Documentary ya umasikini mkoani Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Documentary ya umasikini mkoani Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngonini, Oct 9, 2011.

 1. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wakuu ninaangalia kipindi Star TV kinachoonyesha maisha ya watu wa vijijini huko dodoma. Inaumiza sana maana watu wamekata tamaa na maisha maana ardhi imechoka na uzalishaji ni mdogo sana.

  Watoto wanaenda shule nusu mwaka wakati kukiwa na chakula tu kikiisha wanaanza kwenda porini kuhemea. shule ndo zinategemewa kuwapa watoto chakula, kikiisha hata shule hawaendi mpka kikija tena ndo wanarejea. Inamaana watoto wanaenda shule kwa sababu ya chakula tu.
  Wanawake wanasota maana waume zao wanawakimbia.
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Star TV wanaonesha wimbo wa Ali Kiba, Dushelele. Jamani hata kama mmeruhusiwa kupost mnachojisikia lakini muwe mnajitahidi kudanganya kwa kutumia kichwa.
   
 3. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haitakusaidia kufanya propaganda za kijinga kama hizi. Wataanzania ndiyo wanaoumia na tayari wapo watu wa kuwasemea sasa hivi si kama ilivyokuwa zamani kwamba mateso yao mliweza kuyaficha kwa propaganda kama hizi.

  Kumbu maumivu ya hawa watu Mungu anayasikia na kamwe hatayasahau na ole wako unayefurahia leo maana ipo siku utashiriki uchungu huU.

  Mungu turehemu!
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hicho kijiji kipo ndani ya wilaya gani?. Ili tuweze kumtambua mbunge wake.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ngonini... Dodoma ni mkoa wenye matatizo makubwa sana
  kwanza watu wake wana uvivu fulani,,,, ukweli mtupu
  pili wana hali mbaya ya ardhi
  tatu ni watu wasiojua au wasiopenda mabadiliko

  what you see in dodoma, is typical ya mikoa yote ambayo CCM wamewachota

  usishangae, ni mpaka watakapoamka then ndio utaona hali inakua tofauti
   
 6. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii documentary nadhani imechukua maendeo mengi tu ya mkoa wa dodoma, pia walionyesha na mkoa wa manyara kidogo sasa hivi wako wilaya ya kilwa.
   
 7. M

  Mzelokotwa Member

  #7
  Oct 9, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Uko sahihi kwa kiasi kikubwa ktk mchango wako, lkn natofautiana na wewe kwenye uvivu ambalo wengi wasiofahamu mazingira ya dodoma wamekuwa wakiamini hivyo, wakazi wa Dodoma kama ilivyo sehemu nyingi za Tz na afrika kwa ujumla wanategemea kilimo cha jembe la mkono kilimo ambacho hakina uhakika wa kupata mavuno, msimu wa mvua kwa mkoa huu ni mfupi sana miezi 2-3 kwa mwaka wakati mwingine chini ya hapo, utakuta mkulima anaamka saa 11 alfajiri na kurudi saa 12 jioni lkn anachokipata ni chini ya gunia moja kwa ekari. kwamsingi huo mkulima huyu masikini hawezi kujitoa katika umasikini alionao bila kuwezeshwa. Kilimo pekee kinacho weza kuinua maisha
  wakazi wa Dodoma ni kilimo cha zabibu, hatahivyo kilimo hiki kinahitaji mtaji mkubwa sana kiasi ambacho wengi hawamudu. hivyo uwezeshaji kutoka serikalini au taasisi za kifedha(maarifa/fedha) unahitajika sana.
   
 8. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Mkuu Ngonini huo ndo mtaji wa CCM....na kauli mbiu yao TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE...wamewafanya wananchi vijijini washindwe kuelewa haki zao
   
 9. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wananchi wale sio wavivu tatizo ni ardhi na hali ya hewa kwamba mvua hazitabiliki na hazitoshelezi. Serikali ya CCM inakwepa jukumu lake la kuwaongezea tija (labour productivity) wananchi wale hivyo inabuni uongo na kuwasingizia kuwa ni wavivu. Kukosa chakula kunaisaidia CCM kwani wakati wa uchaguzi wana peleka chakula cha msaada ili kununua kura zao. Wabunge waliojichokea kama Livingstone Lusinde badala ya kujenga hoja bungeni za kuwasaidia wananchi wale wao watatumia dakika 15 kumpongeza Jakaya kwa kuchaguliwa kwa kishindo na kuwasifia wake na mahawara zao.
   
 10. MALI YA BABA

  MALI YA BABA JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Dodoma wanasubiri huruma ya Mungu2 wengi wao ni wavivu ndomana kuna ombamba wengi sana!! mungu awasaidie2
   
 11. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Matatizo ya mkoa huo ni mengi, lakini cha ajabu hata usipo uliza utawaona tu, wapo wengi kama si kilemba cha ccm basi t shirt
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  P
  Asante mkuu kwa ufafanuzi, ndio maana wahenga wanasema ishi kwingi uone mengi, hii ndio hali halisi ya mkoa wa dodoma. hawajajikomboa kifikira na ndio maana
   
 13. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dodoma kukame saana ila nature ya watu wake si wa kupenda saaana kazi.Anyways polen sana Watu wa Dom na endeleeni kuichagua CCM ili Maisha yenu yawe zaidi ya apo
   
 14. m

  mteule Member

  #14
  Oct 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah kweli umaskini ni fikra za mtu tu, sasa kama hao watu wa dom, miaka nenda rudi, maisha ni duni sana na bado mbunge wanaendelea kumchagua kwa tiketi ile ile.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu ahsante kwa taarifa, ila ingekuwa bora zaidi kuchagiza thread kwa kurekodi kipindi, una-upload youtube na kubandika hapa watu wajadili kwa kuona. Mimi nilipoona thread nikajua nakuja angalia documentary hiyo.
   
 16. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Haya maswala ya Dodoma, Igunga na kwingineko, mkoloni aliyaishajua. Alitamka wazi kuwa Nyie wananchi wa Tanganyika bado sana kuomba uhuru, hivyo vuteni subira muwekewe misingi mizuri ya maendeleo kwanza ndipo mdai uhuru. Hata mangi mareale naye alisappoti hiyo hoja ya Edward Turnbul. Sasa tuling'ang'ania kupata uhuru wetu. Ona sasa miaka 50 baada ya uhuru bado watu wnakula mlo mmoja kwa siku! Shule za msingi nyingi ni za nyasi na walimu hamna!

  Utaona baada ya kupata uhuru tuu, tulianza kusaidia wakimbizi, kuanzisha mgambo,kuukana utajiri,kutukana mabepari, kueneza nyimbo za chama toka ngazi za mikoa mpaka vijijini na kucheza kwata! Umasikini unaoonyeshwa Dodoma unasikitisha sana na kuonesha wazi wazi kwa jinsi gani sera za ujamaa na kujitegemea zilivyowapotosha watanzania.

  Hao sio wakulima bali ni waganga njaa. Halafu watu kama hao wa dodoma, walipokuwa wameshindwa na maisha ya kijijini na kuja mijini kutafuta kazi, walikuwa wnakamatwa na kuwekwa keko miezi sita na kurudishwa huko huko kwenye shida! Jamani mungu mkubwa kuuuwa ukomunisti na kutawanya nguvu za siasa za ujamaa.

  Sasa kama tukija tambua kuwa 90% ya maisha ya watanzania walio wengi vijijini yapo sawa na ya watu wa huko dodoma, Igunga na mtwara, hilo zigo la lawama atwishe nani? Hivi hii siasa ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa inatupeleka wapi jamani? Kwa nini tusiamini kuwa kufa kwa ukomunisti duniani ni lengo la mungu kuwaokoa wananchi wa Tanzania ambao walikumbatia siasa ambayo ilikuwa inawalea vibaya?

  Kama kuna mtu atanibishi, basi aseme kwanza kwa nini siasa ya ujamaa na kipindi cha Ujumbe wa leo havipo? Star TV endelea kuonesha ukweli wa maisha ya mtanzania huko vijijini.
   
 17. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nilivyoona mimi mkoa wa dodoma kule vijijini utaendelea kuteketea maana kuna jamaa mmoja aliongea kwa uchungu sana, akasema 'yaani maisha haya unafanyakazi mwaka mzima na hupati kitu mwishowe unakufa tu hakuna kitu ulichokifanya'

  Hili lilinionyesha kwamba wapo watu ambao wanatumia nguvu nyingi kutaka kujiokoa na hii hali lakini mambo yamewakaba na hamna msaada kutoka kwingine.

  Ilisikitisha zaidi vitoto vya darasa kama la nne na tanao hivi vilipoonyeshwa viko nyumbani na mama yake akasema hawaendi shule maana sasa hvi sisi hatuna chakula na shuleni chakula kimeisha tunasubiria kiletwa wataenda tu shule. Yaani watoto wanaenda shule kwa ajili ya chakula tu na si kusoma!

  Iliniumiza sana ninapo ona serikali iko biz na sherehe za miaka 50 wakipoteza fedha nyingi kwa kucheza ngoma na kugawana posho kila wizara na idara huku hali ikiwa hivi huko vijijni? Tunasherehekea nini?

  Tanzania ya miaka 50 ambayo asilimia kubwa ya wananchi mpaka sasa hawana na uwezo hata wa kula chakula kila siku?
   
 18. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  ukame ni tatizo dodoma hata elimu na ufahamu haupo kabisa.Kama mageuzi yatotokea chi nzima basi msiihesabu Dodoma kule wanafikiri wao waliandikiwa umaskini .
   
 19. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  acheni dodoma na igunga wapigike na maisha, labda itawasaidia kujifunza magamba ni hatari kwa afya na maendeleo yao na wakiambiwa kwenda kuchagua viongozi watachukua za kwao waongeze na za mbayuwayu..then fyaaaa
   
Loading...