Abdull Bawazir
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 209
- 162
Nimeingia kwenye mgahawa mmoja kupata chakula cha usiku ni miongoni mwa ile migahawa yenye vioo vya kufugia samaki wa marembo (Aquarium) sasa nikiwa nasubiria chakula nikawa natupa macho huku na kule kilichonipendeza zaidi machoni mwangu wakati huo ulikua hyo aquarium hasa gold fish na utundu wake wa kuonyesha rangi yake ya dhahabu kimadaha akijibinua anapofika chini, pia kutokua na cha kufanya mda huo vilinisukuma niendelee kuwaangalia tu wanavyokwenda kushoto na kulia lakin ghafla likapita swali kwenye akili yangu, Do Fish See Water? Ilinichukua kama dk 3 hvi kupata majibu na nilicheka mwenyewe na kuona ipo haja kuona watu wengine wanafikiria nn?? What Do You Think? Unadhani Samaki Wanaona Maji?