Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
WAPINZANI WAKE WAMKAMIA KUMG'OA DODOMA
na Mwandishi wetu
KINYANGANYIRO cha uteuzi wa urais Zanzibar, kimeingia katika hatua mpya baada ya kuwapo mkakati wa kutaka kumwengua Dk. Ali Mohamed Shein kwa madai kuwa hana sifa.
Mkakati huo ambao Tanzania Daima Jumatano imeunasa, unaandaliwa na kundi la wapinzani wake kisiasa katika kuwania kiti hicho ambapo harakati zake wiki hii zimehamia mjini Dodoma kutakakofanyika vikao vya uteuzi.
Tayari wapambe na mashabiki wa wagombea 11 wanaowania uteuzi wa kiti cha urais visiwani Zanzibar kinachoshikiliwa na Rais Aman Abeid Karume, wamewasili mjini Dodoma kuwapigia debe wagombea wao mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC).
Duru za siasa kutoka mjini Zanzibar na Dodoma kwa nyakati tofauti, zimethibitisha kwamba wapinzani wa Dk. Shein anayepewa nafasi kubwa kutokana na kuungwa mkono na vigogo wa serikali, wamekamia kutumia sheria ya Katiba ya Zanzibar kumuengua kwenye kinyanganyiro hicho.
Vyanzo vyetu vya habari vilisisitiza kuwa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 1984, ndiyo itakayotumika kumbana Makamu huyu wa Rais wa Muungano.
Kwa mujibu wa Katiba hiyo toleo la mwaka 2003, iliyopitishwa Julai 17, sura ya 15, kifungu cha pili kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa Rais wa Zanzibar.
Kifungu hicho chenye sehemu (a) hadi (d), kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa rais wa Zanziabr kuwa ni pamoja na kuwa Mzanzibari wa kuzaliwa, awe ameshatimiza umri wa miaka 40.
Sifa nyingine ni kwamba awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na sifa ya mwisho inamtaka awe mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa 1992.
Katika kifungu cha 2(C), kinachosema awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ndicho kitakachotumika kumbana Dk. Shein maana hana sifa hiyo, alisema mmoja wa makada wa CCM.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na kwamba awe Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 21.
Sifa nyingine ambayo wapinzani wa Dk. Shein wamejipanga kumnyuka nayo ni ile ya kifungu cha 68(b) ambacho kinasema awe amejiandikisha au ana sifa za kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
Kifungo hicho kinadaiwa kinaweza kuwa kitanzi kwa Dk. Shein kwani hakujiandikisha katika jimbo lake la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
Kwa hiyo, Dk. Shein ana mtihani mzito wa kuteuliwa maana hakujiandikisha katika jimbo lake kama mpiga kura. Amekiweka chama na yeye mwenyewe kwenye wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi, alisema mmoja wa wajumbe wa NEC ya CCM.
Hata hivyo kifungu hicho cha Katiba kimewagawa baadhi ya wana-CCM hasa wanaomwunga mkono Dk. Shein kwamba hawezi kubanwa nacho.
Mmoja wa watetezi wa Dk. Shein ambaye ni mjumbe wa NEC, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa Dk. Shein hawezi kubanwa na kifungu hicho na wanaopanga kumwekea pingamizi, wameshindwa kukisoma na kukielewa vizuri.
Waambie wasome vizuri kifungu hicho na hata nyie waandishi wasaidieni. Hicho kifungu kinasema awe amejiandikisha au na sifa ya kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.
Kwa hiyo, kama hakujiandikisha kupiga kura katika jimbo lake, haina maana kwamba hana sifa maana kifungu kinasema awe amejiandikisha au awe na sifa ya kujiandikisha. Sifa za mtu kujiandikisha zipo na Dk. Shein anazo, hivyo hakuna kibano hapa ila watu hawajui kukitafsiri kifungu hicho cha Katiba, alisema kada huyo.
Wakati wapinzani wake wakijipanga kumnyuka kwa kutumia kifungu hicho cha sheria, Dk. Shein tayari alishaeleza mara mbili juu ya kifungu hicho ambapo mara ya mwisho alijieleza kwenye kikao cha Kamati Maalum ya CCM, Zanzibar.
Tatizo la Dk. Shein linafanana na lile lililowahi kumkuta Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ambapo mwaka 2007 alizuiliwa na sheha kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura kwa madai kuwa alikuwa hana makazi maalum.
Endapo Maalim Seif angeshindwa kujiandisha, wapinzani wake kisiasa walipanga kutumia Katiba ya Zanzibar kumuengua kwenye kuwania kiti cha urais. Hata hivyo Maalim aliruhusiwa kujiandikisha.
Katika harua nyingine, wapambe wa waliomba uteuzi kuwania urais Zanzibar, wako mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya juu vya maamuzi vinavyotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii, mjini Dodoma.
Kama ilivyo ada ya mkutano mkuu wa CCM, mji wa Dodoma umefurika wapambe wa wagombea ambao wamekuwa wakikesha kupiga kampeni.
Tayari makada watano kati ya 11, walioomba kuteuliwa kuwania nafasi ya urais Zanzibar, wamependekezwa kwa kupewa alama za juu na kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Waliopendekezwa ni pamoja na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein, Naibu Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Haroun Ali Suleiman.
Wagombea wengine ni Balozi Ali Karume, Hamad Mshindo, Mohammed Yusuf Mshamba, Mohammed Aboud, Mohamed Raza na Mussa Omar Sheha
Source: Tanzania Daima.