Dkt. Mwakyembe: Bunge liiombe radhi Mahakama

Dkt. Mwakyembe: Bunge liiombe radhi Mahakama

[uQUOTE=jameskijalo;11196046]Nimnafiki mwakyembe yeye aripokuwambunge aripigakerere sana juu ya rechimond reo kapewamadaraka anajifanya ajuirorote[/QUOTE]
Duh!!!! Wewe umezidi, hizi r r r r zimezidi mno..
 
Nimegundua hapa JF kuna watu wanaandika coment bila kulijua jambo kwa undani kama GT. Wengi wanaanduka si kwa facts ila ni kwa hisia zao kutokana na uungaji mkono wao baina ya CCM na Ukawa. Suala la kuwepo kwa barua toka mhakama kwenda bunge liliibuliwa na ukawa na kusema barua hiyo imepelekwa bungeni na Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya mjadala Ndugai alisema bunge halijapokea barua ya aina hiyo, kwa hiyo barua hiyo ilikuwepo kwa dhana tu. Lissu wakati anachangia alisema "kama barua hiyo ipo" maana yake hata yeye hakua na hakika kama kuna barua ya aina hiyo
Wee unajiona ndo GT mkuu humu jamvini lakini sijaona cha maana ulichoandika. Kinachojadiliwa hapa ni kama barua au maandalizi ya hiyo barua hayakuwepo kabisa kwanini Naibu spika (ambaye anapaswa kujua uwepo au kutokuwepo kwa barua) aruhusu mjadala wa kitu kisichokuwepo? Mbali zaidi akatoa nafasi kwa watu zaidi ya 6 mmoja baada ya mwingine kudebate kwenye kitu hewa? Haikumpasa kuwakata palepale na kuwaambia hiki kitu hakipo na michango isiendelee kwa jambo hili? Haya niambie GT mkuu
 
Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.

Mwakyembe nae hana jipya.Huku ni kujikosha tu kwani ni uobgo?mahakama imeogopa kuumbuka baada ya Tundu lissu kusoma vifungu vya sheria vinavyoibana mahakama ndio maana wamekanusha kuandika barua lakunu walukuwa wameandika,walichofanya ni ku withdraw ila mapambani yanaendelea
 
tufanye akili zetu kufikiri sawasawa,tusiongozwe na mawazo au hisia za mawazo ya wengine,tupambanue mambo kwa uhakika,ndio useme

Unafikiri ni kina nani hawafikiri sawasawa kati yako Mwakyembe na Werema?
 
Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.
hilo somo lake la mahakama tunalijua na tulifaulu kwa kiwango cha A....tunataka atufundishe somo la eskroo....namna alivyomshawish maswa kisha gavana wakachota pesa basiii hatuna shida na elimu ya mahakama kwa sasa
 
haihitaji kuwa na elimu kubwa sana kujua hili
+kama barua haikuwepo naibu spika alianzaje kuruhusu mjadala ule bungeni ?
Na vile vile ni kwa nini PM alimcaution Naibu Spika, Ndugai kuwa awe makini na maamuzi yake, ili maamuzi yake kuhusu ripoti ya CAG kujadiliwa bungeni kusije kuingilia mhimili wa mahakama, hadi bunge zima likamzomea, wakiwemo wabunge wa chama chake cha CCM?!
 
Umeona eeeeee.....moto umewawakia, wameona upepo hauelekei kwao. Sass huyo naye in my black book! Ama kweli Mungu ni Mungu, amewavuruga wasielewane,.....wautetee uovu, wajipake kinyesi wenyewe....na watanzani mazuzu ya ccm yawaone yenyewe!
 
Werema anadai atatenga siku kuzungumzia mahakama. Atazungumza lini na wapi, mana wiki ijayo tu kibarua kinaota nyasi.
 
[uQUOTE=jameskijalo;11196046]Nimnafiki mwakyembe yeye aripokuwambunge aripigakerere sana juu ya rechimond reo kapewamadaraka anajifanya ajuirorote
Duh!!!! Wewe umezidi, hizi r r r r zimezidi mno..[/QUOTE]
Huyo jamaa bila shaka atakuwa ametoka eneo moja na wale waliopata mgao mnono wa Escrow account, akina Maswiiii, yule Profesa aliyewaita wazawa kuwa hawana uwezo wa kuwekeza kwenye gesi, bali uwezo wao unaishia kwenye kutengeneza vijuisi, na yule mwanasheria mkubwa kabisa, aliyetishia kunyofoa shingo ya Kafulila na akamuita tumbili!
 
Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.
Aombe radhi PM kwa kuonyesha dalili kuwa kitu hicho kipo!
 
Si kejeli. Ubongo unahitaji oksijeni ili ufanye kazi yake, oksijeni haiwezi kuufikia ubongo bila kusafirishwa na damu, sumu iliingia kwenye mfumo wa damu... Unafikiri ubongo wake utakuwa salama? Utakuwa mtu wa ajabu sana kama unakerwa na ukweli.

Wewe ulimpima ubongo wake?
 
Safari hii waziri mkuu dhaifu hachomoki..

ktk vita hii serikali inafurushwa kwa mara nyingine..
wiki ijayo natangazwa kuwa waziri mkuu mupya kabisa
 
Barua ilikuwepo ila mijadala ndio iliyoficha barua, Lissu amehoji barua iletwa ijadiliwe ajulikane nani kaandika hapo ndo palikua pazito na ikabidi bunge libadilishe upepo na waseme hakuna barua kutoka mahakamani
 
Safari hii waziri mkuu dhaifu hachomoki..

ktk vita hii serikali inafurushwa kwa mara nyingine..
wiki ijayo natangazwa kuwa waziri mkuu mupya kabisa

Nasikia wanahangaika sana kujinasua.
 
Hawa akina Malyafyale (Si Mwakwembe wala Mwandosya) siku hizi wamekuwa watu wa hovyo kupindukia. Hata sijui kuwa hizi ndio athari za ule ulimbo wa sumu uliokuwa umewanasa kuwa ndio unawazuzua. Au sijui nini kingine kitakuwa kimewasibu?

Yaani wana wahuzunisha na kuwavunja moyo WaTanzania kwa matendo yao ya kuwahujumu watu waliowapigania kwa dhati na mapenzi mema dhidi ya watu waliokuwa tayari kuwatoa roho. Lakini, tazama leo ndio wamegeuka kuwa madalali na wasemaji wa wadhalimu (watesi) wao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom