BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,115
Posted Date: 10/16/2007
Wapinzani waeleza sababu za kuikataa Takukuru
Kizitto Noya na Salim Said
Mwananchi
UMOJA wa Vyama vya CUF, TLP, Chadema na NCCR Mageuzi, vimeueleza sababu za kutotaka tuhuma za ufisadi kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwa ni kuokana na kushindwa kwake kutoa ripoti inayoridhisha katika mikataba Richmond na Dowans iliyoikabili serikali.
Katika tamko la vyama hivyo lililotolewa jana jijini Dar es Salaam, umoja huo umesema kuwa hautofanya makosa kukubali taasisi hiyo kuchunguza tuhuma nzito za ufisadi wa viongozi wa serikali kwa kuwa wanaamini kuwa haitatenda haki.
Akisoma tamko hilo katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Chama cha Tanzania Labour (TLP), Mwenyekiti wa chama hicho, Augostine Mrema, alisema kuwa kitendo cha taasisi hiyo kuisafisha serikali na kashfa ya mikataba hiyo ya Richmond ni doa kwake lisiloweza kusahaulika kirahisi na mwanaharakati yeyote.
Ikiwa Kampuni ya Richmond ambayo serikali ilifanya usimamizi wa kawaida kuhakikisha tatizo la umeme lililoikumba nchi yetu wakati huo linapatiwa ufumbuzi haikuzalisha umeme, Kwa nini serikali haikuwajibika kwa kusimamia mikataba iliyozaa matunda?� alihoji Mrema.
Alisema umoja wa upinzani hauna imani na Takukuru katika kushughulikia wala rushwa na mafisadi ambao ni viongozi wavyeo vya juu serikalini kwa kuwa haiwezi kutenda haki.
Alisema ingawa taasisi hiyo iliisafisha serikali dhidi ya rushwa katika mikataba ya Richmond na Dowans, taarifa za hivi karibuni kutoka Mamlaka ya Kusimamia Manunuzi nchini (PPRA) zinasema kuwa kulikuwa na mkono wa rushwa iliyofanywa na vigogo wa seriakali katika kutoa zabuni na kuidhinisha mikataba hiyo.
Mrema alidai kuwa serikali ilijua kuwa takukuru itailinda katika uchunguzi wake na ndiyo maana iliamua kupinga hoja ya wabunge waliotaka kujadili suala hilo bungeni na kulipeleka kwenye taasisi hiyo.
Wabunge kadhaa walitaka kujadili suala la kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond Development Corporation (sasa Dowans) bungeni ili kujua endapo ulitawaliwa na rushwa lakini serikail iligoma na kuamua kulipeleka suala hilo Takukuru.
Hata hivyo wabunge hao hawakuweza kutimiza azma yao hiyo baada ya kushindwa kutimiza kanuni ya 45 ya Bunge ya kuwasilisha hoja binafsi inayotaka mbunge kutoa hoja hiyo kimaandishi siku mbili za kazi kabla ya mkutano husika wa Bunge.
Richmond iliingia mkataba na Tanesco wa kuzalisha megawati 100 za umeme kwa kutumia gesi asilia, lakini ilikuwa ikikumbwa na matatizo katika utekelezaji wa mkataba huo hadi ilipouzwa kwa kampuni ya Dowans. Mradi huo uligharimu dola za Marekani 172,500,000 (sawa na Sh225 bilioni).
Katika kuchunguzi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) iliisafisha Kampuni ya Richmod Development Company dhidi ya tuhuma za rushwa zilizokuwa zikiikabili katika uingiaji wa mkataba wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa TANESCO.
Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea, alisema baada ya uchunguzi wa taasisi hiyo kuwa hakuna ushahidi wowote uliopatikana kuthibitisha rushwa au upokeaji wa kamisheni kwa watendaji wa serikali.
Alisema uchunguzi wa Takukuru umebaini kuwa Richmond Development Company, LCC ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited inayomilikiwa na Naeem Gire mwenye uraia wa Tanzania na Mohamed Gire raia wa Marekani, ilifanikiwa kushinda zabuni iliyotangazwa na TANESCO baada ya kuyashinda makampuni mengine manane yaliyojitokeza.