Polisi anayeua jambazi bila hata kulifikisha mahakamani, ambalo ni kosa la jinai, (ambayo hiyo si rushwa) anasimamiwaje na TAKUKURU?
Takururu ni chombo kilichoundwa kwa lengo la kuthibiti Rushwa na kupambana na wala Rushwa, sasa badala ya kukupambana na wala rushwa ambao ni watumishi ktk vyombo mbalimbali kama TRA, POLISI, nakadhalika zake zote, imekua inapamba rushwa na kuwasafisha wala rushwa na mbaya zaidi wao ndio wala rushwa wenyewe.
Kwa hiyo TAKURURU haijatimiza lengo au kusudi la kuanzishwa kwake, na kama haijatimiza lengo na imekwenda kinyume na kazi iliyotakiwa kufanya, basi na Ifutwe.
Kesi ya polisi kuuwa jambazi ni tofauti kidogo na kesi ya TAKURURU. Kwanza jambazi ni muuaji na anapokuja kukuvamia pale ni ama zako, ama zake, manaka amejiandaa kukumaliza kwa namna yoyote ili mradi apate kile kilichomleta.
Kwa namna ingine naweza kusema jambazi ni adui kama maadui wengine, ni mwanadamu ambaye utu wake umeondoka anaishi kama mnyama mkali anayewinda wanadamu wenzake.
Na kama umevamiwa na jambazi, kama yeye hajakuuwa labda wewe umuue au Mkono wa Mungu ukunusuru katika makucha ya jambazi huyo/hao.
Na polisi nae anapopambana na jambazi ni ama za polisi au za jambazi, ni vita hiyo kati ya polisi na jambazi sasa polisi atamkamata vipi mtu mwenye silaha na uwezo wa kukatisha maisha yake?
Jamani usiombe kuvamiwa na jambazi, wapo watu waliopoteza wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwa unyama wa jambazi, ndio maana nasema jambazi ni adui wa mwanadamu aliyebebwa katika boksi lenye umbo kama mwili wa mwanadamu.
Na Mungu ameturuhusu kupigana ma maadui zetu, tena anasema yeye ni Mungu wa adui zetu na yeye pia ni bwana wa majeshi.
Kwa nguvu zake polisi akimkuta jambazi anavamia akifanikiwa kumuua na amuue tu kwani kinyume na hapo ni yeye anauawa.
Mi naona hata lisiitwe kosa la jinai, lakini polisi akikamatwa anapokea rushwa na akamatwe na akipokea rushwa ili kumtetea jambazi na akamatwe.