PostGE2025 Dkt. Rioba wa TBC: Niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania

PostGE2025 Dkt. Rioba wa TBC: Niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kama anataka kulinda taifa akawatandike risasi watekaji na wauaji wa raia.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook amesema yupo tayari kuomba silaha kwaajili ya kuilinda Tanzania dhidi ya tishio lolote la usalama na amani kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 1990.

"Mwaka 1990 nikiwa JKT, Chimala, Mbeya, nilikaa miezi 3 nikiwa na bunduki kulinda madaraja ya reli na barabara pale dhidi ya tishio la makaburu wa Afrika Kusini. Leo hii niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania kutoka kwa maadui wa sasa, ambao sisi wengine tunawajua!"

View attachment 3511350
Tishio gani la makaburu 1990, mwaka ambao De Klerk alimuachia Mandela?

Amandla...
 
Rioba aache uongo! ... Mtu mzima kusema uongo hadharani haipendezi hasa akiwa kwenye nafasi ya upashanaji habari...
Mandera aliachiwa February 1990 kutoka gerezani, hakukuwa na tishio lolote la kulazimisha kulinda madaraja, ilikuwa ni matayarisho ya utawala wa kibaguzi kufikia tamati.

Labda kama alikuwa anabeba silaha kwa raha zake.... Lakini ni mtunza silaha gani huyu aliyemruhusu kuwa na silaha bila kuwa na tishio la Vita?
 
Huyu Dr vipi, amani HAILINDWI kwa mtutu - kinacholindwa ni HAKI ambayo by default huzaa AMANI.

Hata kwako we Dokta ondoa Haki kwa mkeo na wanao afu uone kama kutakuwa na Amani humo ndani hata kama friji limejaa nyama - hapatakalika.
 
Anakaa kwenye nyumba ya serikali
Anaendeshwa kwenye gari ya serikali

Kwanini asiwe mkali sponsor wake anapokuwa na stress
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook amesema yupo tayari kuomba silaha kwaajili ya kuilinda Tanzania dhidi ya tishio lolote la usalama na amani kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 1990.

"Mwaka 1990 nikiwa JKT, Chimala, Mbeya, nilikaa miezi 3 nikiwa na bunduki kulinda madaraja ya reli na barabara pale dhidi ya tishio la makaburu wa Afrika Kusini. Leo hii niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania kutoka kwa maadui wa sasa, ambao sisi wengine tunawajua!"

View attachment 3511350
Apewe silaha kama ni rahis? Watu wa propaganda bwana strong on the keyboard waka oct 29 alikimbilia dodoma
 
Back
Top Bottom