Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati Area C Mtaa wa Makongoro.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.

#NiYeye2020

Updates leo tarehe 8/8 Jumamosi

Tayari mgombea wa Urais Tundu Lissu amewasili katika ofisi ya Chama Kanda ya Kati na amesaini kitabu Cha wageni na kupata ukaribisho na maelezo mafupi kutoka viongozi wa Kanda.

Kwa Sasa msafara wa kuelekea Tume ya uchaguzi umeanza ukiongozwa na pikipiki nyingi, magari makubwa ya mabasi na madogo huku wananchi wengi wakiwa kandokando ya Barabara waliounga mikono

Live Millard Ayo na UTV ya Azam

Saa 5 kamili Jumamosi

Mgombea wa Urais Tundu Lissu ndiyo anaingia hapa Time ya Taifa ya Uchaguzi akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama wafuasi na wananchi.

Chadema imetii masharti ya Tume ya Uchaguzi kwamba wafuasi na mashabiki wabaki nje na ndani wameingia viongozi wachache kumsindikiza Lissu.Viongozi waliomsindikiza Lissu ndani kwenye ukumbi ni Godbless Lema,Peter Msigwa,John Heche,Suzane Kiwanga na Baraka Mwago wote wakiwa Wajumbe wa Kamati Kuu.

Hamasa ni kubwa Sana na hapa ukumbini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi yupo na meza yake Kuu wakisubiri kuingia mgombea Urais na Mwenza wake

Saa 5.20

Lissu akiwa na mgombea Mwenza wake wameingia kwenye ukumbi na Mkurugenzi wa uchaguzi ndiyo anatoa maelekezo kwa wagombea

Mheshimiwa Lissu anasikiliza kwa umakini mkubwa na kwa utulivu maelekezo ya Mkurugenzi wa Tume.

Sasa Mkurugenzi amemaliza kuongea na amemkaribisha Mwenyekiti Jaji Kaijage kukabidhi fomu kwa wagombea.Mwenyekiti anatoa maelezo mafupi ya nyongeza

Saa 5.27

Rasmi Sasa Tundu Lissu anakabidhiwa fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano baada ya kukamilisha mambo yote muhimu.Mgombea Urais na Mgombea Mwenza wanapokea kwa Pamoja huku makofi yakipigwa.

Saa 5.32
Shughuli zimekamilika rasmi hapa ndani ya ofisi ya Tume na kuagana rasmi Kati ya viongozi wa Tume na Chadema.

Umati mkubwa Sana wa wafuasi wa Chadema unasubiri nje ya ofisi ya Tume huku watu wengi wakiwa wanafuraha kubwa isiyoelezeka

Kinachoendelea baada ya Kutoka Ofisi za Tume:

Kwa Sasa ni maandamano makubwa yakiongozwa na pikipiki nyingi, magari yasiyo na idadi huku mgombea wa Urais Tundu Lissu akiwa katika gari ya wazi akipungia watu waliojipanga kando kando ya Barabara.

Gari ya Mgombea Tundu Lissu imezingirwa na maafisa wa Usalama wa Chama maarufu Kama Red Brigade ambapo idadi ya walinzi wa gari lake waliozunguka hawapungui 12 kwa Idadi
 
Tunashukuru Molemo kwa kuleta hii habari. Kuna uzito fulani kwenye kitengo cha habari cha cdm, kiasi kwamba kuna uzi humu jukwaani unaohimiza kitengo cha habari kuamka. Kuna ushauri pia kuhusu Tundu Lisu jinsi ya kufanya siasa zake bila kupoteza credibility yake. Ni vyema kama chama mkakaa na Lisu na kumfunda. Kuna baadhi ya maneno anaongea yanampotezea haiba yake.
 
Akumbuke tu huo ndo mji ulioweka historia ya uhai wake,ikibidi atembelee eneo la tukio kutoa sadaka na aende hospitaliya mkoa kuwashukuru madaktari na manesi...zaidi ya yote awe MAKINI

Ushauri mzuri, ila akienda hapo hospitalini huenda akaambiwa anaenda kufanya siasa. Hilo la umakini ni muhimu, na sio kwa Dodoma tu, bali popote awapo.
 
hapo kila mtu anadai yeye ni wa Wanyonge na kweli mnawanyonga, yaani sisi waafrika tukijinasibu umasikini na unyonge kwetu sijui ni au kutaka huruma? lakini hii yote tumezoeshwa kusaidiwa na kufadhiliwa nilimsikia spika wakati wa kufunga bunge akitoa aibu zake alivyokuwa akiishi kiufukara na maisha ya dhiki
 
Tunashukuru Molemo kwa kuleta hii habari. Kuna uzito fulani kwenye kitengo cha habari cha cdm, kiasi kwamba kuna uzi humu jukwaani unaohimiza kitengo cha habari kuamka. Kuna ushauri pia kuhusu Tundu Lisu jinsi ya kufanya siasa zake bila kupoteza credibility yake. Ni vyema kama chama mkakaa na Lisu na kumfunda. Kuna baadhi ya maneno anaongea yanampotezea haiba yake.
Tutazingatia
 
Back
Top Bottom