wa miaka 19 aliyefungua biashara ya 75M+

Dogo wa miaka 19 aliyefungua biashara ya 75M+

Hakuna cha pongezi wala nini hapo,naona mnajipa promo tu.

Kama zawadi tu alipewa ni altezza sasa unategemea nini kama sio kufanyiwa kila kitu na hao wazazi wake

Huyo hana tofauti na Trump aliposema "when I finished college I asked my dad for a loan and he borrow me $200,0000,000/- sasa wewe unategemea nini maana mtu hata awe kichaa vipi hawezi kutoifanyia jambo iyo pesa

Acheni unafiki wenu wa kujidai kupeana promo, there a lot of people out there who started their business from zero to hero
Duu ndonakisoma kitabu cha Trump basi nakiacha kumbe mahela yote ayo alipewa.
 
Ninachojuta ni kutokuwa na hii passion na mawazo haya nikiwa na umri kama wake.

Any way, I hope sijachelewa sana
 
Ninachojuta ni kutokuwa na hii passion na mawazo haya nikiwa na umri kama wake.

Any way, I hope sijachelewa sana

Wewe sasa ndio umeongea katika uzi mzima binafsi katika uwo umri nawaza kusomasoma tu sina chochote nawaza mawazo ya kibiashara na passion ya ujasiriamali na kuwaza mafanikio nimeipata mwaka jana ila sijachelewa.
 
Mm nampongeza tu kwani wangapi kwao wana pesa mingi ila akili zao zimelala kabisa hawajiongezi kutafta zao.
 
Ndo maana mimi nikasema nampongeza kwa kuwa na idea na uthubutu wa biashara..ila kwenye jinsi alivyopata mtaji No
Labda ulikua unahitaji apate mtaji kwa njia gan? Maana zipo njia nyingi za kupata mtaji nahisi na hiyo ni Moja wapo
 
Sasa madanga washamjua. Ma-Sweetheart wameshamfahamu. Akifanikiwa kuwakwepa na hao nitampongeza tena
 
Sikua na majukumu, nilikua na muda, ningekua risk taker, ningekimbia hapa na pale kutafuta fursa. Lakini jana imepita! The past is myself
Nimejifunza kupitia comment hii, hongera Mkuu..
 
Nilikuwa kwenye Youtube channel ya Millard Ayo nikakutana na stori ya kijana mmoja kwa jina Scott ambaye ni Mtanzania,aliyefungua biashara ya restaurant ya Pizza na ikanivutia kuangalia video hiyo..

Kwenye maelezo yake amesema alikuwa na lengo la kuwa na biashara yake kabla hajafikisha umri wa miaka 20+..

Alianza kusave fedha ambazo nyingine alikuwa akilipwa na mama yake alipokuwa anamsaidia katika kazi zake..

Pia aliuza gari aina ya Toyota Altezza aliyopewa zawadi na baba yake ili aongezee kwenye mtaji huku pia akiomba backup kutoka kwenye familia yake..

Katika maelezo yake nikagundua huyu kijana pongezi ninazoweza kumpa ni kuwa na idea ya biashara na kuishi katika ndoto zake and nothing else..maana inaonyesha familia yake iko vizuri,kwahiyo suala la mtaji sio big deal sana..



Wakuu katika jukwaa hili mnalipi la kuongea kuhusu kijana huyu na je biashara ni kweli inaanzia kwenye idea au both idea na mtaji vinaitajika ila kuanzisha biashara??

Biashara au kitu chochote ni ideas. Kupata mtaji ni sehemu ya utekelezaji wa ideaa. Mtaji ni sawa na uendeshaji wa biashara
 
Kasaidiwa na wazazi wake ...pongezi kwa wazazi.
Hebu na wewe usaidiwe na wazazi wako kwa uwezo walio nao tuone kama utasonga mbele. Hii kitu ni dogo mwenyewe ana hiyo akili na ndiyo maana ameweza kuendesha. Wengine hata pesa aliyokuwa akiweka baada ya kulipwa angetumia tu akijua wazazi wana pesa watampatia.
 
Kweli kabisa sio wazazi wote wana huo moyo
Wazazi wanasaidia mtoto anaejitambua. Huyu kijana kaonesha kujitambua mapema kwani hata pesa alizolipwa alitunza kwaajili ya mtaji wa biashara yake. Biblia husema ALIYENACHO HUONGEZEWA.

Sasa unalalamikia wazazi hata ukiulizwa inataka kufanya biashara gani hujui. Unapewa pesa ukachezee?

Tatizo vijana wengi hawajitambui wanasubiri wazazi wao wafariki ili warithi pesa za kutesa mtaani.
 
Huyu dogo majina yake kamili anaitwa nani? Accounts zake za mutandao ya kijamii ni zipi, tuendeko tukawe inspired huko
 
Back
Top Bottom