tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,847
- 18,253
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Huko nchini Uganda kimeuma sawasawa. Ndivyo unavyoweza kusema. Mashirika mbalimbali ya habari yakiwemo BBC na DW yameripoti kwamba kasi ya upimaji wa DNA kwa wanandoa wa kiume umepamba moto kwa siku za hivi karibuni na kwamba 56% ya vipimo vimebainisha kwamba watoto waliopimwa sio watoto wa kibaiolojia kwa akina baba wanaowalea.
Jambo hili limekuja baada ya wanaume wa Uganda kushtukia wake zao kuzaa nje ya ndoa na kuwabambika watoto. Wanaharakati wa ndoa na haki za watoto wanalaani upimaji huu na wanatoa wito kwa serikali kusitisha zoezi hili haramu mara moja. Madai yao makubwa ni kuwa wanaopata shida baada ya vipimo ni watoto. Hivyo, wanaomba zoezi hilo lisitishwe haraka iwezekanavyo ili kuokoa ndoa na kuleta utengamano wa kifamilia na kijamii.
Kwa jinsi hali ilivyo, kuna uwezekano wanaume kutoka Tanganyika nao wakaiga mtindo huu wa kupima DNA kwa wingi. Je, huu upimaji ukihamia nchini Tanganyika kutakuwa na usalama? Na, je wewe mwanaume unakubali kulea mtoto wa nje ya ndoa kwa kisingizio kwamba ukipima DNA ndoa itavunjika?
MAONI YANGU
Pamoja na kwamba uchepukaji kwa akina mama na kuzaa nje ya ndoa na kisha kuwachomekea waume zao watoto sio jambo zuri, mimi naona akina mama wanajaribu kubalance mzani kwa kuwa akina baba nao wamekuwa wakitoka nje ya ndoa na wakizaa watoto huwaleta kwenye familia na kukubaliwa na mwanamke bila shurti. Sasa kwanini ndoa ivunjike pale mama anapozaa nje ya ndoa lakini baba akizaa nje ya ndoa huleta mtoto na kuasiliwa na mke wake bila tatizo lolote?
Nawasilisha.