johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,875
- 141,809
Kwa mfano Kanisa Katoliki wao Mkuu wa Kanisa ni Papa na kila Dayosisi inajitegemea chini ya askofu wake aliyeteuliwa na Papa.
Ila kuna Rais wa baraza la maaskofu (TEC) yeye hutokana miongoni mwa maaskofu lakini hana nguvu kwenye shughuli za kila Dayosisi.
Anglican wao Askofu mkuu anaingia hadi kwenye shughuli za kila Dayosisi na anaweza kufanya maamuzi hata ya kumsimamisha askofu kama amekiuka taratibu.
Sasa kufuatia mgogoro wa Dayosisi ya Konde nimesikia baadhi ya maaskofu wa KKKT wakimtambulisha Dr Shoo kama Mkuu wa Kanisa na wengine wanamtambulisha kama Askofu mkuu.
Waumini wa Konde wanadai askofu Dr Shoo ndio kiini cha huo mgogoro kwa sababu haelewani na askofu Malasusa wa DMP ambaye kiasili Konde ndiyo nyumbani kwao. Waumini wanadai askofu Dr Shoo hana mamlaka ya kuwaamulia jambo lolote.
Waumini wa KKKT naomba ufafanuzi Tafadhali.
Ni kama katiba ya ACT Wazalendo ni ngumu kujua kazi za Zitto Kabwe na Mzee Haji Duni.
Mungu wa mbinguni awabariki nyote!