Dodoma: Makarani wasusia sensa wakidai kutolipwa fedha zao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Waongozaji 90 wa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamesusia zoezi la Sensa ya watu na makazi linaloendelea kote Nchini kwa madai ya kutolipwa fedha zao.

Waongozaji hao wa Makarani wamedai kuwa waliahidiwa kulipwa laki moja kwa awamu mbili lakini hadi kufikia Agosti 28, 2022 hawakuwa wamelipwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wa Chemba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Samson Chacha alikutana na waongozaji hao wa makarani hao na kuahidi kuwa watalipwa kama walivyokuwa wamepangiwa.

Source: Azam TV
 
Sensa ya mwaka huu imefeli vibaya. Ni sensa ya hovyo kuwahi kutokea na ukiangalia saikolojia mama wa sensa amepaniki kawa mkali hovyo. Serikali iitishe sensa upya na dodoso lifupishwe ifanyike kwa siku 1 tu kwa mafanikio
Wapi ilipofeli mkuu..
Upo dar sehemu gani?
 
Mgomo wao hauna impact yoyote
Umejiunga Jf 2009 lakini umecomment kama mtoto aliitoka Fb na kujiunga Jf 2022.

Mgomo unaimpact kubwa katika maisha na sehemu nyingi imekua chachu ya mafanikio ,hata mwanafunzi akimgomea Mzazi haebdi shule bila madaftari au viatu vipya baada ya kupewa kalenda nyingi hapo lazima mzazi atajipinda hata kwa kukopa ili mtoto awahi shule maana ataogopa kesi na kujitafakari kweli mtoto hapa limemgusa maana kavumilia sana.
 
Hivi kwa nini Rais hatoi matamko katika mambo muhimu yanayogusa wananchi moja kwa moja kama hili zoezi la sensa ambalo limekuwa na dosari na malalamiko mengi toka kuanza kwa mchakato?

Au amewaachia wenyewe watatazame huku wananchi wakipata maumivu na kuridhia kulalamika?
 
Una miaka 13 jf na hiki ndio unaongea😳😳😳
Sawa, lakini huwa tunaangalia zaidi hoja kuliko personal issues za mtoa hoja. Turudi kwenye hoja. Hivi unadhani bila waongozaji, karani hawezi kuzifikia kaya?
 
Ilitakiwa wachukue chao mapema ndipo waanze Kazi huwa awajifunzi kupitia Yale ya kusimamia uchaguzi
 
Back
Top Bottom