Dodoma: Kambi ya Upinzani yanyang'anywa Watumishi, Wagoma kuandaa Hotuba, Katibu wa Bunge anawahujumu

Wapinzani wa Tanzania wamekua kama kondoo vichwa chini baada wapambane kwasababu vyama vya kisiasa vipo kikatiba wanaogopa kufa Tatizo Mboe angekua kama Lissu au Lema ndo angalau wana roho Ngumu lakini mwenyewekiti Mboe muoga sana
Wewe ndio muoga zaidi. Unaongea "kishujaa" huku umejificha kwenye handaki. Duh.
 
Watawala wameshikwa pabaya sana. Badaya ya kuhangaika na vi-wonder, wao wanahangaika na uhochezi, mitandao, maandamano, media, nk. Soon miaka mitano inakatika
 
Hawa jamaa wamechuja sana kwa ujinga wa viongozi wao,matamko kila kukicha utekelezaji sifuri,hapo utakuta wanataka kujitutumua tena wakati jamaa wiki nzima walikua wametulizwa ngomeni na hali ni shwari ,bado akili yao haijajityuni kwamba hii si awamu ya nne ,ni awamu ya tano
Roho mbaya kama ya kiongozi wa malaika
 
Ni pale mwenyekit wangu wa CCM anaposimama majukwaani na kutuambia maendeleo hayana chama, tunamuelewa sana ktk hili kwa maana huu ni wajibu na ndivyo yapasa kuwa...tena kwa ujasiri kabisa husema kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wote na yuko kuwatumikia wananchi wote bila kujali itakadi, dini wala ukanda, vizuri sana na pongezi kwa kauli hizi. Huenda mbali zaidi na kuahidi kuilinda na kuitetea katiba na sheria za nchi hii, well said.

Sasa ktk uhalisia, kuna nyakati Mwenyekiti wangu mpendwa mara chache amejisahau na kutamka kuwa atawashughulikia wapinzani, sawa hapa naamini ilikuwa utani na hakuwa serious. Mshangao na butwaa kwangi inakuja pale wateule wake bila kificho wamekuwa mwiba na watesi wa upinzani hata kudiriki kutoa kauli za "kiuhasama dhidi ya wapinzani" rejea kauli za Mh. Mnyeti, Makonda na wengineo....pia matendo ya watendaji wa tume ya uchaguzi ya taifa, wakurugenzi, wakuu wa vyombo vya usalama, na hivi sasa bunge letu. Je, hawa wanafanya kwa utashi wao wenyewe? Mh. Rais hayaoni? Kama anayaona na kupiga kimya, je wateule wake wanampuuza?

Je, ikiwa tatizo ni kukosa rasimali (watu na pesa) kwa upande wa upinzani au wakati mwingine pesa za maendeleo kupelekwa sehemu zisizokuwa na upinzani tu.....je hizi kodi zinakusanywa toka kwa wanachama wa chama changu pendwa cha CCM tu? Kama kodi inatoka mifuko kwa watazania wote iweje tuirudishe kwa ubaguzi? Au ndio tunahubiri umoja wakati sisi ni waasisi wa mipasuko na mifarakano!!!

CCM OYEEE
 
Ghazwat Hii ni dharau kubwa sana kwa watanzania. Kwa nini mda wakuandaa press kila wiki unapatiakana na wakati mwingine press za CDM huandaliwa kila siku na kuwasilishwa kwa waandishi!

Je sisi watanzania tujiulize watu wa kuandaa press za CDM kila wiki wapo na mda upo lakin wa kuaanda Hotuba KUB Bungeni hakuna. Kitu gani hiki watanzania?
 
Mboe amejitahidi sana kutumia akili yake vizuri kuwahadaa wabunge wenzake make kama angesema wasusie vikao vya bunge naamin pangechimbika kwenye kikao nani angekubali kirahisi kususia bunge na aache hizo posho za miezi mitatu. Pasingetosha akaona awazuge kwa kisingizio cha wafanyakazi wa kuandaa hotuba hana. Tokea December kweli siamini wangekuwa walishairusha kitambo kwa Mange kama msemaji wao na yeye angekuwa alishaituma na tungekuwa tulishajua zamani sana siyo Leo ndo utuletee hizo ngonjera mpya. Mkiendelea hivyo ata mange atawakimbia
 
Hawa jamaa wasipo badili namna ya kufanya siasa wataumbuka utawala huu sio ule

Wabadili mbinu kwa kuwa wamebadili mbinu watawala matamko,maandanamo na kauli tata zitawapeleka kubaya
Wanafiki mtaongea mengi sana lkn mjue haki haiombwi ila inadaiwa mmekalia eti wasipo badili mbinu kwa hiyo mlitaka wamlambe miguu mungu wenu asiesikia hata maaskofu.
 
Wanataka kusema nini?

Watu waliostaaribika sasa hivi wanafanya kazi halali na kwa bidii na kuimarisha miundombinu muhimu ya Nchi.

Hawa wahuni kutwa kuleta zogo tu hapa nchini.
Kichekesho waliostaarabika ndio Hawa wanaokataa hata ushari wa maaskofu na mapadre aibuu
 
Huyu Mugabe wa Chadema kanyoa ndevu? Masuala ya Bunge wamalizane huko huko Bungeni. Wanataka watumishi lukuki wakati Bungeni kwenyewe hawakai walipwe mishahara bila kufanya kazi na sasa wanaandaa mkakati wa kususia Bunge la Bajeti
Wasusie tu, wanaonewa mno na hao oppressors.
 
Hawa jamaa wamechuja sana kwa ujinga wa viongozi wao,matamko kila kukicha utekelezaji sifuri,hapo utakuta wanataka kujitutumua tena wakati jamaa wiki nzima walikua wametulizwa ngomeni na hali ni shwari ,bado akili yao haijajityuni kwamba hii si awamu ya nne ,ni awamu ya tano
Ni bora watoaji matamko kuliko wanafiki wanaodanganya watu na kujidai na kuropoka kila siku hakuna linalobadilika ila upuuzi tu waroho na washamba wa madaraka
 
Hawa jamaa wasipo badili namna ya kufanya siasa wataumbuka utawala huu sio ule

Wabadili mbinu kwa kuwa wamebadili mbinu watawala matamko,maandanamo na kauli tata zitawapeleka kubaya
Nchi inaongozwa na washamba, tusitegemee maendeleo!
 
Huyu Mugabe wa Chadema kanyoa ndevu? Masuala ya Bunge wamalizane huko huko Bungeni. Wanataka watumishi lukuki wakati Bungeni kwenyewe hawakai walipwe mishahara bila kufanya kazi na sasa wanaandaa mkakati wa kususia Bunge la Bajeti
Na huyo Nkurunzina wa Tanzania kanyoa vuziii za kwapa
 
Mkuu Hekima Kwanza,

Haya matatizo ni makubwa kweli, pamoja na ukubwa wake, tunahitaji kufahamu undani wake;
1. Kulikuwa na wafanyakazi wangapi hapo kabla?
2. Waliajiriwa na kulipwa na nani?
3. Mikataba yao ilikuwa ya muda gani?
4. Kwa nini mikataba ilisitishwa?
5. Utaratibu wa kuwepo kwa hao wafanyakazi ulianza lini na kazi zao zilikuwa zipi?

Yawezekana ni maboresho tu ya utendaji wa kazi za kiofisi ya bunge ili kuongeza ufanisi.
Hata hivyo, kuna uwezekano wa kuwepo watendaji wa uma wenye tafsiri potofu za kanuni na sheria ili kutimiza kiu zao za kutenda uovu kinyume na malengo ya utawala kwa ujumla.

Na kuongezea labda pia tufahamu:

1. Hao wafanyakazi wa ofisi ya KUB ni nani anawaajiri ? Je, ni ofisi ya bunge ama KUB ?

2. Kama ni bunge lenyewe ndilo linalowajiri kwa vyovyote iwe kwa mikataba ya muda maalumu ama kudumu, je hawakujua kuwa muda wa mikataba yao umekwisha na wanastahili kuongezewa ama kuajiriwa wengine ili ofisi ya KUB iendelee kutekeleza kazi/majukumu yake kwa mujibu wa kanuni za bunge, sheria na katiba?

3. Kama ni ofisi yenyewe ya KUB ndiyo yenye wajibu wa kuajiri, kulipa na kuwapangia majukumu/kazi wafanyakazi hao, basi ofisi ya KUB yenyewe ndiyo inayopaswa kulaumiwa (japo hii hoja mimi binafsi siiamini kwa sbb ofisi ya KUB ni sehemu ya Bunge na katibu wa bunge anawajibika kuihudumia moja kwa moja)

4. Lakini pia tujiulize na tupate majibu toka KUB, kwamba, je ni lazima hotuba zote mbadala za wizara za kisekta ziandaliwe kupitia ofisi hii moja kwa moja ? Hakuwezi kuwa na njia mbadala ya kuziandaa hotuba hizo bila kuitumia ofisi hiyo ?

5. Na je, kuna faida ama hasara gani iwapo hakutakuwa na hotuba za kambi ya upinzani bungeni ? Nataka kuelewa kwa sbb KUB kasema hawatakuwa na hotuba mbadala za kambi rasmi ya upinzani baada ya kufanyiwa hivi....

LAKINI TUKUMBUKE KUWA:

1. Moja ya mkakati wa hovyo na kijinga kabisa chini ya uongozi wa Bwana John Pombe Magufuli ni kuzuia ukosoaji wa serikali yake kwa njia zozote zile.

Lengo lake ni kinyume chake. Asike yeye tu, aonekane yeye tu. Aaminiwe yeye tu. Bila kujali ni uongo ama ukweli usemwao ama kusikika kutoka kwake ama serikali yake.....

Hii ni kuwa, haijalishi ni nje uraiani, bungeni, vyombo vya habari, social medias ama njia zozote zingine za mawasiliano......

This is a primitive strategy of a stone age kutoka kwa washamba tuliowakabidhi mamlaka na madaraka ambayo kiukweli yamewalevya chakariiiii !!

Sasa swali la kujiuliza ni hili.

Je, hili la ofisi ya KUB kunyimwa uwezo wa kufanya kazi yake kwa mujibu wa kanuni za Bunge, sheria na Katiba kwa wafanyakazi wake kuondolewa ni moja ya mikakati ya kuhakikisha hakuna maoni mbadala bungeni ambayo mara nyingi huonesha mapungufu na makosa ya utendaji wa serikali ??

Kwangu mimi nadhani huu ni mwendelezo wa mikakati hii ovu kabisa.

USHAURI KWA KUB:

Nadhani it doesn't matters whether maoni yenu yatapokelewa ama yatawasilishwa kwa kusomwa bungeni. It's meaningless na haina maana yoyote kwa sasa na kwa viongozi hawa wa kizazi cha zama za mawe....

Kwa sbb aidha yapokelewe ama myasome bungeni, lakini kwa vyovyote vile yataingilia kwenye masikio ya kushoto ya watawala na kutokea ktk masikio yao ya kulia kwa sbb wao wanaamini maendeleo ya nchi hii watayaleta wao tu bila msaada wa wengine.... Wamelewa madaraka hawa, achaneni nao. Mwisho wao hauko mbali tena wa aibu tu. Mungu anawaona sana......

Ni kwa mantiki hii, hamna haja ya kubembelezana nao. Kwa sbb mnapowakosoa, kimantiki mnawasaidia wao ili warekebishe na kisha watende kwa uzuri zaidi.....

Lakini kwa kuwa akili na ufahamu wao umefungwa kwa mapipa, hawawezi kuliona hili. Wao wanadhani kuwa, watanzania na ulimwengu kwa ujumla utapokea na kulishwa kila aina ya matango pori (uongo) kutoka kwao na kumeza tu.

Wanajidanganya kwa sbb nyakati hizo hazipo. Tuko kwenye nyakati za kuhoji kila jambo, kila kitu. Huwezi kutoa maelezo watu wafuate tu kama ming'ombe.

No way. Sisi ni binadamu tunaofikiri, wenye akili na ufahamu pengine kuliko hata wao viongozi. Wasidhani kwa kuwa wao ni viongozi basi wana akili na ufahamu kuzidi mamilioni ya watanzania wanaowaongoza. Kama wanafikiri hivi, basi ni wajinga na wapumbavu kwa kiwango cha juu sana ...!!

Mwisho, nyie ni wabunge na viongozi wa vyama vilivyo nje ya serikali (vya upinzani), mmechaguliwa na wananchi pia.

Kama mna jambo lolote liwe la kupongeza serikali, kukosoa, kuelekeza ama kuishauri serikali pelekeni kwa wananchi wenu kwa kutumia njia yoyote ya mawasiliano. Wao ndiyo watoa hukumu kwa watawala na kwenu pia.

Acheni kulia lia mbele ya "watawala hawa waovu" ambao kwa namna yoyote ile wameshajitangaza kuwa ni maadui wa wananchi wote wanaowaunga mkono. Asiwadanganye mtu kuwa hampendwi na umma. Mimi nawahakikishia zaidi ya 85% ya umma upo upande wenu....!!!

Pigeni kazi, kuweni wabunifu ktk kufanya siasa zenu bila hofu wala woga wowote. Tumieni njia mbadala kuwasilisha hoja zenu kwa wananchi, zitapokelewa na kupimwa na kulinganishwa na za watawala......umma wenyewe utaamua.

Kumbukeni watawala wana mtandao mpana sana wa hujuma dhidi ya kila hoja yenu. Msishangae kila hoja yenu kugeuzwa upside down. Ya kweli kupakwa rangi ya uongo, uchochezi, kumtukana Magufuli wao nk nk

Hawa wana bunduki na kila aina ya silaha, wana polisi, usalama wa taifa (TISS), jeshi la wananchi, magereza, jeshi la "wasiojulikana" na zaidi sana wana PESA kodi zetu....

Lakini haya yote historia inaonesha hayajawahi kuishinda nguvu ya umma kutoka kwa watawala wajinga, wapuuzi, wauaji na hatari kabisa kuliko huyu Magufuli na CCM yake !!!
 
Back
Top Bottom