Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
Huko makao makuu ya nchi jijini Dodoma kulianzishwa mji wa Magufuli uliotangazwa na waziri wa tamisemi wa wakati huo Seleman Jafo ili kuenzi juhudi za rais Magufuli kwa kuahidi na kukamilisha ahadi ya kuhamishia serikali yote Dodoma ndani ya miaka 5 ya utawala wake.
Sasa mji huo umefikia asilimia 90 ya ujenzi wake na huduma zote muhimu kama barabara,maji na umeme zimeshafika. Bila shaka kukamilika kwa mji huo itakuwa mateso makubwa kwa wasiompenda hayati Magufuli kwani sasa watalazimika kupandia mabasi stendi ya Magufuli, au SGR ya Magufuli au ndege za Magufuli hapa kazi tu na kwenda Magufuli City Dodoma.