Hayo yamesemwa na Waziri Mwakyembe wakati akihitimisha azimio la bunge alilowasilisha. Amesema kitendo cha wabunge kuishambulia mahakama ambayo ni muhimili mwingne hakikustahili na hata yaliyosemwa juu ya mahakama hayana ukweli. Kwan mahakama haijaleta barua kuzuia mjadala wa Escrow. Pia, amemsifia Werema kuwa ni AG makini kwa 100%. Mh. Werema naye kakoment kwa kusema ametenga siku atazungumzia suala la mahakama.
Leo ndio nimeamini JF
hakuna GT, yaan kwa kumlaum mtu ambaye anawaeleza kuwa Bunge
limekurupuka kuishambulia Mahakama kwa tuhuma hewa mnamponda, kwa
ufahamu wangu taasisi zote za umma hufanya kazi kwa Maandishi na siyo
uvumi,sasa Bunge letu limeamua kufanya kz kazi kwa kuhisi, kama Mahakama
ingetuma barua bungeni si ingeoneshwa kwa Wabunge, ebu tujaribu kutumia
akili japo darasa la tatu tu kuliko kutoa lugha za kuudhi km
kumshambulia Mwakyembe kuwa sumu imemuathiri Ubongo. Si busara hata
kidogo!
Si kuna uwezekano
pia pengine barua hiyo ilikuepo walipoona wabunge wamechechemaa sana
kuhusu mahakama kuingilia bunge mihimili hiyo mitatu ikaamua kuiondoa
kwa kuwa bahati nzuri ilikua haijawasilishwa bungeni?