Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.
Barua yawezekana ilikuwepo/ipo lakini haikuandikwa na Mahakamahaihitaji kuwa na elimu kubwa sana kujua hili
+kama barua haikuwepo naibu spika alianzaje kuruhusu mjadala ule bungeni ?
Hayo maneno mwamkyembe amueleze Naibu spika aliyeruhusu mjadala wa barua ambayo ofisi yake haijaipokea.
Au ndo ccm mlikua mnapima upepo then mjiandikie barua wenyewe?
mwakembe naye anasema maneno haya au utakuwa umemkote vibaya?
Hii piga nikupige haina tija kwa taifa na nashauri hawa viongozi wetu wawe makini kutoa matamko. Hakika hiki ni kipindi kigumu sana kwa taifa letu na wangekuwa watu makini wasingethubutu kusema haya kama hili ni la kweli na kalitoa huyu Mheshimiwa. Mantiki ndogo tu inaelekeza kwamba iwapo madai ya kuwasilishwa barua ya mahakama yangekuwa ya uongo, ilitakiwa hiyohiyo jana likanushwe, kwanza na bunge kwamba halijapokea barua hiyo na mahakama kwamba haijaandika barua hiyo. Yale maneno ya Naibu Spika na Waziri Mkuu jana hayakutoa picha ya kanusho wala dalili zake. Kuibuka kwa hizi tahadhari leo tena kutoka kwa wabunge au mawaziri kwa mtindo huu inatia shaka. Angalizo langu, yanatengenezwa mazingira mabaya sana ambayo iwapo hayatadhibitiwa yatawajengea watanzania fikra mbadala ambazo kwangu sina matatizo nazo bali tatizo langu ni namna/ njia watakayoitumia kuziwasilisha. I have spoken.
Yaani hata mimi sielewi kwa nini Ndugai aruhusu mjadala kwa kitu ambacho hakipo!haihitaji kuwa na elimu kubwa sana kujua hili
+kama barua haikuwepo naibu spika alianzaje kuruhusu mjadala ule bungeni ?
Kejeli za namna hii zinakera sana!Ile sumu iliharibu ngozi na ubongo.
Pinda na Ndugai hawapo. Yuko Mwenyekiti Zungu.