Wazee hawawezi kusuluhisha kwani katika katiba ya KKKT hakuna mahali inaposema waitwe wazee kutatua migogoro ya kanisa. Mkutano mkuu uliofanyika Mbeya ulikuwa halali. Akina Mwaikali ni viburi tu vinawasumbua na wanaomtetea wote ni wapambe wake tu. Kanisa ni la Mungu na waumini. Kila kitu kinachoamuliwa lazima kiguse wenye kanisa yaani waumini. Mgogoro ni kuhamisha makao makuu toka Tukuyu hadi Mbeya. Haya mengine wanayosema ni porojo tu. Wanaposema kiti kirudi ina maana makao makuu yarudi Tukuyu. Kiti cha Askofu kinakaa makao makuu ndiyo maana wanasema kiti cha Askofu kirudi TKY. Akina Mwaikali na genge lake wanamdhalilisha mkuu wa Kanisa ambaye ni Mwenyekiti wao kwenye vikao vyao vya maaskofu na ni mwenyekiti wa halmashauri ya kanisa la KKKT. Wanasemaje hana mamlaka? Yaani mkuu wa kanisa hana mamlaka ya kutatua migogoro ya kanisa? Kwanini tuna mkuu wa kanisa? Basi kila dayosisi ingejiendesha yenyewe independently bila kuwa na huu umoja uliopo wa makanisa yote. Hawa wanaturudisha nyuma wakati makanisa ya kulutheri yalikuwa hayajaungana. Sasa hivi tumeungana hivyo lazima mkuu wa kanisa apewe heshima yake ya kuwa kiongozi mkuu wa makanisa yote Tanzania.Kwa mujibu wa askofu Mdegela wanaopaswa kusuluhisha ni wazee wa huko zkonde akina Prof Mwandosya na wenzake siyo kamati ya maaskofu.
Mchawi mpe mwanao amlee ndicho alichotaka kufanya Shoo!