Anaandika: Dr. Wilbrod Slaa
Msingi wa vitendo vyote vya utekaji unaoendelea nchini ni Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa (TIS) ya mwaka 2024. Bila kurekebisha sheria hii, Watanzania wataendelea kutekwa, kupotezwa na kudhulumiwa hadi tutoweke kabisa kama taifa huru.
Sheria hiyo imeipa TIS mamlaka makubwa ya kukamata watu, lakini bila kuweka utaratibu bayana wa:
(a) Wanapomkamata mtu, wampeleke wapi? Tofauti na Jeshi la Polisi lenye vituo maalumu vya kushikilia watuhumiwa, TIS haina vituo vinavyotambuliwa kisheria vya kuwapokea waliokamatwa.
(b) Hakuna mwongozo wa kisheria unaoeleza nini kifanyike baada ya mtu kukamatwa na TIS. Kwa mfano, Polisi wanapaswa kuhakikisha kuwa ndani ya saa 4 baada ya kumkamata mtu, maelezo (statement) ya mtuhumiwa yanakuwa yamechukuliwa, huku haki za mtuhumiwa zikiwa zimeainishwa wazi katika Sheria na katika taratibu za Police General Orders (PGO). Kwa upande wa TIS, sheria yao haina mwongozo wowote kuhusu haki za waliokamatwa wala hatua zinazofuata baada ya kukamatwa.
(c) Sheria ya TIS imeiruhusu Idara kutumia silaha nzito, pingu na vifaa vingine vya kiusalama, lakini tofauti na Polisi, hakuna mahali sheria inapotamka wazi kuhusu vifaa hivyo vinahifadhiwa wapi, vinatumiwa kwa utaratibu gani, na ni nani anawajibika kuvihifadhi.
Hayo ni baadhi tu ya mapungufu makubwa ya sheria hiyo. Kwa ujumla, sheria hii imeifanya TIS kuwa taasisi isiyoguswa, isiyodhibitiwa na isiyoajibika kwa namna yoyote kwa umma au kwa vyombo vingine vya dola.
Kwa hiyo, kama raia — hususan wasomi — tumeshiriki kimya kimya kuzalisha mazingira haya ya kinyume na utawala wa sheria kwa kukubali kupitishwa kwa sheria hii mbovu bila kupiga kelele. Sasa tunavuna tulichopanda.
My take: TLS Mwabukusi hamuwezi kuipinga hii sheria mahakamani kama Olengurumwa alivyopinga sheria ya kutoshitaki akina Rais na wenzake?