Dkt. Slaa ashauriwe

Tangu astaafu ubalozi na kurudi nchini Dr Slaa amekuwa akitoa kauli zenye utata ambazo mwishoni humrudia yeye mwenyewe.

1. Kwanza, Dr Slaa aliwaataka wafuasi na wanachama wa wachadema wakae kimya na kuacha kudai kuwa Mbowe sio gaidi na hana hatia. Nadhani akilini mwa Dr Slaa alijua lazima Mbowe atatiwa hatiani. Cha kushangaza DPP anafuta mashtaka yote kwa Mh Mbowe na Wenzake.

Aibu ikamwangukia Dr Slaa kwa kudandia kesi asiyoijua imetokea wapi.

2. Pili, Juzi Dr Slaa kasema Ripoti ya CAG imepotoshwa, kwa maana ikishafikishwa mbele ya bunge haitakiwi kuwa public document. Kumbe sheria ilifanyiwa marekebishi na Sasa Report ya CAG ikiwekwa mbele ya bunge inakuwa ni Mali ya Umma. Hivyo jamii inaruhusiwa kuijadili.

Aibu ikamwangukia Dr Slaa kaishia kuomba radhi kuwa amekosea na alipitiwa alidhani sheria ya mwaka 2009 bado inatumika.

3. Jambo la tatu Dr Slaa amedai kwamba Kuna uwezekano ya kwamba CHADEMA ndio wanahusika na kumlima risasi Lissu na akatumia issue ya huko nyuma kutetea hoja yake bila kujua ukweli wa Jambo. Juzi wamelumbana na heche kwenye club house na kuishia kusema amenukuliwa vibaya hakumaanisha hivyo.kwa bahati nzuri CHADEMA bado wanheshimu mzee, wangeweza kumfungulia kesi ya ya madai.

Hivyo walio karibu na Dr Slaa wamshauri ya kwamba alidai amestaafu siasa basi aendelee kustaafu, maana Ni Kama amerudi kwenye siasa.

Pia ajifunze kutoka kwa akina Musiba waliotoa kauli wasizo kuwa na uhakika nazo leo zimewafunga wamejificha hata Uhuru wa kuongea hawana.
Hoja ya kwanza kwamba aliwataka wanachama wa Chadema wakae kimya kusema wakae kimya ni kweli maana Issue iliyopo Mahakama kiutaratibu hatupaswi kuitolea majibu mpaka mahakama itoe hukumu ili Dkt hakukosea ila ndo utaratibu wa ulivyo Duniani.

Dkt Slaa wala hakuwazia kama Mbowe angefungwa na wala hakuweka percent kuwa DPP asingeweza kufuta kesi ila tukiweka maneno mengi pembeni DPP kafuta sio kwa maamuzi yake ila kwa Kauli kutoka kwa Mh Rais, kwa bahati mbaya ili hatulioni kama tatizo la Muhimili wa Serikali kuingilia mihimili mingine kwasababu ili limetugusa sisi. Ila kitendo cha Mahakama kusema Mbowe kakutwa na kesi ya kujibu alafu DPP siku ya pili anakuja hana nia ya kuendelea na kesi ilikuwa udhaifu mkubwa wa mihimili yetu!

Angalau wangeiwahi pale Mahakama iseme kuwa hawajamkuta Mbowe na kesi ya kujibu ikaishia hapo! Lakini kwakuwa ili linatufurahisha sisi acha lipite, tumefunika kombe mwanaharamu apite.


Kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi ilo ata Tundu Lissu aliwahi kusema kama ata Mbowe alihusika vyombo vya usalama vikibaini vimkamate tu! Tukio la Lissu tumeliweka kisiasa kwakuwa tu mwenyewe ni mwanasiasa nayeye akalibeba kisiasa lakini tu shambulio la Lissu usije kusema Chadema hawahusiki! Ila si Chama ila kuna viongozi ndani ya chama chenu wanalijua vema na ndiyo walilipanga shambulio lile na ndiyo maana Lissu anashindwa kurudi sababu tena sio Magufuli ila mwenyewe anajua hajui kwasasa rafiki yake ni nani wala adui yake ni nani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr. Slaa uuchukue huu ushauri. Usiamini kwamba anaweza kuiharibu CHADEMA kwa maneno yako machafu.

Mwenzako Magufuli alitumia maneno, polisi, TiSS, Mahakama, TRA ili kuiua CHADEMA alishindwa, sembuse Dr Slaa ambaye huna chochote, zaida ya mdomo.
Mchawi sana huyo mzee.
 
Dr. Slaa uuchukue huu ushauri. Usiamini kwamba anaweza kuiharibu CHADEMA kwa maneno yako machafu.

Mwenzako Magufuli alitumia maneno, polisi, TiSS, Mahakama, TRA ili kuiua CHADEMA alishindwa, sembuse Dr Slaa ambaye huna chochote, zaida ya mdomo.
Chadema Sasahivi ina mbunge mmoja,tena nae ni mwananke 🤣🤣🤣harafu mnasema haijafa,labda Chadema ya jamii forums
 
Dr. Slaa uuchukue huu ushauri. Usiamini kwamba anaweza kuiharibu CHADEMA kwa maneno yako machafu.

Mwenzako Magufuli alitumia maneno, polisi, TiSS, Mahakama, TRA ili kuiua CHADEMA alishindwa, sembuse Dr Slaa ambaye huna chochote, zaida ya mdomo.
Mwendazake alikiapiza kuifuta CDM matokeo yake kafutika yeye CDM ni kama ya juzi jana leo na mwakani..
Kama vipi ajiajiri tu.
Hakuandaliwa / hakujiandaa kujiajiri na ndiyo maana sasa hivi anafanya kazi ya unyoka ili aishi
 
Kimsingi sikuwahi kuandika Jambo lolote baya juu ya mzee huyu toka amehamia ccm kwa kuwa nilihisi bado anayo heshima yake ktk mageuzi ya siasa za nchi hii hususani ktk demokrasia ya Vyama vingi na upinzani kwa ujumla.
Lakini siku za hivi karibu huyu Mzee amekuwa akieleza Mambo kadhaa ambayo huwezi amini kuwa yanatapikwa na yeye mwenyewe.

Kwa mwenye Akili anaweza kujua kuna tofauti kubwa sana ya Dr. Slaa ambaye alikuwa Chadema akishindia Mihogo huku akiibua hoja fikirishi Bungeni na nje ya Bunge na huyu Dr.Slaa aliye hamia ccm na kuzawadiwa ubalozi na sasa anatuletea vioja.

Nami nitajikita ktk hoja mbali mbali alizo zungumza ili tuweze kumpima Kama huyu Dr.Slaa ni yule yule au Watanzania tumepigwa tena kuletewa Dr. Slaa feki kutoka huko Canada.

Kwanza Dr. Slaa anasema Ripoti ya CAG haitakiwi kuwa wazi kwa jamii na CAG hapaswi kudadavua hiyo Ripoti kiundani.Kwa kuwa watuhumiwa wanaweza kuwa wanaonewa kwa kuwa hawaja hojiwa na kujieleza.

Hivi kwa Akili za kawaida tuu CAG toka lini amekuwa mahakama? Vipo vyombo vingine vingi vya uchunguzi kubaini ukweli wa Ripoti ya CAG kwa nini huyu Mzee hataki raia tujue matumizi ya pesa zetu?

Pili huyu Slaa alikuwa kinara wa kutoa taarifa za ufisadi Bungeni na nje ya Bunge akiwa Chadema mpka kutangaza orodha ya Mafisadi papa( List of Shame) pale Mwembe Yanga na ikafikia mpaka watu wasio julikana kumuwekea vinasa sauti ktk chumba chake ili kujua anatoa wapi taarifa. Hakujua hao watuhumiwa alio kuwa akiwalipua walikuwa wanaonewa na walihitaji kwanza kusikilizwa?

Anapata wapi kiranga Cha utetezi wa Serikali ili hali Rais huwa anamuagiza CAG kuweka Mambo hadharani bila kumung'unya maneno?

Ukiwa na jicho pevu utaona pia Slaa anamponda Rais Samia kiaina kwa kuruhusu Ripoti ya CAG kuwa hadharani huku ikionesha ufisadi mkubwa wakati Magufuli alikuwa Madarakani kwa kuwa alimpa ulaji wa tumbo lake.

Amesema kupigwa Risasi Tundu Antipas Lissu hawezi kueleza kwa kuwa akiwa Katibu Chadema kulitokea tukio la kiongozi mmoja wa Chadema kutekwa na mmoja wa viongozi wa ulinzi wa Chama alimueleza kuwa ni yeye ndie alaye mteka.

Kwa maelezo yake kwa wenye Akili tunajua anasema kuwa sio Serikali tuu mtuhumiwa huenda Chadema pia wamehusika.

Tukisema tukubaliane na hoja yake Kuna maswali magumu yanaibuka. Iweje Katibu wa Chadema ambaye ndiye kiongozi wa shughuli zote za Chama asijue operesheni za Chama chake mpka aje aambiwe na mlinzi?

Huyu mlinzi mtekaji na muuaji ni kwa nini amueleze Siri hiyo Slaa ?Je ni kwa kuwa alikuwa anamuamini atatatunza Siri na kuwa wamewahi kushirikiana kufanya matendo mengine ya kiharifu? Ni miaka mingapi imepita mpka leo,kwa nini Slaa hakuyasema hayo akiwa Chadema? Ina maana hata Sasa huko CCM Slaa anashuhudia uovu mwingi hasemi anasubiri siku akihamia TLP aje atwambie Watanzania kuwa CCM ndio walio muwekea Mangula sumu? Je tumwamini huyu Mzee? Ni kwa nini hakuripoti tukio hilo ktk vyombo vya usalama?

Slaa ameshindwa kutuambia ktk eneo ambalo viongozi wa Serikali wanaishi lenye geti na ulinzi ni kwa namna gani Chadema wanaweza kuingia na kuwaondoa Walinzi wenye siraha na kuingia ndani na kumpiga Risasi Tundu Lissu na kufanikiwa kuondoka na Serikali isifanye juhudi zozote kuwatafuta ikakubali kuwa watumiwa.

Lakini ameshindwa kutueleza ni kwa nini Serikali haikuweza kutumia vifaa vya ulinzi Kama Camera zilizo kuwepo au kuomba msaada toka nchi zenye teknolojia nzuri kubaini ni nani wahusika mpka Leo hii.

Pia amezungumzia kuhusu KATIBA mpya akasema kwa maoni yake KATIBA mpya sio kipaumbele Cha wananchi. Nikawa najiuliza huyu Dr. Slaa wakati akiwa mgombea Urais kupitia Chadema aliinadi ilani ya Chadema amabayo ilikuwa na agenda ya KATIBA mpya na alituahidi Watanzania akiingia lkulu ndani ya siku 100 Tanzania tutakuwa na KATIBA mpya.

Lakini pia hata baada ya Uchaguzi kuisha na Matokeo kutangazwa kuwa Kikwete ameshinda uchaguzi huyu Mzee aliyapinga Matokeo kwa kudai kuwa sio halali.Huyu Slaa ndio mwanzilishi wa neno kuchakachua, alilitumia wakati ule akidai kuwa Tume ya Uchaguzi ilitangaza Matokeo feki yaliyo pikwa.

Iweje leo Dr Slaa awe na Imani na KATIBA hii mbovu na Tume hii ya Uchaguzi aliyo ilalamikia miaka yote? Huyu Mzee yupo timamu kweli kichwani?

Slaa tunakushauri sisi wajukuu zako kuwa Sasa umezeeka mzee.Kalale mzee pumzika mzee, hufai mzee.
Hako kaheshima kadogo uliko bakia nako kanatokana na Chadema kukupa nafasi. Huwezi ukaichafua Chadema halafu wewe ukabakia msafi. Maandiko yanasema ni heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu.
 
Dr. Slaa ni mgonjwa wa Dementia. Hili nina uhakika nalo kwa 100%. Tumsamehe anayoropoka ni kwa sababu ya ugonjwa
IMG_20220429_132918.jpg

Dementia siyo ugonjwa wa kucheka. Wazee kama Slaa wanapata sana huu ugonjwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom