Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameitisha mkutano na waandishi wa habari muda huu mjini Dodoma. Taarifa zaidi ya mkutano huo kukujia.
========
Moja kwa moja kutoka mjini Dodoma
Freeman Mbowe: Bunge lina watumishi zaidi ya 400 lakini kambi ya upinzani inao 4 tu, huu ni mkakati wa makusudi kuhakikisha kambi rasmi inakufa
Freeman Mbowe: Leo hatukuwasilisha hotuba ya Kiongozi wa Upinzani kwa sababu ya Bunge kusitisha utaratibu wa Kambi kuwa na ofisi na wafanyakazi
Freeman Mbowe: Kambi Rasmi ya Upinzani imeeleza kwa nini leo haikuwasilisha hotuba ya Kiongozi wa Upinzani Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa sababu ya Bunge kusitisha utaratibu wa Kambi kuwa na ofisi na wafanyakazi
Freeman Mbowe: Watumishi wa upinzani walifukuzwa na Katibu wa Bunge Januari kutokana na mikataba kumalizika Disemba
Freeman Mbowe: Kanuni ya 16 (4) ya Bunge ndiyo iliyozaa Kanuni za kambi ya Upinzani, inaruhusu kambi kutunga kanuni zake
Freeman Mbowe: Nilipomfuata Katibu wa Bunge kumuuliza kulikoni unawafukuza hawa watumishi kama mbwa, akanijibu anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni. Ajira zao watumishi msubiri Spika. Hadi leo kambi haina hata mtumishi mmoja. Hatuna hata mtaalamu mmoja wa kuandaa hotuba na kuchambua nayaraka
Freeman Mbowe: Alitegemea mimi niandae hotuba Segerea ambako hakuna sekretariet
Freeman Mbowe: Watumishi wa CCM hapa bungeni wapo na hawajafukuzwa kama wa kwetu
Freeman Mbowe: Sasa kwa hali hii tunapata wapi taarifa ya kuwasilisha bungeni?
Freeman Mbowe: Mikakati ya Katibu wa Bunge ni kuua upinzani. ndiyo jukumu alilokuja nalo
Freeman Mbowe: Baada ya kuona kuna tatizo kwa Katiba. Nilimwambia Spika anipatie kibali cha kuajiri lakini kanipa cha ajira 3. Hivi kweli watumishi watatu wasimamie wizara zote
Freeman Mbowe: Tangu Januari nimenyimwa hata Dereva.Tangu Januari sijatumia gari hilo la KUB na hawanipi stahiki zangu ambazo zipo kisheria
Freeman Mbowe: TAMKO: Hatutakuwa na hotuba za upinzani katika Bunge hili la Bajeti hadi pale watakaporuhusu kuajiri. PILI: Hatutakubali hotuba zetu kuhaririwa. TATU: Katibu wa Bunge afahamu upinzani ni watumishi wa watu na wameletwa hapa na watu
Freeman Mbowe: Spika aelewe Katibu wa Bunge ni tatizo.Amekuja kwa mkakati wa kutudhibiti
Freeman Mbowe: Hakuna mpango wa Kambi Rasmi kususia Bunge.... Tumeshindwa kuingia wote bungeni asubuhi kwa sababu wengi wetu tulikuwa Dar es Salaam kwa shughuli nyingine
Freeman Mbowe: Hotuba hazipo mpaka watakapokubali kufuata kanuni za Bunge