Dodoma: Serikali yasitisha mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa kati unaopita kata ya Nkuhungu

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Serikali ya awamu ya tano ya Hayati Magufuli sote twajua iliasisi miradi mingi ktk maeneo mbalimbali ya nchi, mfano bwawa la Mwl. Nyerere, Reli ya Mwendokasi (SGR), barabara za njia nane,ringroads na miradi mingine mingi.

Miradi hii kiukweli ilileta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya miji na vijiji,na kuleta mvuto wa miji maeneo ambayo miradi hiyo ilipita.

Baada ya kifo cha Hayati Magufuli, aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, kuna mijadara mingi mitaani kuhusu kuendelezwa kwa hii miradi.katika pitapita nikakutana na hili la kusitishwa kwa ujenzi wa ringroad ya kati ya jiji la Dodoma, ambayo ilipitia maeneo ya mtaa wa Nkuhungu.

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma amesitisha ujenzi wa ringroad hiyo, na kuwaruhusu wananchi waendelee na shughuli zao za ujenzi kama kawaida. Mradi huu wa ujenzi wa middle ringroad hii, ni baadhi ya miradi ambayo iliasisiwa kipindi Cha Hayati Magufuli enzi za uhai wake,ktk kulifanya jiji la Dodoma kuwa na muonekano mzuri na uliopangika vizuri.

Kwasasa mitaani watu wanajadili je! hii miradi iliyoasisiwa na Hayati Magufuli itakamilika kweli!? au ndo hivyo tena itabaki kuwa hadithi isiyokuwa na mwisho!

Japo kuna siku nilimsikia Waziri Mkuu akiwatoa wasiwasi watanzania kwa kusema , "watu waondoe mashaka miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Serikali ya awamu ya tano, yote itakamilishwa kwa muda uleule uliokuwa umekadiliwa awali, enzi za uhai wa Hayati Magufuli".

Je, ilikuwa ni kuwatuliza watu pressure za mashaka au! Kama hii miradi midogo imeanza kusitishwa mdogomdogo, je hii mingine ya mabilioni ya pesa itakuwaje!? Anyway ngoja tuone mambo yatakuwaje.

Ila wananchi tumeyatunza maneno ya Waziri Mkuu kwenye kumbukumbu zetu, alitutia moyo na kutuondoa mashaka kwamba miradi yote iliyoasisiwa na Serikali ya awamu ya tano itakamilika.

Waziri Mkuu, tunakumbuka maneno yako, ipo siku tutataka utupe maelezo, ilikuwaje?

FB_IMG_1623130023151.jpg

 
Serikali ya awamu ya tano ya Hayati Magufuli twajua iliasisi miradi mingi ktk maeneo mbalimbali ya nchi,mfano bwawa la mwal. Nyerere,reli ya mwendo Kasi (SGR) ,barabara za njia nane,ringroads na miradi mingine mingi.

Miradi hii kiukweli ilileta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya miji na vijiji,na kuleta mvuto wa miji maeneo ambayo miradi hiyo ilipita.

Baada ya kifo Cha Hayati Magufuli, aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kuna mijadara mingi mitaani kuhusu kuendelezwa kwa hii miradi,katika pitapita nikakutana na hili la kusitishwa kwa ujenzi wa ringroad ya kati ya jiji la Dodoma ambayo ilipotia maeneo ya mtaa wa Nkuhungu

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma amesitisha ujenzi wa ringroad hiyo na kuwaruhusu wananchi waendelee na shughuli zao za ujenzi kama kawaida, hii ni baadhi ya miradi ambayo iliasisiwa kipindi Cha Hayati Magufuli enzi za uhai wake ktk kulifanya jiji la Dodoma kuwa na muonekano mzuri na uliopangika vizuri.

Kwasasa mitaani watu wanajasili je hii miradi iliyoasisiwa na Hayati Magufuli itakamiika kweli!? au ndo hivyo tena itabaki hadithi ilisiyokuwa na mwisho!

Japo kuna siku nilimsikia Waziri Mkuu aliwatoa wasiwasi watanzania kwa kusema , watu waondoe mashaka miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Serikali ya tano yote itakamilishwa kwa muda uleule uliokuwa umekadiliwa awali enzi za uhai wa Hayati Magufuli.

Je, ilikuwa ni kuwatuliza watu pressure za mashaka au ! Kama hii miradi midogo imeanza kusitishwa mdogomdogo je hii mingine ya mabilioni ya pesa itakuwaje? Anyway ngoja tuone mambo yatakuwaje, ila wananchi tukeyatunza maneno ya Waziri Mkuu kwenye kumbukumbu zetu, alitutia moyo na kutuondoa mashaka kwamba miradi yote iliyoasisiwa na Serikali ya awamu ya tano itakamilika.

Waziri Mkuu tunakumbuka maneno yako,ipo siku tutataka utupe maelezo ,ilikuwaje?

View attachment 1812069
Hapa hautawaona kina missile of the toilet..babati..robert herielii..wao huwa wanakuja kwenye mada za kuwasuta kina sabaya na makondaa..
Mzee alishasema..mtanikumbukaaa..tartiiibuuu tunaelekea hukoo..
 
KUNA WATU WANAFIKI SANA HUMU,HAKUNA JINSI TUTAISHI NAO HIVYO HIVYO.
=======================================
TUKUBALIANE IPO MIRADI AMBAYO ILIANZISHWA KATIKA MWENDO WA KICK TU.
->Daraja la salender (lile la baharini)
Kila nikilitathimini sioni umuhimu wake,
-->pamoja na maintachenji foleni ipo palepale,
#miradi ya kick...!
#population ya dodoma Ahihitaji ring roads,wakajifunze #zimbabwe.
#Dar es salaam lihitaji ring road,ianzie kurasini ipite pembeni ya mji itokeze hata ikibidi chalinze waende ZAO mbali....!
 
Back
Top Bottom