Dkt. Kalemani achangia Bungeni kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 8, Spika amuongezea muda

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,049
49,733
Yule Waziri wa Zamani wa Nishati aliyetumbuliwa na Rais Samia Bwn. Kalemani amechangia Kwa mara ya kwanza Bungeni baada ya miaka 8..

Hongera bwana Kalemani wa Chato Kwa kushinda Kinyongo 🤪🤪

=======

Kalemani.PNG

Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani leo amechangia bungeni kwa mara ya kwanza akiwa kama mbunge ukiwa ni mwaka wa nane ndani ya mhimili huo wa dola.

Akichangia Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alimpa muda wa zaidi kutoa mchango wake kwa sababu ni mara yake ya kwanza kuchangia bungeni kama mbunge.

Kalemani aliingia bungeni mwaka 2015 ambapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 2017 alipoteuliwa kuwa Waziri wa wizara hiyo.

Alishika nafasi hiyo hadi Septemba 2021, ilipochukuliwa na January Makamba.

Chanzo: TBC
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom