Doctor of honoris causa of Sokoine university of Agriculture

mokala1989

JF-Expert Member
May 4, 2013
2,236
728
Aliyewahi kuwa makamu mkuu wa kwanza wa chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA), chuo kikuu cha Dar es salaam, chuo kikuu huria cha Tanzania na Provost wa chuo kikuu cha Tumaini tawi la Dar es salaam Professor Geofrey Mmary amekuwa mtanzania wa pili baada ya raisi wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere mwaka 1997 kutunukiwa shahada ya juu ya heshima ya udaktari ya chuo kikuu cha sokoine (Doctor of honoris causa of Sokoine university of Agriculture) katika mahafali ya 29 yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Nelson Mandela Freedom Square Kampasi ya Mazimbu. Kitaaluma alikuwa MATHEMATICIAN .Hakika kuna watu waliofanya makubwa katika taifa hili, tunalo deni kubwa sisi vijana la kufanya kudumisha waliyoyajengea msingi HONGERA PROFESSOR MMARI.
 
Back
Top Bottom