Mara nyingi huwa hatupendi kuukubali ukweli wa jambo, ama kwa kujua au kwa kutokujua.
binafsi ninaamini biashara ni wazo na sio mtaji. zamani nilikuwa siamini hivyo, niliamini biashara ni mtaji, na ilinichukua miaka mingi sana hadi nilipogundua kuwa kumbe ninaidanganya akili yangu.
kwanini nasema biashara ni wazo na sio mtaji. wengi tunaolalamika mitaji, tuna mitaji lakini hatujui tuna mitaji.
unawaza biashara ya mtaji wa milioni 5 wakati huna uwezo wa kuipata milioni 5 halafu unasema una wazo la biashara. Wazo ambalo huna uwezo wa kulitekeleza sio wazo, unaidanganya akili yako mwenyewe.
huna uwezo wa kupata milioni 5 lakini unao uwezo wa kupata laki 5 na hauwazi biashara ya laki 5 ili uanze nayo na baada ya muda au miaka kadhaa ufike kwenye huo mtaji wa milioni 5 kwa kudhani utachelewa. Basi endelea kulalamika hadi utakaposhushiwa huo mtaji.
Hii naizungumza kwa uzoefu wangu binafsi. Nimekaa miaka mingi nalilia mtaji, na mawazo ya biashara za mitaji mikubwa nikijifariji ndio inayolipa. Kwa miaka mingi sana, siku moja nikawaza, hivi mimi kama mtumishi mwenye mshahara wa kima cha chini, mbona ninao uwezo wa kukopa milioni 2 kupitia mshahara wangu kwa ajili ya biashara? Maana ninaishia kukopa kununua kiwanja, nikimaliza marejesho nakopa kununua Flat screen na mengine, kwa nini nisiwaze biashara nilito na uwezo na mtaji wake?
najua wengine mtalipuka, bora una pa kukopa kupitia mshahara, ni kweli lakini hoja yangu ni kuwaza biashara ya mtaji ulio na uwezo nayo hata kama ni laki moja ya kuuza simu uliyopewa na mjomba.
leo, hatuna la kujifunza kwa dogo kwa kuwa tunasikia 75ml, tunaiwaza hiyo 75 bila kumkubali kwa kuwa na wazo hilo.
yeye aliuza gari ya zawadi, usiye na gari umeshauza simu uliyopewa ili uwe mtaji hata kama ni ya elfu 50?
tunalalama hajaanzia chini. Kwa taarifa yako, inawezekana kwa uwezo wa familia yake, huenda hiyo 75 ndo ameanzia chini hapo, alitamani hata kuanza na 250. Maana kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
hata humu tunapolalama mitaji, tukiulizana hapa, mwingine atasema ningepata 20ml, mwingind ningepata 5ml, mwingine ningepata 500k, mwingine 150k, n.k
tusiangalie 75m, tuangalie uthubutu kwa kila mmoja kwa uwezo wake katika mazingira aliyomo na kubadili mtizamo kwa kuanza na tulichonacho.
binafsi nampongeza dogo kwa wazo la biashara kwa kuanza na saving kwa alichokuwa nacho bila kujali kiasi cha mtaji.