Dkt. Shoo ni Mkuu wa KKKT au ni Askofu mkuu wa KKKT? Maana kuna tofauti hapo!

Kwa mujibu wa askofu Mdegela wanaopaswa kusuluhisha ni wazee wa huko zkonde akina Prof Mwandosya na wenzake siyo kamati ya maaskofu.

Mchawi mpe mwanao amlee ndicho alichotaka kufanya Shoo!
Wazee hawawezi kusuluhisha kwani katika katiba ya KKKT hakuna mahali inaposema waitwe wazee kutatua migogoro ya kanisa. Mkutano mkuu uliofanyika Mbeya ulikuwa halali. Akina Mwaikali ni viburi tu vinawasumbua na wanaomtetea wote ni wapambe wake tu. Kanisa ni la Mungu na waumini. Kila kitu kinachoamuliwa lazima kiguse wenye kanisa yaani waumini. Mgogoro ni kuhamisha makao makuu toka Tukuyu hadi Mbeya. Haya mengine wanayosema ni porojo tu. Wanaposema kiti kirudi ina maana makao makuu yarudi Tukuyu. Kiti cha Askofu kinakaa makao makuu ndiyo maana wanasema kiti cha Askofu kirudi TKY. Akina Mwaikali na genge lake wanamdhalilisha mkuu wa Kanisa ambaye ni Mwenyekiti wao kwenye vikao vyao vya maaskofu na ni mwenyekiti wa halmashauri ya kanisa la KKKT. Wanasemaje hana mamlaka? Yaani mkuu wa kanisa hana mamlaka ya kutatua migogoro ya kanisa? Kwanini tuna mkuu wa kanisa? Basi kila dayosisi ingejiendesha yenyewe independently bila kuwa na huu umoja uliopo wa makanisa yote. Hawa wanaturudisha nyuma wakati makanisa ya kulutheri yalikuwa hayajaungana. Sasa hivi tumeungana hivyo lazima mkuu wa kanisa apewe heshima yake ya kuwa kiongozi mkuu wa makanisa yote Tanzania.
 
Kwa mfano Kanisa Katoliki wao Mkuu wa Kanisa ni Papa na kila Dayosisi inajitegemea chini ya askofu wake aliyeteuliwa na Papa.

Ila kuna Rais wa baraza la maaskofu (TEC) yeye hutokana miongoni mwa maaskofu lakini hana nguvu kwenye shughuli za kila Dayosisi.

Anglican wao Askofu mkuu anaingia hadi kwenye shughuli za kila Dayosisi na anaweza kufanya maamuzi hata ya kumsimamisha askofu kama amekiuka taratibu.

Sasa kufuatia mgogoro wa Dayosisi ya Konde nimesikia baadhi ya maaskofu wa KKKT wakimtambulisha Dr Shoo kama Mkuu wa Kanisa na wengine wanamtambulisha kama Askofu mkuu.

Waumini wa Konde wanadai askofu Dr Shoo ndio kiini cha huo mgogoro kwa sababu haelewani na askofu Malasusa wa DMP ambaye kiasili Konde ndiyo nyumbani kwao. Waumini wanadai askofu Dr Shoo hana mamlaka ya kuwaamulia jambo lolote.

Waumini wa KKKT naomba ufafanuzi Tafadhali.

Ni kama katiba ya ACT Wazalendo ni ngumu kujua kazi za Zitto Kabwe na Mzee Haji Duni.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
Ni askofu mkuu na ni mkuu wa kkkt.
 
Mkanisa ya kiluteri yameungana kivipi?

Ufafanuzi Tafadhali!
 
Ni vyote viwili
 
Huo mgogoro uchunguzwe yasije yakawa yale ya KKKT dayosisi ya meru kukusanya sadaka halafu matumizi yanapangwa KKKT Moshi nakumbuka lile tifu lake halikua la kitoto.
 
Supreme leader na mwenyekiti

Kuna jamaa alitoka mahali akisema kabaniwa kuwa mwenyekiti

Matokeo yake kaenda kwake katengeneza nafasi ambayo hataki kuchallenjiwa ndio mjue yule jamaa ni ndumilakuwili haaminiki hataka chembe
 
Mkanisa ya kiluteri yameungana kivipi?

Ufafanuzi Tafadhali!
Soma hii makala hii uelewe.

Ifahamu Historia ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)​

JAIZMELA July 09, 2020
"Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya KKKT inaelezwa kuwa Mwaka 1887 kazi ya Injili kwa Kanisa la Kilutheri ilianzishwa nchini Tanganyika (baadaye Tanzania) na Chama cha “Misioni cha Berlin III” au “Evangelical Missionary Society for East Africa” (EMS) kutoka Ujerumani. Kituo cha kwanza cha misheni kilikuwa ni Kigamboni, Dar es Salaam.

Chama cha pili, yaani “Chama cha Misioni Berlin I”, nacho kutoka Ujerumani, kiliingia Tanganyika kikitokea Afrika ya Kusini na kuanza kazi Nyanda za Juu Kusini mwaka 1891 kilipoanzisha kituo cha misheni sehemu iitwayo Ipagika au Pipagika (Wangemannshöhe) katika Dayosisi ya Konde.

Mwaka 1890 “Chama cha Berlin III” kilibadilika na kuchukua sura mpya baada ya kubadili sera yake na kujulikana kwa jina la “Bethel” au “Misioni ya Bethel”. Misioni hii ikafika Tanga na kuanza kazi eneo la Mbuyukenda. Baadaye Misioni ya Bethel iliamua kufikisha Injili ya Kristo nje ya mipaka ya Tanganyika. Wamisioari waliohusika walipanga kwenda Rwanda kupitia Bukoba. Walipofika Bukoba mwaka 1910 wakashawishika kufungua kituo Bukoba na ile nia ya kuanzisha kazi ya misioni Rwanda ikawa imesitishwa.

Chama cha tatu kufka Tanganyika ni “Chama cha Misioni cha Leipzig” (nacho kilitokea Ujerumani). Kiliingia nchini mwaka 1893 na kuanza kazi ya misioni Kaskazini ya nchi kwa kuweka kituo cha misheni Kidia, Old Moshi.

Kutokana na vyama hivyo vitatu kijiti cha kueneza Injili ilipokelewa na wenyeji toka kwa wamisionari wa Ujerumani.
Na vyama vingine vya misioni vilivyofka baadaye kutoka Ulaya na Marekani navyo vilieneza Injili kwa kufundisha Neno la Mungu kwa upendo na kwa usahihi, hasa baada ya Vita ya I ya Dunia (1914 - 1918) na Vita ya II ya Dunia (1939 - 1945).
Pamoja na kueneza Injili, Kanisa lilianza kutoa huduma mbalimbali za kijamii na diakonia kwa lengo la kumhudumia mwanadamu kikamilifu – kimwili, kiroho na kiakili. Makanisa saba yanayojitegemea ambayo baadaye yaliungana na kuunda Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika yalianzishwa.

Mnamo Juni 1963 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanganyika (KKKT) likaundwa. Baada ya KKKT kuanzishwa Kanisa la Ubena-Konde (eneo la Nyanda za Juu Kusini) likaitwa Dayosisi ya Kusini; Kanisa la Uzaramo-Uluguru likaitwa Dayosisi Mashariki na Pwani; Kanisa la Usambara-Digo likaitwa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki; Kanisa la Kaskazini likaitwa Dayosisiya Kaskazini; Kanisa la Mbulu likaitwa Dayosisi ya Mbulu; Kanisa la IrambaTuru likaitwa Dayosisi ya Kati na Kanisa la Kaskazini Magharibi likaitwa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi.

Yapo maeneo nchini ambayo yalikuwa yanafanya kazi ya Injili kama misheni nayo ni: Mkoani Mara, Mashariki ya Ziwa Victoria, Ruvuma, Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Kusini Mashariki ambayo sasa ni Dayosisi. Dayosisi za mwanzo nazo kwa kutegemea vigezo vya kikatiba na historia zikaendelea kugawanyika na hadi 2014 KKKT ikawa na Dayosisi 24 kama ifuatavyo: Dayosisi ya Kusini, Dayosisi ya Konde; Dayosisi ya Iringa; Dayosisi ya Kusini Kati; Dayosisi ya Kusini Magharibi; Dayosisi Mashariki na Pwani; Dayosisi ya UlangaKilombero; Dayosisi ya Morogoro na Dayosisi ya Dodoma. Nyingine ni Dayosisi ya Kaskazini Mashariki; Dayosisi ya Kaskazini; Dayosisi ya Kaskazini Kati; Dayosisi ya Pare; Dayosisi ya Meru; Dayosisi ya Mbulu, Dayosisi Mkoani Mara; Dayosisi ya Kati; Dayosisi ya Kaskazini Magharibi; Dayosisi ya Karagwe; Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria; Dayosisi ya Ruvuma; Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria; Dayosisi ya Kusini Mashariki na Dayosisi ya Ziwa Tanganyika."

Hayo makanisa tajwa hapo juu yalikuwa yanajitegemea hadi yalipoungana mwaka 1963.
 
Mhhhh, wewe nawe hujui kitu, nani alikudanganya kwamba Simba na Yanga kuna vita ? Pale kuna utani wa jadi tu na burudani. Hayo mambo ya vita unayajua wewe usiyefahamu soka.
mkuu unakumbuka ile mechi washabiki wa simba waliwapiga mashabiki wa yanga
 
Back
Top Bottom