Dodoma: Kesi ya Kupinga Uchaguzi wa TLS yatupiliwa Mbali kwa mara ya Pili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
Heshima kwenu wakuu,

Wakili Godfrey Elia John Sabato Wasonga, amewasilisha Maombi Mapya Mahakama kuu ya Dodoma jana jioni akipinga Uchaguzi wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) unaotegemea kufanyika kesho.

Maombi hayo yanaweza kusajiliwa rasmi leo asubuhi hii kwenye Ofisi ya Msajili wa mahakama na Kupewa namba.

Taarifa zaidi zinakuja.

Mahakama kuu ya Dodoma hapo jana iliruhusu Uchaguzi kuendelea baada ya Mapingamizi yaliyowekwa awali kutupiliwa Mbali na Mahakama.

Stay tuned.

=====

UPDATES; 1830hrs:

Kesi namba 15 ya 2017 iliyokuwa imefunguliwa leo mjini Dodoma, na wakili Godfrey Wasonga imetupiliwa mbali na Jaji Kalongora wa mahakama kuu kanda ya Dodoma. Kesi hii ni ya pili kwa wakili Wasonga kutupiliwa mbali baada ya nyingine kutupwa jana.
 
Mawakili waliofika tayari Arusha atawarudishia gharama za kusafiri na malazi? Mawakili zaidi ya 6000 ndio wanatarajiwa kupiga kura!

Pingamizi lake likipita basi na mawakili waliopo Arusha wamshitaki Wasonga,kama Wakurugenzi na watumishi wengine wa serikali waliamriwa kurudisha nauli na masurufu ya kwenda kwenye kilele cha mbio za Mwenge,kwa nini mawakili wasidai fidia kutoka kwa mtu anayesumbua taasisi yao na kutia hasara rasilimali zao?!

Jana kashindwa,mahakama ikaamuru alipe gharama,leo amekuja tena,huu ni upotevu wa raslimali,CCM waone aibu basi!!
 
Huyu ana tick the box na yuko strong mana nyuma yake na ninaamini anafanya si kwa matakwa yake bali ambao hawapendi kuongoza kwa mujibu wa sheria. Kama sheria zinafuatwa kwa nini mtu kumwogopa Tundu Lissu. Mambo mengine ni utoto kabisa
 
Heshima kwenu wakuu,

Wakili Godfrey Elia John Sabato Wasonga, amewasilisha Maombi Mapya Mahakama kuu ya Dodoma jana jioni akipinga Uchaguzi wa TLS unaotegemea kufanyika kesho.

Maombi hayo yanaweza kusajiliwa rasmi leo asubuhi hii kwenye Ofisi ya Msajili wa mahakama na Kupewa namba.

Taarifa zaidi zinakuja.



Mahakama kuu ya Dodoma hapo jana iliruhusu Uchaguzi kuendelea baada ya Mapingamizi yaliyowekwa awali kutupiliwa Mbali na Mahakama.

Stay tuned.


Ukisifia utawala huu wa kuwafanya malaika kuwa mashetani unachuma laana kwa Mungu
 
Back
Top Bottom