Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.
Naanza kwa kusema mimi ni mwana CCM.
Pili, ni mwana CCM nisiyeshabikia maovu katika jamii yetu na anaye ficha ficha uozo kila unapotokea.
Hivyo basi uozo unapojitokeza, uwe umefanywa na mtu au taasisi yoyote ile, napendelea ukweli ujulikane ili yaliyokosewa yasahihishwe.
Na nafikiri huo ndio msingi wa utawala bora.
siyo siri kwa hivi sasa, kulingana na tafiti tofauti, kuwa idara za mahakama, polisi, ardhi na hata tawala za mikoa ndizo zinaongoza kwa RUSHWA nchini.
Sasa tumujishuhudia wenyewe Jaji wa ngazi za juu akichukua mulungula na hivyo kushiriki katika uovu wa kuibia wananchi.
Katika suala la escrow account, Jaji Werema na hata yule Luhangisa ni dhahiri wamefedhehesha taaluma zao na intergrity kwa yale ysnayojiri juu ya kugawana mabilioni ya escrow account.
Achia mbali hilo suala ni criminal, lakini hata impartiality hakuna.
Sasa anapokuja mwanasheria kama Mwakyembe na kutetea uozo uliotokea, hili linatushangaza wengi.
Mbaya zaidi, ati bunge la wananchi liliombe radhi mahakama iliyojaa rushwa na wizi hadi ngazi ya majaji.
Je serikali ina misread public anger juu ya sakata hili?
Kwa kumkubushs usemi wake mwenyewe, huyu ni Mwakyembe kweli( aliyechunguza ufisadi wa Richmond) au ni fotocopy?
Kwamkweli tunamshangaa Mwakyembe kwa kutetea ufisadi huu, na hivyo ku doubt moral justification yake wakati wa kumuondoa mh Lowasa mwaka 2007.
Kwa hili historia itamhukumu kuwa ni kigeugeu na oppurtunist wa kisiasa, na kwamba kwa kweli kama wanasiasa wengi, anatazama tu mkate wake unatoka wapi.