Dkt Slaa aligawa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dkt Slaa aligawa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Risk taker, Apr 24, 2009.

 1. R

  Risk taker Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ONYO lililotolewa na Serikali kwa Wabunge juzi kutothubutu kutumia nyaraka muhimu za Serikali kama kithibitisho katika kujenga hoja mbalimbali Bungeni, limechukua sura mpya baada ya wawakilishi hao wa wananchi kugawanyika juu ya uamuzi huo.
  Mgawanyiko huo umetokana na baadhi ya Wabunge wa CCM kuitaka Serikali kumchukulia hatua za kisheria haraka Mbunge wa Karatu Dkt. Wilbrod Slaa (CHADEMA) na kueleza kwamba hawatarajii kuona akiachwa hivi hivi, huku baadhi ya pia wakitofautiana na wenzao na kumuunga mkono Dkt. Slaa kwa maelezo kwamba onyo la Serikali ni vitisho vinavyolenga kuwaziba mdomo Wabunge kuelekea uchaguzi Mkuu 2010.

  Wabunge watatu wa CCM, Bw. Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini), Bw. Ponsiano Nyami (Nkasi) na Bw. George Simbachawene (Kibakwe) walisema wanaungana na Serikali na kwamba hatua ya kutoa onyo imechelewa kwa maelezo kwamba tayari tabia hiyo imeiletea nchi dosari kubwa mbele ya Mataifa mengine ya nje.

  "Kwanza kabisa Serikali imechelewa kuchukua hatua na hata hivyo hatutarajii kuona akiachwa hivi hivi. Tunataka Serikali imchukulie hatua za kisheria haraka aliyekwishahusika na hilo kosa, tayari tumepata athari watu wa nje wanatuona kama watu waliochanganyikiwa," alidai Bw. Nyami akiungwa mkono na wenzake wawili.

  Naye Bw. Simbachawene alisema amesikitishwa na hali hiyo na kueleza kwamba chanzo cha tatizo hilo ni hulka ya Watanzania ya kuvumiliana, busara na hekima inayotumiwa na viongozi kutoharakisha kuwachukulia watu hatua wakitaka Watanzania waendelee kuishi kwa amani na utulivu na kuamini kwamba kila mtu akitambua hilo hawezi kufanya kile kilichofanywa na baadhi ya Wabunge kutoa siri za Serikali hadharani.

  "Kinachofanywa na Dkt. Slaa ni kutaka kuichanganya Serikali kwa ujumla ili ifikie wakati wananchi wakose imani na Serikali yao jambo ambalo ni hatari sana kwa Taifa. Anataka kutufanya kama watu wote waliochanganyikiwa, hatuwezi kukubali, Mbunge ana njia nyingi za kuishauri Serikali si kutoa siri za nchi tena kwenye mkutano wa hadhara," alidai Mbunge huyo.

  Naye Bw. Nyalandu alidai Mbunge kuweka hadharani nyaraka za siri za Serikali katika mkutano wa hadhara ni aibu kwa Taifa kubwa na lenye sifa
  njema kama Tanzania na kwamba haliwezi kuvumiliwa.

  Kwa upande wake Mbunge wa Bumbuli (CCM), Bw. William Shellukindo alisema kitaratibu zipo nyaraka za Serikali ambazo haziwezi kuwa wazi hadi kufikia kipindi cha miaka 20 au zaidi na kwamba ikibainika umezitoa unaweza kuchukuliwa hatua kali hivyo anaungana na Serikali kuhusu onyo hilo.

  "Mimi nimefanya kazi Serikalini muda mrefu, zipo nyaraka za siri ambazo haziwezi kuwa hadharani mpaka miaka 20 ya muda fulani, ukibainika umezitoa unastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Naungana na Serikali kabisa," alisema Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

  Kwa upande wake kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Bw. Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema kinachotakiwa kwa Serikali ni kushughulikia chanzo cha tatizo badala ya kuwatishia wabunge na kuwajengea hofu wananchi kuhusu taarifa za kweli kuhusu vitendo vya ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka serikalini.

  "Ushauri wangu kwa Serikali ni kushughulikia ufisadi badala ya kutishia Wabunge na kutaka kujenga hofu kwa wananchi. Kama ikishughulikia tatizo la ufisadi na kika kitu kikawa wazi utahitaji nyaraka za nini?" Alihoji Bw. Hamad.

  Kuhusu taarifa za siri zinazotokana na nyaraka Serikali kujulikana kwa watu wa nje, Bw. Hamad alisema anayedhani wapinzani ndio wamevujisha siri hizo kwa watu wa nje hana upeo mpana wa kuelewa kwa kuwa mataifa ya nje wana taarifa za siri za ufisadi wa Tanzania kuliko hata Watanzania na kuongeza kwamba hata wapinzani wanapata siri nyingine nje ya nchi.

  "Nataka nikuhakikishe kwamba hata siri ya ubadhilifu katika Wizara ya Maliasili na Utalii zimeibuliwa na nchi moja kubwa ya nje. Sisi tunapata taarifa nyingi sana nje na kushangaa kwamba kumbe nchi za nje zinajua siri za matumizi mbaya ya madaraka ya nchi yetu kuliko hata sisi Wabunge," alisema Bw. Hamad.

  Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutoatajwa majina baadhi ya Wabunge wa CCM walionesha masikitiko yao kwa Serikali kutoa onyo kwa kwao kuhusu nyaraka muhimu na kudai kuwa hilo si dawa katika nchi ya demokrasia kama Tanzania.

  Walisema hatua iliyokwishaanza kwa Bunge kutekeleza wajibu wake haitakiwi kutiwa dosari kama ambavyo Serikali inavyotaka kufanya na kwenda mbali zaidi wakidai huenda baadhi ya mafisadi wameanza kuwazidi nguvu baadhi ya watendaji wa Serikali na kukubali hoja zao za kutaka kukitaka Serikali kulegeza kamba katika vita dhidi ya ufisadi.

  SOURCE: MAJIRA
   
 2. SOARES

  SOARES Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 6, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Jamii,
  Suala siyo siri za serikali, cha muhimu ni zinamnufaishaje mlalahoi hizo siri. Nchi ni ya wote kwa nini wachache wajifiche huku wakinufaika peke yao. Ni bora kila mtu ajue kinachoendelea kwani tunaposema maendeleo ya wananchi najua ni kusonga mbele kimaisha na siyo kuuana!!

  Ii wabeja nkoyi
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hiyo ni moja ya kampeni yao kumtisha DR SLAA..

  Wamejipanga kumnyamazisha na SIX naye atatumia rungu lake pia kumtishaaa DR slaa.

  hawajazoea(CCM) uwazi wa uchafu wao kuwekwa wazi namna hiii..

  DR ALUTA CONTUNUE....
   
 4. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,293
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  CCM wameshakuwa desperate, wameamua kuanza kutishia wapinzani bila hoja za msingi ila kwa ubabe kama kawaida yao. Kwani hizo nyaraka za siri wapinzani wanazipata wapi? Si kutoka ndani yaserikali? Halafu kama ni wasafi, kitu gani cha siri? Wajisafishe halafu waone kama Dr. Slaa na wenzake watakuwa na nyaraka yoyote ya kuwaonyesha wananchi. Kikwete kubali nchi imekushinda na washikaji wako uliowajaza kwenye uwaziri, ukuu wa mikoa, wilaya na kwingineko! Wananchi tumechoshwa na tabasamu lako lililojaa hila na uongo.
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa; ALUTA Continue; tena ongeza kasi kumkoma nyani-ni njama za CCM za 2010
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kama sio kwa wananchi wanataka hizo nyaraka zionyeshwe wapi?
   
 7. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Kinachojitokeza hapa ni Wabunge kutokuelewa wajibu wao. Wajibu wa Bunge siyo kuitetea Serikali bali ni kuisimamia na kuhakikisha kuwa inatekeleza matakwa/mahitaji ya Raia wake kama ilivyoainishwa kwenye mipango na bajeti za wizara mbalimbali na kuidhinishwa na Bunge. Laiti kama Dr. Slaa angekuwa ametoa hoja za uongo, kulikuwa na haja ya Wabunge kuitaka Serikali kumchukulia hatua. Lakini hoja aliyoitoa Dr. Slaa ilikuwa ni ya ukweli na kwa kiasi kikubwa ililipatia Bunge sifa na kuwafanya wananchi wengi kurejewa na hamu ya kuangalia na kusikiliza vipindi vya Bunge ambavyo hurushwa na Runinga na Redio. Kabla ya hapo wananchi wengi walishakosa ladha ya kusikiliza na kutazama vipindi vya Bunge kwani ilionekana kama kijiwe fulani hivi; maana Mbunge wakati fulani alisimama na kuanza kutoa pongezi kwa Mbunge mwenzie au kufagilia ushindi wa Simba/Yanga.
   
 8. H

  Herbert Member

  #8
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huu mkuu ni ukweli usiofichika.

  Naona pale wanakula per deam tu. Hata hoja wanazoziridhia sidhani kama sinapitiwa kwa undani. Maswali yanayoonyesha kwamba wabunge wanaaply crirical thinking hamna kabisa.

  Bunge letu Michosho sana.
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Kwa tunavyomfahamu Dr Slaa, vitisho hivyo walivyotoa hao wanaojiita wawakilishi wa wananchi kumbe ni wawakilishi wa mafisadi ni sawa na KUMPIGIA MBUZI GITAA.
  Dr. Slaa ni jasiri,mzalendo na anayejua nini anafanya sio kama hao wanaojikombakomba kama vile ubunge wao ni kuiwakilisha serikali Bungeni.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hongera Slaa those guys are feeling the heat .Usiacha kusema tuko nyuma yako .
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Tumeshakosa imani na serikali yetu ya sasa, ni KAULI tu inasubiriwa. Wizi mkubwa umefanyika na unaendelea kufanywa serikali inasua sua kuadhibu. Nilishawahi sema wamakonde wana akili sana pindi wamkamatapo mwizi wa sukari husema "uchiteme wala uchimumunye". Hii ni kwa maana ya ushahidi. Sasa ukisuasua kwa wizi wa fedha zinakuwa-channeled in such a way evidence itapotea pamoja na viainisho vingine. Kisha inatetea na kuongoza nchi kisanii. Kwamba Slaa ata-implicate wananchi kukosa imani na serikali. FINE. Hapa anawataarifu wananchi repoti ya hali ya fedha na wizi ambayo CCM wasingesema kamwe. Sasa CCM si wezi kwa maana ya kuongoza kwa double sided na kublind fold walalahoi? I mean it is a crap.

  Wezi wa kuku hufungwa mara, wezi wa simu na fedha mitaani hufungwa au kutozwa faini mara, wafanya ajali barabarani na wanaosasababisha vifo hufungwa mara, ila wezi wa EPA, ajali za vichenge na wauaji wa silaha kama Marehemu Dito hawa ni senior citizens na katiba inatakiwa ielewe hivyo. And the list goes on. I mean I do not see why tusikose imani na serikali yetu ya sasa?
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sheria ni lazima ichukue mkondo wake kama mbunge atavuka mipaka basi itabidi achukuliwe hatua tu ,hili natumai lipo na wabunge wanalifahamu. Tunapigia makelele utawala wa sheria ,hivyo tuwe wakweli na kukubali.

  Tusiende kichwa kichwa lazima ziwepo mbinu zingine za kufichua maovu na ushahidi uwepo pale ambapo mtu atapelekwa mahakamani hapo nyaraka za madai zinaweza kuekwa hadharani.

  Mbinu za kuyasema maovu ya serikali yaliokutwa ndani ya nyaraka za siri zinaweza kuhubiriwa katika mikutano,vikao vya bunge na sehemu nyingine kwa kuzisuka habari zilizomo ndani ya nyaraka na kuziwakilisha kivyako vyako kwa uhakika zaidi bila ya kudai kuwa una ushahidi ,zaidi utadai anaepinga aende mahakamani huko ndiko kunakotakiwa ushahidi na ikiwa ndani ya bunge kunatakiwa ushahidi vilevile utazusha hoja ikiwa ushahidi utaonyeshwa nini kitafuata na unaweza kutoa ushahidi kwa kuandika kivingine kabisa na kuwakilisha na wao watafute hizo nyaraka walizonazo kulinganisha na ushahidi.

  Kwa ufupi kunahitajika mbinu za kuzizungumza siri za ufisadi maana ikiwa una tarehe za mambo ya ufisadi ambayo yamo kwenye documents ,basi itatosha kuwatajia tarehe bila ya kuonyesha maandishi halisi ,na doc halisi utazicopy na kuzihifadhi kwenye mitandao na email zako ,unageuza email yako kama sehemu muhimu ya kuhifadhi nyaraka ila isiwe common email ambayo umejiunga nayo hapa JF inakuwa ni separate na huitumii kupeleka wala kupokea email ,ipo tu kuhifadhi mambo yako ya private hivyo hata wakikagua PC yako hawakuti kitu.
   
 13. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  siri za serikali ndo siri gani hizo ? je wabunge (akiwemo dr slaa) sio sehemu ya hiyo serikali ? sasa kama wao ni sehemu ya serikali kuna ubaya gani hao wabunge wasitumie hizo nyaraka ? au serikali ni ya wabunge wa ccm pekee ?

  kinachoshangaza bunge zima linapelekeshwa na mtu mmoja tu, Dr. Slaa !

  Hongera zako Mheshimiwa Dr. Willy Slaa
   
 14. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kwani Lazaro na wenzie wako kwa ajili ya kuwasaidia wananchi huyu bwana si alibebwa kwa mgongo wa mama Mkapa pindi tu alipotoka huko marekani,ili aishi si lazima ajipendekeze mchango gani amewahi kuutoa kwa taifa na wananchi wake? zaidi ya kuchumia tumbo.Wananchi tuanze kukemea wabunge wachumia tumbo na ikibidi tuwalipe ujira wao punde tu 2010.
  Hivi kweli mtu aliye na akili timamu atazungumzia DR. Slaa na wenzake wanaotimua mabomu ya uhujumu kuwa achukuliwe hatua, Hivi serikalini ni nini na ni ya nani. hawa wabunge wetu wamelewa mil 7.wanazolipwa pasipo jasho.
  watanzania tumegeuzwa mabwege muda mrefu ila wanagalie ukimwamsha aliye lala uta lala mwenyewe. imefikia wakati wa kuwalaza kina Lazaro na watu wa sampuli yake.
   
 15. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanatafuta cheap populality either ili waendelee kuteuliwa kuwa wabunge au waje teuliwa kuwa mawaziri. hakuna cha siri kama ufisadi unafanyika katika idara hata kama ni mimi nitautoa tuu. Mfano ukaguzi uliofanyika Boti mwanzo walipogundua kuwa maovu yamegundulika wakawafukuza wakaguzi. Ningekuwa mfanyakazi wa Boti hizo taarifa ningepenyeza tu ili umma ujue nini kinaendelea. Mafisadi wasifanye Tanzania ni ya kwao even we poor people we need to enjoy prosperity in our country.

  Viva Dr. slaa na watendaji wote wa serikali wenye moyo wa kufichua maovu.
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Napata shaka kuhusu ufahamu wa baadhi ya wabunge, kusema tu wanaunga mkono onyo la serikali ina maana gani? Wanaunga mkono serikali kuiba? Kwa maana nyingine siri zinazozungumziwa hapa zinahusu ufisadi uliofanyika, kwa hiyo serikali imedhalilika kwa ufisadi kuwekwa hadharani? Ni bora kuwa na taifa lililodhalilika kuliko heshima inayolindwa kwa nguvu. Wangekuwa na akili wangeishauri serikali isiwe na nyaraka za wizi zinazoitwa za siri.
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  DR. Slaa kaza buti wananchi wengi tuko nyuma yako!!. Kitu kilichowachanganya hawa wabunge hasa wa CCm ni kule mshahara na marupurupu yao kuanikwa na wananchi kujua jinsi wanavyokomba mamilioni ya wapiga kura wao huku wapiga kura wakifa na njaa!! Mshahara wa mbunge sio siri hata siku moja, na hata hizo wanazosema ni siri mataifa ya nje yamezipata kutokana na wabunge kuzitoa humo bungeni sio kweli; hakuna taarifa ya nchi hii ambayo mataifa kama Marekani na Uingereza wanazihitaji wasizipate in fact ukitaka taarifa/siri juu ya Tanzania ni rahisi sana kuzipata ukiwa washington D.C.kuliko ukiwa Dar!! Sasa hawa wabunge wanaomsakama DR. Slaa kwa wanachokiita kutoa siri ni kwasababu ya ignorance yao tu. Tanzania hakuna SIRI ambayo mataifa makubwa hayaiju; Kwahiyo ni ujinga tuu unawasumbua hawa wabunge wa CCm kumuandama DR. Slaa zote hizo ni mbinu chafu za kuficha ufisadi wao.
   
 18. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa wamekamatwa bapaya, na dawa yao ni moja tu kuwazomea wakija huku majimboni! Kumbe tukidhani wanaenda tuwakilisha wao wanaenda kujaza matumbo yao na kujifanya eti ni siri. Ndo maana huwa wana sinzia tu na hawawezi kuhoji lolote kwani mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Big up Dr.. slaa. Tunataka wazalendo kama nyie.

  Slaa kwanini usigombee upresidaa??
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Haya mambo yalimshinda Marmo alipotaka kuyaibua ktk bunge lililopita ila sasa naona jamaa wamebanwa ktk kona mbaya.
  Ila nilichojifunza hapa ni kwamba SERIKALI inaficha maradhi yaani hizo siri zinazotakiwa kufichwa ni WIZI MTUPU. mikataba feki, vijimemo vya wizi kule hazina na taka taka zinginezo.

  Mmbona hakuna nyaraka hata moja inayonyumbua masuala ya ulinzi na usalama mbayo imewekwa hewani au peupe? Serikali na wadau wake watambue kuwa wao ni watanzania kama sisi na nchi ni yetu wanachi hivyo kama kuna mambo zanayogusa maslahi ya taifa yanafanyika gizani basi hiyo ni dalili ya UHAINI ambao sasa unawatokea puani.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nitawauliza swali moja tu hawa Wabunge waloshindwa kusimama siku zote kukemea Ufisadi lakini leo maneno yanawatoka inapofikia swala la Dr. Slaa kwa sababu wanajua hana Ubavu..ili tupate kuelewa hili neno siri za serikali linatumika vipi kisheria..

  Swali lenyewe rahisi sana... Je, Kuna siri inayotakiwa kusitiriwa, ikiwa baba kampa Mimba mwanae wa kike?..

  Na hadi lini ikiwa mimba hawezi kufichika!.. Jamani, nyaraka zile ziznzungmzia zaidi n ani kampa mimba mwana hii sio siri hata kidogo, Ufisadi hautokanani na siri ya Uwekezaji nchini isipokuwa ni matokeo ya matendo haramu ya baadhi ya mikataba uwekezaji nchini..Kuna wawekezaji wengi sana nchini ambao nyaraka zake ni siri na zimebakia kuwa siri kwa sababu hakuna utata...
  Kwa ufafanuzi zaidi, hawa Wabunge ni lazima wafahamu kwamba hakuna Mtanzania hata mmoja anayepinga uwekezaji nchini kwa maana ya mtoto wa kike kupata mimba..
  Ni jambo la kheri na sote tunategemea maendeleo hayo kutokea na sii lazima kila mtu afahamu relation kati ya serikali na mwekezaji ilianza vipi!..Kuna mikataba mingapi nchini ambayo imewekwa na hakuna mtu anazo nyaraka zake isipokuwa hii michache ambayo inawaweka viongozi hatuiani?..Wajiulize kwanza why ime leak?.. kwa sababu ni Haramu, ni kitendo haramu kama cha mzazi kumpa mimba mwanaye ndicho kinachoondoa Usiri halali wa makubaliano kati yao..
   
Loading...