Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,542
- 2,171
Wanafunzi 1,000 wanufaika na msaada wa vifaa vya shule vyenye thamani ya tsh. milioni 32 kutoka kwa Mariam Ditopile Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM mkoani Dodoma.
Mbunge viti Maalum Mkoa wa Dodoma anayetokana na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ditopile amewawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu vifaa vya shule kwa wanafuzi 1000 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 30.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wilaya zote saba za Dodoma Ditopile amesema ikiwa ni kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha amewaomba wadau mbalimbali mkoani humo na nchini kutoa kipaumbele zaidi katika Sekta ya Elimu kwa kutoa misaada hasa wa watoto yatima na wenye mazingira magumu yatakayosababisha kukatisha masomo na kupoteza ndoto zao za elimu.