Dkt. Nchimbi: Mimi ni mtu wa misimamo, Utamaduni wa CCM unajulikana Rais anahudumu awamu 2 nawaambieni Mapema kabisa!

Hivi Saa100 ni raisi wa awamu ipi ?.Naona watu wachache ndio wanaojua kwamba huyu ni raisi anayemalizia awamu ya tano ambayo inaishia oktoba 2025.Huyu alikuwa mgombea mwenza wa JPM,hivyo baada ya kutangaziwa ushindi moja kwa moja akawa makamu wa raisi
.JPM asingefariki basi wote wangemalizia awamu ya tano kwa pamoja.Kwa hiyo fomu zinatakiwa zitolewe zaidi ya moja.Au mna hofu kwamba zikiwa fomu zaidi ya moja Saa100 hatatoboa.Kinachowasumbua ni uchawa wenu.
 
Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi amesema yeye anajulikana kwa misimamo yake na kama hawapendi misimamo basi wamuondoe tu mapema kabisa

Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi

Mungu mbariki Dr Nchimbi
Kwahiyo mgombea huko ccm anapatikana kwa msimamo wa katibu mkuu na sio katiba Yao?!
 
Ninavyoelewa mimi vipindi viwili vya Samia havijaanza.
Anamalizia ngwe ya JPM, Halafu aanze vipindi vyake, hivyo basi 2025 ni kapu la wote, halina mwenyewe,Sandakalawe mwenye kupata na apate.
Hata mimi nilikuwa naelewa hivyo. Mchakato ufanyike kumpata mgombea. Ndio demokrasia yenyewe.
 
Yaani huyu hafiki hata miezi sita ccm watakuwa washamfanyia zengwe na ataondolewa kiti kitakuwa wazi. Polepole huwa anaaema sana wahuni ccm wapo wengi
 
Katibu wa CCM akitetea ugali wa Mwenyekiti wa CCM...simple as that
 
Inaonekana ndani ya Ccm kuna upinzani mkubwa dhidi ya Dr Samia kuzidi ule wa Membe dhidi ya Magufuli.

Yaani kila move anayochukua Mwenyekiti wa CCM Taifa inalenga ku secure kiti chake.

This time wanamkimbiza Mwizi kimya kimya.
TISS wakiwa wapi?
 
uzuri wa maisha mambo hujirudia, mlango walioingilia ndio watakao tokea, 2025 tuna raisi mwingine imeshapangwa hivyo na aliyewaweka hapo na ndiye atakayewatoa kama ni wabishi wakamuulize bosi wao uhuru kenyata na raila odinga …
Boss wao Uhuru kwa namna gani mkuu
 
Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi amesema yeye anajulikana kwa misimamo yake na kama hawapendi misimamo basi wamuondoe tu mapema kabisa

Utamaduni wa CCM ni Rais wa JMT kuhudumu kwa Mihula miwili hivyo nawaambieni Mapema kabisa tusije kuzinguana huko mbele ya safari, amesisitiza Dr Nchimbi

Mungu mbariki Dr Nchimbi
2021-2025,anamalizia ngwe ya Hayati tu, na si rais wa kuchaguliwa na wananchi, 2025-2030, sasa hapa anachaguliwa na watanzania kwa awamu ya kwanza, 2030-2035, hapa ndipo anamalizia vipindi vyake viwili.
 
Back
Top Bottom