Kuna kaka yangu mtoto wa mjomba alikuwa kibaka kama huyo unayemsifia mtaani walichoka siku yake moja akaingia kwenye 18 za wajeda walimchakaza vibaya sana, wakaenda kumtupa karibu na kwao kufika asubuhi alifariki, mtu anayeiba siyo wa kumchekea kabisa maana mwisho wake ni kifo tena kifo cha mateso na fedheha kama unampenda huyo dogo smart mwambie aachane na hizo ishu afanye kazi.