MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Kila nikijaribu kukumbuka na kutafakari zaidi kuhusu kauli za huyu Mama alizozitoa mbele ya Rais wa JMT kuwa mihimili yote haiko sawa, kwamba mhimili wa dola ni mkubwa zaidi kuliko miingine. Hii kauli binafsi naichukulia kua ni ya kujikosha na kujipendekeza, si kauli ya kutamka kwenye media mbele ya macho ya umma.
Spika wa aina ya Dkt Tulia hata kama kuna jambo linalohatarisha ustawi wa taifa ikatokea likafanywa na serikali ataangalia tu wala hatofanya uamuzi wowote kwa vile dola ndio mhimili mkuu? Maana Dola siyo Mungu wala malaika kwamba haikosi.
Tunatambua kua kwa katiba yetu hii iliyopo dola ndiyo kila kitu lakini usiifanye mihimili miingine kutokujiamulia mambo yake ya uhuru, lakini kila mhimili una mipaka ya majukumu yake huru bila kuingiliwa na mwingine. Huyu alimaamisha kwamba Ndungai alikosea kwa kauli zake? Alikuwa anamaanisha kua mhimili wa bunge si lolote wala chochote?
Tukiwa na bunge chini Spika aina ya Dkt Tulia ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na kwa maslahi vya taifa. Niwashauri wanaccm wenzangu, hata kama kuna wakati tunatakiwa kulinda maslahi vya chama lakini Dkt Tulia hafai kabisa . Huyu mwanamama anataka kulitia bunge Kibogoyo liwe kama mihuri wa gogongea kupitisha hoja za serikali hata kama hazifai.
Hawa ndio wasomi wetu, wapo radhi kupotosha ili kulinda maslahi yao binafsi.Haijalishi wewe ni CCM au upinzani, tafadhali kemea watu wa aina hii kwa maslahi ya taifa letu. Tuachane na watu aina ya Tulia hawatufai.